Uchaguzi wa viongozi wa bodi ya ligi unataraji kufanyika
leo, ila kuna ubabaishaji mkubwa kwenye mchakato huu wa uchaguzi na kama
ingekuwa ni uwezo wangu basi ningelisimamisha zoezi hili mpaka pale taratibu
zitakapofuatwa.
Bodi hiyo ya ligi ni chombo kinachoundwa kwa ajili ya kuvisimamia
vilabu vya ligi kuu pamoja na vile vya ligi daraja la kwanza,cha ajabu ni
kwamba Raisi na makamu wa chombo hiki watachaguliwa
na vilabu 14 vya ligi kuu tu huku vilabu 24 vya ligi daraja la kwanza vikiwachagua
wajumbe wawili tu wa kuviwakilisha kwenye bodi hiyo.
Cha kustaajabisha ni kwamba vilabu vya ligi daraja la kwanza
havitashiriki kwenye mchakato wa kuwachagua raisi na makamu wa raisi wa bodi. Swali:
kama vilabu vya ligi daraja la kwanza havitashirikishwa kwenye mchakato wa kuwachagua Raisi na makamu
wake sasa iweje wawe viongozi wao?
Hili nalifananisha na mchakato wa uchaguzi mkuu wa nchi uwambie
wakazi wa jimbo fulani wana haki ya kumchagua mbunge wao ila hawana haki ya
kumchagua raisi na makamu wa nchi. Je kidemokrasia hili linawezekana ?.
Soka hapa kwetu ni kwa watu maalumu, kwahiyo watafanya kila njia ili wabaki wenyewe. Hii ni hatari sana kwa maendeleo ya soka letu.
ReplyDelete