Search This Blog

Tuesday, November 5, 2013

TFF YATAKA ORODHA YA WALIOSAMEHEWA



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma waraka kwa vyama vya mpira wa miguu vya wilaya, mikoa na vyama shiriki kuvitaka kuwasilisha orodha ya wote waliofaidika na msamaha wa Oktoba 28 mwaka huu.

Oktoba 28 mwaka huu wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu baada ya uchaguzi, Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi alitoa msamaha kwa wote waliofungiwa kwa sababu mbalimbali.

Hata hivyo, msamaha huo hauwahusu waliofungiwa kutokana na makosa ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile haugusi adhabu zilizotolewa ndani ya klabu.

Vyama vya mikoa vinatakiwa kuhakikisha waraka huo unafika kwa wanachama wao (vyama vya mpira wa miguu vya wilaya). TFF inataka orodha ya wote waliofaidika na msamaha huo kwa ajili ya kumbukumbu zake (records).

2 comments:

  1. NDUGU WADAU NAHITAJI KUJUA KAMA ATHUMAN KAZI NAYE AMEACHIWA HURR TOKA KATKA KIFUNGO ALICHOKUWA AMEFUNGIWA AU LAH..

    ReplyDelete
  2. GREAT! JAPO ADHABU YENYEWE NI NDOGO,LAKIANI KWA KUANZIA SIO MBAYA! MTENGENEZE KANUNI KALI ZAIDI YA HIZI FAINI. AIENEI AKILINI ETI UHISI UMEONEWA UHARIBU MALI ISIYO KUHUSU. PALE MLIKUJA NA SIMU ZENU SURUALI NA MASHATI YENU MNGEHARIBU HIZO AU HATA KUJITOA UHAI WENU TUNGEJUA MUNA MACHUNGU KWELI, LAKINI KWA KILICHOFANYIKA NI UHUNI TU.
    HONGERA KAMATI YA LIGI KWA KILA ALIYETIMAMU HATOSITA KUWAPONGEZA.

    ReplyDelete