KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts anatarajiwa kutua nchini Jumapili
Novemba 24 kusaini mkataba mpya wa kuitumikia timu hiyo katika mzunguko
wa pili.
Brandts amemaliza mkataba wa kuitumikia timu hiyo katika
mzunguko wa kwanza ambapo kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na uongozi wa
klabu hiyo kwa ajili ya kuingia mkataba mpya.
Akizungumza jijini
Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin
Kleb alisema, wameshamalizana na kocha hivyo wanasubili akitua tu nchini
Novemba 24 ndio wamsainishe mkataba mpya.
“Brandts anatarajia kutua
nchini Novema 24 ambapo ndipo likizo yake itakuwa imefikia tamati kwa
ajili ya kuja kukiandaa kikosi kwa ajili ya mzunguko wa pili.
“Mara tu atakapotua ndio tunaingianae mkataba mpya, hadi sasa hatujajua
tutamsainisha wa muda gani lakini usiozidi chini ya mwaka mmoja,” alisema Bin Kleb.
No comments:
Post a Comment