KANUNI YA 24
KUVURUGA MCHEZO
1. Wachezaji na
viongozi wa timu itakayosababisha mchezo kuvurugika na hatimaye kuvunjwa,
itapoteza mchezo huo hata kama ilikuwa inaongoza kwa magoli na timu pinzani
itapewa ushindi wa pointi tatu na magoli matatu, iwapo timu pinzani inaongoza
kwa magoli zaidi ya matatu, itabakia na idadi ya magoli hayo iliyokwishafunga.
2. Magoli
yaliyofungwa na wachezaji wa timu iliyosababisha mchezo kuvunjika yatafutwa
lakini magoli yaliyofungwa na timu pinzani hayatofutwa na yataendelea kuonekana
katika idadi ya magoli yaliyofungwa na wachezaji wa timu hiyo wakati wa
kutafuta mfungaji bora.
3. Endapo
itatokea vurugu ya aina yoyote ile na kusababisha mchezo kusimama, mwamuzi atasubiri
kwa dakika zisizozidi kumi na tano, na endapo hali ya vurugu bado inaendelea
mwamuzi atavunja mchezo na kuwasilisha taarifa ya mchezo kwa kamati ya
Usimamizi ya ngazi husika.
4. Timu iliyosababisha vurugu itapoteza mapato
yote ya mchezo.
5. Timu
iliyosababisha kuvurugika kwa mchezo italipa faini ya shilingi 300,000/=.
3.
Faini hiyo italipwa kabla ya mchezo unaofuatia.
4.
Mchezaji/wachezaji na kiongozi/viongozi watakao bainika
kusababisha vurugu zilizopelekea mchezo huo kuvunjika watafungiwa kujihusiha
namasuala yote ya mpira kwa kipindi cha miaka mitano.
5.
Endapo uvunjikaji
wa mchezo utakuwa nje ya kanuni ya 22(3), mchezo huo utarudiwa kama inavyoainishwa
katika kanuni ya 9(e) na utachezeshwa na waamuzi wengine katika siku itakayo
pangwa na chombo husika.
Hays ndio soka la bongo
ReplyDeleteHi Shaffi, kwanza nikupongeze kwa hili. binafsi niliiyona hiyo clip kwenye local tv mmoja ya hapa nchi last week. niliamua kutuma messgae kwenye kipindi chenu bora kabisa cha michezo cha sports extra, unfortunately hiukusomwa. Shaffi, hao TFF waache ubabaishaji, its clearly seen on that clip JKT ndiyo walikuwa wameanzisha hizo vurugu, refa ikabidi naye ajitetee kama binadamu. sasa hili swala la mechi kurudiwa linatoka wapi? tena hao walionzisha vurugu wanaonekana waziwazi kwanini wasichukuliwa hatua, Jeuri hiyo wameleta kwakuwa wao ni JTK je wangekuwa JWTZ si wangeua kabisaa. Mwisho nikupongeze wewe wa team yako nzima kwanye kwa kufichuwa uozo uliokuwepo kwanye michezo, keep it up....tupo pamoja, Happy new year. Ray
ReplyDelete