KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel imemtangaza Rashid Kagomola, mkazi wa Bukoba mkoani Kagera kama mshindi wa tiketi mbili na safari iliyolipiwa ya kwenda kuangalia moja kwa moja (live) mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza katika uwanja wa Old Trafford.
Kagomola alishinda safari hiyo
wakati wa droo ya kila wiki ya promosheni ya ‘Mimi Ni Bingwa’ inayolenga
kuwazawadia wateja waaminifu, iliyoingia katika wiki ya pili.
Anakuwa mshindi wa pili wa tiketi
baada ya Dickson Lyatuu kutoka mkoani Arusha, kuibuka mshindi wa kwanza.
Akitangaza mshindi wa tiketi hiyo
katika wiki ya pili, washindi wawili wa shilingi milioni 5 na washindi wanne wa
shilingi milioni moja kila mmoja, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson
Mmbando alisema washindi wote wa tiketi watapewa nafasi ya kuchagua mtu mmoja
watakaesafiri nae kwenda Uingereza, kuangalia mechi ya Manchester United katika
uwanja wa Old Trafford.
“Tunafuraha kutangaza kuwa mshindi
wetu wa tiketi ya kweneda Old Trafford wa droo yetu ya pili ya promosheni ya
‘Mimi Ni Bingwa’ kuwa ni Rashid Jacob Kagomola atakaeungana na Bw. Dickson
Lyatuu aliyeshinda tiketi ya kwanza na wengine 11 watakaojishindia tiketi
baadae kwenda kuangalia mechi moja kwa moja (live) katika uwanja wa Old
Trafford katika mwezi huu wa kwanza wa droo yetu.
“Kagomola alichaguliwa baada ya
namba ya mtu wa kwanza kujitokeza, kushindwa kupokea simu baada ya kumpigia
mara tatu. Kwa maana hiyo napenda kumuasa kila aliyejisajili katika droo hii
kujiweka tayari kupokea simu kutoka Airtel kwa sababu anaweza kuibuka mshindi,”
alisema Mmbando.
Aliwataja Godfrey David Msiu kutoka
Arusha na Junior Ashery Pesambili, mkazi wa Arusha mjini kuwa washindi wa
shilingi milioni tano kila mmoja wa wiki hii na wateja wengine wanne
waliojishindia shilingi milioni moja kila mmoja.
Mmbando alisema kuwa bado zawadi
nyingi zaidi kushindaniwa na kuongeza kuwa ili kushiriki katika promosheni hiyo
mteja anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) ukiwa na neon “BINGWA’ kwenda namba
15656.
Alisema kuwa Airtel pia imeweka
vituo maalum kwa ajili ya wapenzi wa Man U kuangalia mechi za Manchester United
bure kupitia luninga kubwa, na kuyataja maeneo hayo kuwa, Mbeya – Shaba Pub,
Mwanza – Shooters Pub, Dodoma – Four Ways, Dar es Salaam – Rose Garden,
Morogoro – Nyumbani Lounge na mkoani Arusha ni Empire Sports Bar.
Droo hiyo ilishuhudiwa na
wawakilishi kutoka katika Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, (Katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kumtangazi Rashid Jacob Kagomola, mkaazi wa Bukoba mkoani Kagera, kama mshindi wa pili wa tiketi mbili na safari ya kwenda kuangalia mechi ya klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) nchini Uingereza kwenye uwanja wa Old Trafford wakati wa droo ya wiki ya pili ya ‘Mimi Ni Bingwa’ iliyochezeshwa jana. Kulia ni Ofisa Huduma Kwa Wateja Airtel Pamela Marinyo na Emmanuel Ndaki, Msimamizi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, (Katikati) akimpigia simu Rashid Jacob Kagomola, mkaazi wa Bukoba mkoani Kagera, aliyeibuka mshindi wa pili wa tiketi mbili na safari ya kwenda kuangalia mechi ya klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) nchini Uingereza kwenye uwanja wa Old Trafford wakati wa droo ya wiki ya pili ya ‘Mimi Ni Bingwa’ iliyochezeshwa jana. Kulia ni Ofisa Huduma Kwa Wateja Airtel Pamela Marinyo na Emmanuel Ndaki, Msimamizi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, (Kusoto) akimpigia simu Rashid Jacob Kagomola, mkaazi wa Bukoba mkoani Kagera, aliyeibuka mshindi wa pili wa tiketi mbili na safari ya kwenda kuangalia mechi ya klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) nchini Uingereza kwenye uwanja wa Old Trafford wakati wa droo ya wiki ya pili ya ‘Mimi Ni Bingwa’ iliyochezeshwa jana. Kulia ni Ofisa Huduma Kwa Wateja Airtel Pamela Marinyo.
No comments:
Post a Comment