WAKATI
Yanga ikicheza na JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mashabiki
wake walikuwa wakifanya kitu kimoja cha ajabu kidogo kwani walikuwa
wakishangilia matukio yaliyokuwa yakitokea katika mchezo wa Azam FC na Mbeya
City kwenye Uwanja wa Chamazi Complex.
Wakati
Azam inapata bao la kwanza dakika ya 13, mashabiki wa Yanga walionekana
kushangilia kwa nguvu huku wakiamini Mbeya City itasawazisha, huku wakifuatilia
matangazo ya moja kwa moja ya mchezo huo kupitia vituo kadhaa vya redio,
mashabiki hao walilipuka kwa shangwe dakika ya 30 baada ya Mbeya City
kusawazisha.
Kuna
wakati mashabiki hao walikuwa wakishangilia mambo waliyokuwa wakiyasikia kutoka
Chamazi Complex hali iliyokuwa ikiwachanganya wachezaji wa Yanga na Oljoro
waliokuwa wakicheza kwenye Uwanja wa Taifa.
Furaha
ya mashabiki hao ilirudi tena baada ya Mbeya City kupata bao la pili na hata
Azam waliposawazisha ilikuwa ilikuwa vilevile. Hali hiyo kuna wakati ilikuwa
ikiwasumbua mashabiki wengine ambao hawakuwa wakifuatilia mchezo huo kupitia
redio ambao walikuwa wakijiuliza tukio lipi linashangiliwa Uwanja wa Taifa
wakati hali inaonekana ni ya kawaida.
Huku
Yanga ikiongoza kwa mabao 3-0 hadi dakika ya 85, na Azam na Mbeya City zikiwa
na matokeo ya sare pia mashabiki wa Yanga walionekana wakiomba dua zote matokeo
hayo yasibadilike ili timu yao ishike usukani wa Ligi Kuu ya Bara.
Hata
michezo hiyo miwili ilipisha mashabiki wa Yanag kwenye Uwanja wa Taifa na wale
waliokuwepo Uwanja wa Chamazi Complex, walionekana wakishangilia kwa nguvu kitu
ambacho awali hawakuwa wakikifikiria sana.
KIIZA ACHAFUA HALI YA HEWA
Yanga
ilipokwenda mapumziko haikurudi uwanjani na mshambuliaji wake, Hamis Kiiza na
nafasi yake ilichukuliwa na Jerry Tegete, lakini jambo la kushangaza Kiiza
hakuweza kurudi katika benchi badala yake alibadili sare zake na kupanda
jukwaani kufuatilia mchezo huo.
Kiiza
alikuwa ana mabao manane na kama leo angefunga mabao mawili tu angekuwa
amefikia Amisi Tambwe wa Simba ambaye ana mabao 10.
Mshambuliaji
huyo alishuka jukwaani mara baada ya mchezo huo na kwenda katika vyumba vya
kubadilishia nguo mara baada ya mchezo huo na alitoka chumbani humo akiwa
amefura kwa hasira huku akimuacha Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji akizungumza
na wachezaji wenzake na benchi la ufundi.
Mtandao
huu ulipomfuta Kiiza kumuuliza kulikoni kuondoka kabla ya wenzake na kukataa
kurudi katika benchi, alisema; “Niache sipo katika hali nzuri ya kuzungumza.”
Kiiza
alionekana akiwa na begi lake akiondoka kwa kasi kuelekea katika maegesho ya
magari uwanjani hapo.
No comments:
Post a Comment