Search This Blog

Wednesday, December 4, 2013

MAN UTD VS EVERTON: TOFFES WALIO KWENYE FOMU NA UNITED WALIO NA MWANZO MBAYA KULIKO YOTE KATIKA HISTORIA YA EPL.


Manchester United – wapo katika kipindi cha mapito kuelekea mbele au wanaurid nyuma kimaendeleo ya kisoka? 

Yote mawili yanaweza kuwa majibu yanayotokana na mjadala ulioanza tangu David Moyes aliporithi timu kutoka kwa Sir Alex Ferguson mwezi wa tano mwaka huu.

Kitu pekee ambacho mpaka sasa hakiwezi kuwa na mjadala ni kwamba mpaka kufikia mwezi December, United wapo katika nafasi ya chini kabisa kwenye msimamo wa ligi katika historia ya klabu hiyo ndani ya Premier League.

Tofauti na miaka mingine iliyopita United sasa wanaingia katika kipindi cha winter wakiwa wametulia kwenye nafasi ya nane kwenye ligi. 


Vitabu vya rekodi vinatuambia kwamba hawatoweza kutetea ubingwa wao kutokana na nafasi waliyonayo sasa.

Katika msimu wa michezo 38, hakuna timu iliyowahi kuingia mwezi 12 ikiwa inashika nafasi chini ya tano imewahi kuja kuchukua ubingwa mwishoni mwa msimu.

Katika miaka 21 tangu mfumo wa ligi kuu ya England ubadilishwe, washindi wa kombe 15 walitoka kwenye nafasi mbili za juu mpaka kufikia mwezi Disemba.

Kwa rekodi hii, inaonyesha wazi ni vigumu kwa Bwana Moyes kuanza msimu wake wa kwanza na ubingwa ndani ya Old Trafford.

Presha kubwa iliyopo kwa Moyes sasa ni kuweza kuiwezesha United kupata nafasi ya kushiriki kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya.

Ikiwa United itashindwa kufuzu kucheza Champions League msimu ujao, litakuwa ni pigo kubwa kwa klabu hiyo hasa kibiashara.

Hawajawahi kushindwa kumaliza katika nafasi tatu za juu katika wakati wa  Premier League, hii ni wakati wote wa utawala wa kocha Sir Alex Ferguson.

Lakini kabla hatujazama katika takwimu za Niagara, soka ni mchezo ambao hauna mahusiano mazuri na utabiri - lolote linaweza kutokea, na usiku wa leo, masaa kadhaa kutoka United wanakutana na Everton - ukurasa mwingine unaweza kuandikwa. 
Rekodi ya United katika Premier League tangu mwaka 1992. Kutoka August mpaka December
Everton hawajawahi kuifunga Manchester United katika dimba la Old Trafford, ila kwa fomu waliyonayo leo lolote linaweza kutokea.

Utakuwa ni usiku wa kipekee kwa David Moyes na Phil Neville na Maroune Fellaini wakati watakapokutana na timu ambayo wameitumikia kwa muda fulani ndani ya maisha yao ya soka.

No comments:

Post a Comment