Search This Blog

Monday, November 25, 2013

RAGE SI HAILE SELASSIE I, KAMATI YOTE YA UTENDAJI ING'ATUKE SASA




Na Baraka Mbolembole

" Mimi bado ni mwenyekiti wa Simba" labda ni kutokana na ' Mzuka',
baada ya kushuhudia umati wa watu, hasa wale wapenzi wa Simba, wakiwa nje ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam. Akiongea huku akiwa na ' tabasamu', Mh. Ismail Aden Rage alishindilia ' Msumali' na
kuongeza; ' Kamati ya Utendaji ya klabu haina mamlaka ya kumsimamisha, Mwenyekiti'. Wakati huu ambao, Simba imetoka kupata muendelezo wa matokeo yasiyovutia ndani ya uwanja, katika utawala ni vurugu tupu. Rage

Wakati akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Palisadoes,
katika mji wa Kingstone, Jamaica, watu wapatao laki moja walikuwepo
uwanjani hapo kumpokea, ' Mgeni', Haile Selassie I, aliyekuwa Mfalme
wa Ethiopia. Ilikuwa, mwezi April, 1966. Wakati wa utoto wake, Haile
Selassie I, alikuwa akifahamika kwa jina la RasTafari. Wakati wa utoto
wake alionekana kijana mwenye maadili mema, utiifu, mwenye heshima na
juhudi, alikuwa muwajibikaji na tabia yake hiyo ikafanya watu wajenge
imani zaidi kuhusu yeye. Alipewa jina la ' Dejazmatch' lenye maana ya
' Kamanda wa lango', akiwa na miaka 13 tu.


Wakati shirikisho la soka nchini, TFF kupitia, ofisa habari ambaye
pia ana kaimu nafasi ya katibu mkuu, Boniface Wambura ilipothibitisha
kupokea barua ya kamati ya utendaji ya klabu ya Simba, yenye maelezo
ya kusimamishwa kwa muda wa zaidi miezi mitatu kwa mwenyekiti wao, Mh. Ismail Aden Rage, pia wakasema wamepokea barua ya kiongozi huyo wa Simba, akisema kuwa hatambui kusimamishwa huko na yeye bado ni
mwenyekiti halali wa klabu. Wakati, kamati ya utendaji ilisema kuwa
kwa mujibu katiba wanayo mamlaka ya kumsimisha, Rage. Kwa, ufanunuzi
wa aliyekuwa kaimu mwenyekiti wa kikao cha kamati ya utendaji
kilichomsimamisha, Rage, Ndg. Joseph Itagare, ilionekana wazi kuwa
wapo sahi

  RAGE ALITAKIWA KUJA NA HOJA

Kinachoendelea sasa ni nani ' mbabe' klabuni, uwajibikaji ni mdogo
huku utengano ukishika hatamu. Majibu ya Rage, yalikuwa mazuri kwa
kina-kikulacho, wapenzi ambao wanaweza kujipaka hata rangi za manjano
katika miili yao na kuishangilia Yanga wakati wa mchezo dhidi ya
Simba. Naamini, wakati huu Simba haitaji kuwa na wanachama, achana na
wapenzi zaidi ya 200 walioenda kumpokea, Rage uwanja wa ndege.
Msikilize, Aden Rage, kisha Mpuuze. Ni kinyonga.

Majuzi, TFF kupitia, rais wake, Ndg. Jamal Malinzi walitoa maagizo
rasmi ya kumtaka, Rage kuitisha mkutano wa wanachama. Nafikiri, TFF
iliwahi sana kuliingilia suala hili, na kulitolea maamuzi ambayo ni
mabaya kwa wakati huu. Kuonesha ' Ukubwa', Rage akawajibu siku moja
baadae kuwa hawezi kufanya jambo hilo kwa kushinikizwa na TFF, na
wakiendelea hatang'atuka kwa njia ya kujiuzulu. Ni, kweli Rage anaweza
kujiuzulu kwa hiari yake mwenyewe?. Msikilize, kisha Mpuuze. Mtu
Mkubwa, ni mwanafunzi. Rage anajifunza nini?. TFF, inatakiwa ifunge mdomo wake sasa, si kila mahali wanaweza kuingia na kusawazisha mambo. Simba inawahusu kweli, ila kwa sasa wakati wao bado. Ni wao ndiyo waliompatia nmguvu huyu mtu na kushindwa kufananua mambo ya msingi.

