Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa semina ya siku mbili kwa
makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuhusu maboresho ya timu
ya Taifa (Taifa Stars).
Semina
hiyo inafanyika ukumbi wa Singida Motel, mjini Singida kuanzia kesho
(Januari 18 mwaka huu) ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kwa
washiriki kuhusu maboresho hayo.
TFF
imeandaa mpango wa maboresho kwa Taifa Stars ambapo pamoja na mambo
mengine umepanga kusaka vipaji nchini nzima kwa lengo la kupanua wigo wa
kupata wachezaji wanaoweza kuchezea timu hiyo.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager mwaka huu inakabiliwa
na mechi za mchujo za Kombe la Afrika (AFCON) ambalo fainali zake
zitafanyika mwakani nchini Morocco.
Mechi hizo za mchujo zitachezwa kati ya Septemba na Novemba mwaka huu ili kupata timu 16 zitakazofuzu kucheza fainali hizo.
No comments:
Post a Comment