Mechi
za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinaanza kesho
(Novemba 6 mwaka huu) ambapo Ashanti United itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Taarifa zilizoifika blog hii zinasema bodi ya ligi imeipiga klabu ya Simba faini ya milioni 25 kutokana na vurugu zilizofanywa na mashabiki wa timu hiyo mara tu baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar.
Taarifa iliyolewa na mtendaji mkuu wa bodi hiyo ndugu Sillas Mwakibinga kwenda kwa katibu mkuu wa Simba imeitaka klabu hiyo kulipa pesa hizo kabla ya mchezo dhidi ya Ashanti.
Viingilio
katika mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili chini ya mwamuzi Andrew
Shamba kutoka Pwani ni sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Waamuzi
wasaidizi ni Abdallah Mkomwa na Rashid Abdallah wote kutoka Pwani wakati mezani
atakuwa Hamisi Chang’walu.
Mechi
nyingine za kesho ni JKT Ruvu Stars na Coastal Union (Uwanja wa Chamazi),
Kagera Sugar na Mgambo Shooting (Uwanja wa Kaitaba, Bukoba) na Ruvu Shooting na
Mtibwa Sugar (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Keshokutwa
(Novemba 7 mwaka huu) raundi ya 13 kumaliza mzunguko wa kwanza itakamilika kwa
mechi kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa kwa viingilio vya sh.
5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Azam
itakuwa mwenyeji wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi mjini Tabora utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Rhino Rangers na
Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
Novemba
7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa Tanzania
Prisons.
No comments:
Post a Comment