UCHAGUZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) 2013
ILANI YANGU YA UCHAGUZI
Utangulizi
Ndugu zangu,
Nianze kwa
kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema aliyetulinda na kutuwezesha kufika
hapa tulipo.
Tarehe 19
Novemba 2009 Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati anazindua ziara ya Kombe la FIFA
la dunia uwanja wa Taifa, Dar Es Salaam pamoja na mambo mengine alisema,
namnukuu:
‘‘Kwa
Watanzania wenzangu tuichukulie ziara ya Kombe la Dunia nchini mwetu kama ni
changamoto kubwa kwetu inayotutaka tufanye vizuri zaidi katika soka ili
tulingane na heshima hii tuliyopewa.
Hasa ni changamoto kwa viongozi wa soka wa ngazi zote pamoja na
wachezaji na wapenzi wa mpira wa miguu nchini.
Kuja kwa kombe hili ni deni kwetu na kulilipa kwetu sisi ni kuzinduka,
tuendeleze kiwango chetu cha soka nchini ili na sisi siku moja TUSHIRIKI FAINALI ZA KOMBE HILI (msisitizo ni wa
kwangu). Hili jambo linawezekana. