Na Mwandishi Wetu
Mashabiki wa Simba na Yanga mjini Songea watamenyana vikali
katika michezo mbalimbali kupitia bonanza maalum la Nani Mtani Jembe
lililoandaliwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager litakalofanyika uwanja wa
Maji Maji mjini Songea Jumapili wikendi hii.
Mratibu wa bonanza hilo Amadeus Kalumuna, amesema kuwa
michezo mbalimbali ikiwemo soka bonanza la wachezaji saba kila upande, kuvuta
kamba, na pia mpira wa mezani maarufu kama fussball itapamba bonanza hilo.
Burudani mbalimbali pia zitapamba bonanza hilo zikiwemo burudani ya muziki
kutoka bendi ya Mastaa wa Kusini, kikundi cha sanaa cha Umoja Star au maarufu
kama “Manyoka”, wacheza show wa Chicharito Group pamoja na wasanii mbalimbali
wa muziki wa kizazi kipya wa mkoani Ruvuma.
Kalumuna pia amesema kuwa vilevile kuwa michezo mbalimbali
ya kujifurahisha kama vile kufukuza kuku wa kienyeji, kukimbia na gunia na
kupiga penati ukiwa umefungwa kitambaa usoni itapamba bonanza hilo ambalo ni la
kwanza kufanyika katika mkoa wa Ruvuma kupitia Nani Mtani Jembe. Kampeni hii ya
aina yake inatoa fursa ya kipekee kwa mashabiki hao kujumuika pamoja na
kuburudika na vile vile imeongeza chachu ya ushindani na utani wa jadi kati ya
mashabiki hao huku ikiwapa fursa ya kipekee kuonyesha mapenzi kwa timu zao.
Bonanza hilo linalotarajiwa kuanza saa tatu asubuhi ni
mwendelezo wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo ilizinduliwa Oktoba 2 na inafanyika nchi nzima ikiwashirikisha
mashabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga. Kupitia kampeni hiyo, Kilimanjaro
Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga kiasi cha shilingi
milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila timu inazo shilingi
milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema kuwa
mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa kushindana kwa kushiriki kwenye kampeni
hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata fedha nyingi zaidi ya timu
nyingine.
Akielezea namna ya kushiriki, Kavishe alisema kuwa mpaka
kila timu imetengewa shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa shindano hilo la
Nani Mtani Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga anachotakiwa kufanya ni
kununua bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo kwenye kizibo chake kuna namba
ya kushiriki.
Alisema baada ya shabiki kununua bia ya Kilimanjaro na kuona
namba ya kwenye kizibo, anachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani
na kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na jina la timu anayoshabikia kisha
anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye namba 15440.
Alisema baada ya shabiki kutuma namba hiyo, atakuwa
amepunguza shilingi 1,000 kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki aliyetuma
ujumbe huo ni wa Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi 1,000 kutoka
kwenye fungu la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa amepunguza
shilingi 1,000 kutoka kwa Simba.
Kwa mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa fedha
zinavyopungua kutoka Simba au Yanga yatangazwa kila siku hadi siku ya mwisho wa
shindano hilo Desemba 14, mwaka huu.
DAH! MTANI JEMBE HII AIBU Y MWAKA, ALISAWAZISHA COAST SEKUNDE YA MWISHO MKASHANGILIA NA KUDAI ILIKUWA SAWA, WAUNGWANA WAKATOKA KIMYAKINYA KWA JAPO ILIWAUMA. MKAPATA SARE NA TIMU YA WANANCHI MKAJIITA NYIE NDIO NAJEMBE, WAO WAKATOKA PASIPO BUGHUDH MTU. LEO LIMEWAFIKA MNANG'OA VITI ETI MMEONEWA! KIVIPI? WAKATI NYIE KWENU SARE MNASHANGILIAGA??
ReplyDeleteNILIHISI SIKU MOJA KUNGETOKEA UJINGA KAMA HUU MAANA HATA HUKO KWENYE SHINDANO MTANI JEMBE UNAONGOZA, SASA BASI ENDELEENI KUCHUKUA USHINDI HUKO ILA MKIJA UWANJANI VITI MTUACHIE KWANI HUO UWANJA UMEJENGWA SI KWA NIAMBA MTANI JEMBE USIFUNGWE NA HIVYO VITI VINAHUSIKAJE??. MMLITAKA NAFASI YA NNE AKAE NANI? MNADHANI MPIRA MANENO? HAYA KARIBUNI MSHUHUDIE 3 ZA WAZEE WA KAZI! MMTTANI JEMBEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE! LABDA MSUBIRI KIATU CHA DHAHABU ILA UBINGWA FULL NDOTO YA KICHAA.
NI MIMI NDUGU YENU ISMAIL ADEN RAGE, SIMBA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEE! HA! MMENUNA?