MAAMUZI YA BUSARA

Kamati ya Utendaji ya klabu ambayo ilifikia maamuzi ya kumsimamisha,
Rage kwa upande wao wanasema wameheshimu maamuzi na maagizo ya TFF, ila kutokana na tamko la Rage kupuuzia maagizo hayo watasubiri hadi siku 14 ambazo, TFF walitoa kwa Rage, kama mwenyekiti kuhakikisha anaitisha mkutano kisha ndiyo watatoa tamko la nini wanatakiwa kufanya. Kwa, maslai ya klabu umefika wakati wa kamati ya utendaji yote kujiuzulu, na pengine ili linaweza kuonesha thamani yao kwa
wanachama wengine, kuendelea kwao kuwepo madarakani ni sawa na
kuongeza mafuta ya petrol katika moto. Wanaweza kufanya kama
ilivyokuwa upande wa pili kwa watani wao Yanga, wakati wa utawala wa
Lyod Nchunga, Nchunga alikuwa ni king'ang'anizi ila baadae akakubali matokeo baada ya wajumbe wote wa kamati ya utebdaji kujiuzulu. Hii ndiyo busara pekee ambayo itaifanya Simba kuingia katika mkutano wa lazima wa wanachama wote. Vinginevyo ' filamu;' itaendelea kuchezwa.
Kwa nini, Rage hataki mkutano mkuu wa wanachama?. Kuna kazi bado anaifanya klabuni hapo huku akisaidiwa na wanasiasa fulani wakiongozwa na waziri mkuu wa zamani, pamoja na mmbunge wa jimbo moja la siasa nchini ambao ndiyo ' nguzo' ya wataka ' Simba Kampuni'. Kuna mengi yamejificha nyumas ya jeuri ya Rage, pengine mgogoro wa kuibadilisha katiba ya klabu unasukumwa na suala la Simba Kampuni. Kamati ya utendaji inatakiwa kusalenda sasa, ni hapo ndipo nguvu ya Rage itakwisha kwa kuwa kimamlaka, mwenyekiti wa klabnu hiyo anayo nafasi ya kufanya machaguo yake mawili ya wajumbe wa kamati ya utendaji, huku mmojawapo akitoka katika baraza la wazee wa klabu. Ila kwa muda wote huo, Rage hajawahi kumteua mjumbe kutoka baraza la wazee, hapo katiba atakuwa ameikiuka au inamlinda pia? Msikilize, Rage kisha Mpuuze. Muda utafika na ataondoka tu Simba kwa kuwa ameshindwa kuiunganisha klabu.

Jambo moja katika mambo yasiyo na maana ni kutangaza habari ya kosa
la ' Mtu Mdogo' kwa sababu tendo lake ni kama tendo la mwendawazimu
ambalo wenye akili timamu hawawezi ' Kulipenda'. Walaki, habari za
kosa la ' Mtu Mkubwa' ni wajibu kabisa kutangazwa katika jamii tena
kwa maandiko ya herufi kubwa na wino safi. Mtu mdogo hana nafasi
katika dunia hii ya kutenda jambo kubwa. Hivyo basi kutangaza kosa
lake si vyema, ikiwa makosa makubwa yamo katika jamii. ' Uharabu wa
dunia' huja kwa sababu ya makosa ya watu wakubwa, lakini makosa hayo
hufichwa kwa uangalifu mkubwa. Ni kinyume kikubwa kilichoje kwa
walimwenguni kwa kutukuza wahalifu wakubwa na kuaibisha watu masikini.

Tunadharau maji mengi yawezayo kudhuru na kulaumu kwa nguvu hoja za
msingi. Kama makosa ni chakula , basi , na tuambiwe kinavyoliwa. Huliwa
kwa sababu kinapendeza watu au kwa sababu ni adhabu kwa wale wasioweza kutenda jambo lenye maana?. Wakubwa wanafaidi, Wadogo wanadhulumiwa. Kosa la mtu mdogo kutangazwa si muhimu, Hasara yake ni kidogo. Kosa la mtu mkubwa ni wajibu kutangazwa kwa wino wa kuangaza. Haile Selassie I, apata tuzo 77 kutoka kila pembe ya dunia kutoka na busara zake, hekima zake, huruma yake, na uongozi wake bora uliotukuka. Ndiye kiongozi aliyeshinda tuzo nyingi zaidi katika historia ya kidunia, labda siku moja Ismail Aden Rage, anaweza kupewa heshima ya kiongozi bora zaidi kuwahi kuongoza Simba, Wale jamaa zangu waliokwenda kumpokea uwanja wa ndege, bila shaka waliingiza chochote katika mifuko yao ila si wanachama wa klabu wale. Suluhisho la yote kwa Simba sasa ni kamati ya utendaji kujiuzulu tu. Kuendelea nao kung'ang'ania ni sawa na kujiweka katika kundi moja la watu wenye m,aslai yao binafsi.
0714 08 43 08

1 comment:

  1. Hello, brother huu uongozi wa vilabu na TFF bado hawajajua nini tunataka, hawana hoja ni ubishani tuu mwenye sauti kuu ndo mshindi, wanakera sanaa.

    ReplyDelete