Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema
shirikisho lake limepanga malengo ya muda mfupi na mrefu ikiwa na sehemu ya
mkakati wa kuendeleza na kuinua kiwango cha mchezo huo nchini.
Malinzi
ameeleza mikakati hiyo ya uongozi wake leo (Januari 20 mwaka huu) wakati
alipomtembelea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ofisini kwake jijini Dar es
Salaam.
Amesema
uongozi wake umepanga malengo hayo ikiwemo kuandaa mashindano maalumu ya
kutafuta vipaji mikoani ili kuondokana na mtindo wa timu ya Taifa (Taifa Stars)
kuundwa na wachezaji kutoka katika klabu chache tu.
Kwa
upande wake Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli ameelezea matumaini yake
kwa uongozi mpya wa TFF katika kuunga mkono juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika
kuimarisha na kuinyayua Tanzania katika ramani ya mpira wa miguu duniani.
CAPTION:
Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani
Edward Lowassa ambapo alimwelezea mikakati ya shirikisho lake katika kuinua
kiwango cha mpira wa miguu Tanzania. Mkutano huo umefanyika leo (Januari 20
mwaka huu) ofisini kwa Lowassa jijini Dar es Salaam.
Halafu iweje?mbona tangu achaguliwe hajakwenda kumweleza rais wala waziri wa michezo hiyo mikakati?ameanza kuingiza siasa kwenye mpira na haya ni maandalizi ya kumpigia kampeni Lowasa kupitia TFF,kama alivyofanya makanisani,misikitini na bodaboda.Ndio maana alikuwa wa kwanza kumpongeza Malinzi.Baada ya hapo tutashuhudia akialikwa kuwa mgeni wa heshima kwenye mechi kubwa kubwa zikiwemo za timu ya taifa
ReplyDeleteAfu huyu mng'ang'ania urais na michezo wapi na wapi jamani! Kweli tutayaona mengi mpaka 2015 October ipite
ReplyDelete