Search This Blog
Monday, December 23, 2013
BREAKING NEWS…..! HALI NI MBAYA…! LUNYAMILA ANAPUMULIA MASHINE HOSPITALI YA MWANANYAMALA.
WINGA wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Edibily Lunyamila leo hii asubuhi amekimbizwa katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kusumbuliwa na kifua na sasa anapumua kwa msaada wa mashine.
Mtandao huu ulifanikiwa kufika hospitalini hapo muda mfupi baada ya winga huyo kukimbizwa hospitalini hapo baada ya kuzidiwa tangu jana usiku akiwa nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es Salaam.
Shaffihdauda.com imemshuhudia Lunyamila akiwa amelala kitandani katika wodi ya wanaume namba namba 5 kitanda namba 16 katika hospitali hiyo ya rufaa ya Kinondoni.
Daktari Madirisha Pascal anayemuhudumia winga huyo wa zamani, Lunyamila anasumbuliwa na tatizo la kifua ambalo linamfanya ashindwe kupumua vizuri.
“Kama mnavyomuona anapumua kwa msaada wa mashine na bado tunaendelea kumfanyia uchunguzi ili kubaini nini kinachomsumbua zaidi,” alisema Pascal.
Mmoja wa ndugu wa Lunyamila, Lameck John alisema kwamba, mchezaji huyo wa zamani alianza kujisikia vibaya jana Jumapili na leo asubuhi hali yake ilibadilika ndipo walipomkimbiza hospitali.
Lunyamila alivyokuwa enzi anaichezea Yanga..
“Alianza kulalamika hawezi kupumua na kifua kinamsumbua pia mbavu zilikuwa zikimuuma, baada ya majibu ya vipimo tutajua kinachomsumbua zaidi,” alisema Lameck.
Kutokana na hali iliyoonekana hospitalini hapo, Lunyamila anahitaji huduma ya haraka ili kuweza kuokoa uhai wake kwani anapumulia mashine akiwa katika sehemu yenye joto kali hivyo anapambana na vitu vingi kwa wakati mmoja...
Taarifa za kiuchunguzi zilizofanywa na mwandishi wetu zimebaini Lunyamila anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo.
''Nilikuja jana hospitali ya mwananyaala ikagundulika moyo wangu umekuwa mkubwa,hivi sasa naenda muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi nikifika na kukutana na daktari nitakujulisha ''
ilipofika mchana wa leo mwandishi alipokea simu kutoka kwa Lunyamila akimwambia ameambiwa arejee tena hospitali ya Mwananyamala.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Pole sana edibily lunyamila mungu atakujaalia utapona 2 mkubwa!
ReplyDeleteUgua pole Lunyamila, Mungu akusaidie upone mapema.
ReplyDeletesijakipenda hicho kichwa cha habari na hizo picha!!! ungetoa taarifa kuwa jamaa anaumwa sana tungekuelewa kama hiv huwa sipendi kabisa....
ReplyDeletembona picha za mandela alivyokuwa hospital hamkuziweka humu...
jaribu kuheshimu vyenu...
U wil get wel soon our bro. God z wth u
ReplyDeletejamani naomba aione mrisho ngasa mwenziwe alikuwa star kuliko yy leo anapelekwa mwananyamala wodi ina joto sasa na ww ngasa mpira ikuisha na unaendekeza starehe utakuja kukuta kama mwenzio ambaye kwa jina lake alikuwa awe tajiri na awe india sio mwananyamala
ReplyDeleteSidhani kama una akili timamu mkuu, binadam kamilifu aliye na roho ya imani hawezi kuongea maneno haya wakati mtu anaumwa. We hv born different.
DeleteWe acha upumbavu kumtolea mfano mbaya Edilibily, hapa sio mahala pake.. Ni bora ungemtolea mfano baba yako aliyepunguzwa kazi ya ulinzi kiwanda cha KTM, pesa aliyopata akanunua kibanda Mbagala, kikalipuliwa na mabomu, kalipwa fidia nusu kala nyingine kanunua kiwanja Gongolamboto, mabomu yakakigeuza handaki akalipwa fidia kaenda kuwekeza DECI, upatu ukafungiwa sasa mnakaa kwa shemeji yako mume wa dadaako..
Deletewewe una akili mbaya sana unaonekana kwa mchango ulio toa hapo juu akili yako ni pungufu sana na ni hasara kwa taifa kuishi na watu kama wewe ni vyema usingekuwepo. mabaya uwaombeao wenzio yatakupata kuanzia sasa wewe uliemtakia mabaya ngassa na lunyamila. kuanza sasa mikosi itakuandama.
ReplyDeleteAcha ushamba wewe hizo Picha na kichwa habari lengo watu waamini ili wamsaidie wewe hata Mia ya msaada hutoi kazi lawama tu
ReplyDelete