Search This Blog

Monday, November 18, 2013

USAJILI WA ' MR. KAZINYINGI' YANGA, NA NANI ATAKAYEMPISHA DILUNGA KIKOSINI?




Kwa, Hassan Dilunga ilianza kama ndoto vile, Ndoto ambayo ilionesha dalili za kuwa kweli, ila mwisho wa siku ikaishia kuwa jinamizi. 
Na kwa mashabiki wa klabu ya Simba, matokeo hayakuwa kama walivyotaraji. Wengi walifikiri kuwa kiungo-mshambuliaji, Dilunga angekuwa mmoja wa wachezaji ambao wangesajiliwa na timu yao wakati wa dirisha la usajili wakati wa majira ya kiangazi, 2013. Matokeo yake majina ya wachezaji Sino Agustino, Ibrahim Twaha, Zahoro Pazzi ndiyo yalikuja kuthibitishwa kama wachezaji waliosajiliwa Simba.

Palipo na pesa ndiyo pajaapo watu, na usariti upo kwetu siku zote. Macho hupenda kutazama vitu vizuri, ila wakati mwingine vitu vibaya pia vinaweza kuonekana. Watu fulani wenye madaraka, ambao pia wana uwezo wa kipesa katika klabu ya Yanga wamekuwa hawakosekani katika mazoezi ya timu ya Taifa, ni hapo ndipo wamezoea kufanyia usajili wao. Usajili wa kiungo huyu wa Shooting ni mzuri. Nasema ni mzuri kama yatakuwa mapendekezo ya kocha kwa kuwa inawezekana alikuwa akihitaji huduma ya Dilunga,  sifikirii sana kuhusu hilo kwa kuwa tatizo la msingi la kikosi cha Yanga kwa wakati huu ni nafasi ya ulinzi wa kati, ila kama ni mapendekezo ya ' M

Si, usariti ambao ameufanya baada ya kutoka Shooting, bali maendeleo yake ya kiuchezaji, maslai, na ushindi wa mataji. Vyote hivi atavipata akiwa Yanga, japo pia Shooting alikuwa akithaminiwa, kwa ofa ya miaka mitatu Yanga ni jambo ambalo hasingeweza kuliacha lipite.

 KIUCHEZAJI...

Dilunga anataraji kupata upinzani mkali wa kuwania namba katika kikosi cha Yanga. Wakati alikuwa akicheza mara kwa mara katika timu yake ya zamani, kiungo huyo mwenye uwezo wa kucheza eneo la 
mbele la kiungo akitokea katikati, upande wa kulia ni mchezaji ambaye kiuchezaji anafanana kwa vitu vingi na Saimon Msuva. Wakati, Msuva akiwa hana uhakika wa kuanza mchezo tangu kurejea kwa Mrisho Ngassa, mshambuliaji aliyehamishiwa upande wa kiungo mshambuliaji Said Bahanunzi amejikuta mbali na uwezo wake aliouonesha wakati ule wa michuano ya Kagame Cup, 2012.

Dilunga, atacheza wapi na nani atakayempisha hilo lipo katika jitihada zake binafsi, anatakiwa kusahau yote kuhusu Shooting na kujiuliza inakuwaje wachezaji waliotamba timu nyingine wakishindwa kupata mafanikio Yanga. Frank Domayo ni mfano mzuri kwake, walicheza wote wakiwa timu ya vijana na mara aliposajiliwa Yanga, aluongeza umakini, kujituma, nidhamu, usikivu, na zaidi Domayo ni mchezaji mwenye tabia njema hadi sasa.

Kutoka Shooting hadi Yanga kwa mchezaji wa U21 ni kupiga hatua kubwa, ila wapo vijana ambao walishindwa kuhimili umaarufu na ukubwa wa timu hiyo wakajikuta wakipoteza kabisa uelekeo. Wengi walioshindwa kufanikiwa sana kwa kiwango cha juu cha mpira wetu japo walionekana ni wachezaji wazuri walimalizwa na kupenda sana kuvunja miiko ya mchezo wa soka. Ni wapi Dilunga atacheza na nani atakayempisha, Yanga?

   ANAKWENDA KUJIMALIZA?

Angetamba sana Simba kwa kuwa nafasi ya yeye kufanya hivyo ipo wazi, ila Simba walishindwa kumnasa miezi sita iliyopita kwa kigezo cha maslai, na sasa amekwenda Yanga mahali ambako tayari kuna rundo la wachezaji nyota. Haruna Niyonzima, Domayo, Msuva, Ngassa, hawa ndiyo viungo bora wa mashambulizi wa Yanga kwa muda wa mwaka mmoja chini ya kocha Ernie Brandts ambaye anapoteza michezo miwili tu na kutoa sare mara sita tangu alipoanza kuinoa timu hiyo, septemba mwaka jana.

Katika mfumo wa 4-4-2, Msuva na Niyonzima walitawala, aliporudi Ngassa timu imekuwa ikicheza mfumo wa 4-3-3, ambao mara nyingi uwapanga pamoja Athuman Idd ' Chuji', Domayo, na Niyonzima kama viungo, Hamis Kizza, Ngassa na Didier Kavumbagu katika safu ya mashambulizi na timu imekuwa ikivuna rundo la mabao. Wakati wachezaji kama Bahanunzi, Hussein Javu, Nizar Khalfan, Jerry Tegete, Salum Telela wakiwa katika benchi, Dilunga amekwenda kyuongeza namba.

 OMEGA SEME

Pengine huko aliko sasa kocha Kostadin Papic atakuwa akijiuliza imekuwaje kijana yule Yanga wakamruhusu aondoke?. ' Mr. Kazinyingi' bila shaka alifanya kazi yake, Telela, Omega na Chuji walikuwa viungo wakali wakicheza pamoja, ndiyo maana aliporudi Yanga na kukuta hawapo kikosini akawarudisha, ila sasa Omega hayupo na Domayo abafanya vizuri, bila shaka ni funzo kubwa kwa Dilunga na kujaribu kuepuka katika mlango aliotokea Omega japo alikuwa bora. Dilunga ndani ya Yanga, atacheza wapi na nani atakayempisha?. Ni usajili wa kocha, au ' Mtu mmoja anayejifanya anaweza kufanya kila kitu kwa usahihi' ? Bado nausubiri usajili wa ' Beki tano Yanga' . Namtaka ' libero' mwenye sifa za Lulanga Mapunda. 

No comments:

Post a Comment