Search This Blog

Monday, December 23, 2013

HII NDIO TAARIFA RASMI YA KUFUKUZWA KOCHA WA YANGA ERNST BRANDTS




Uongozi wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.
Hatua ya Young Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili.
Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.
Young Africans SC imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.
Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.
Ikiwa Brandts ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida katika kila siku asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred Felix “Minziro”.
Ili kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote zitakapokamilika tutawajulisha.
Aidha uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.
Mwisho tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika mzunguko wa pili wa VPL.


Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti - Kamati ya Mashindano
Young Africans Sports Club.



DAR ES SALAAM
23 Disemba, 2013

11 comments:

  1. Bonanza limesaidia kweli yani kama c bonanza timu ingeumbuka mashindano ya kimataifa, lkn bonanza hilo hilo liliandikwa ktk blog ya wanajangwani kwa kichwa cha habari kikubwa "KESHO HATUMWI MTOTO DUKANI" matokeo yake watu wafukuzana jangwani, kazi ipo mnyama ametulia msimbazi anapumua,

    ReplyDelete
  2. unamfukuza kocha wakati timu inaongoza ligi? Yanga tulikuwa nafasi ya 9 akaifikisha mpaka hapo iliopo sasa na kuongoza halafu unasema hana lolote? Wewe bin kleb umecheza mpira wapi hata utoe tathmini ya kocha?

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli mpira wa Tanzania maisha hauta develop kwa mambo ya kipumbavu kama haya. Hii kufukuzwa kwa Brandts muda huu inaonesha Yanga wana poor board management and they dont even have a clue about managing a football club. Yaani mtu kaichukulisha Yanga ubingwa last season, na mwaka huu so far ni leader wa ligi halafu anafukuzwa!! kisa eti kafungwa na Simba kwenye mechi ilokua haina hata umuhimu kwao!! (apart from earning those 90+ millions).. Kwa mpango unavokwenda ndani ya club saivi nahisi haikuwa solution kumfukuza Brandts bali ni kumpa muda mpaka angalau mwisho wa msimu then take it from there.. All I can see now is that there are possibilities Yanga could get knocked out earlier in the African Champions League and struggle domestically due to this unnecessary changes of the tactical board.. We should wait and see what happens then!!

    ReplyDelete
  4. Da!,kweli hii ndio Tz.Yani nchi yetu ina maajabu ya peke yake.Kocha aliyefanya vizuri kwenye ligi na kuaribu tu kwenye mechi ya kirafik anafukuzwa.Only TANZANIA

    ReplyDelete
  5. Ingekua clabu za england znafukuza makocha kama tz.! Asenal wenga angekua amefukuzwa kwenye vlabu vingap!? Kwa mfumo huu soka la bongo kaz ipo. Juzjuz ilikua kwa watan wao leo jangwan. Haya 2subr kesho

    ReplyDelete
  6. kama ndo ivo wenger sikunyingi angekuwa amefukuzwa, mpira unahitaji uvumiluvu na pia kufungwa au sare ni sehemu ya mchezo wa mpira. hata timu iwe bora vipi, razima itafungwa tu.

    ReplyDelete
  7. kama ndo ivo wenger sikunyingi angekuwa amefukuzwa, mpira unahitaji uvumiluvu na pia kufungwa au sare ni sehemu ya mchezo wa mpira. hata timu iwe bora vipi, razima itafungwa tu.

    ReplyDelete
  8. ifike wakat tuwaige na wenzetu walioendelea kwani arsenal imepigwa vipigo vingap vya aibu lakin kocha bado yupo, yanga acheni ubabaishaji

    ReplyDelete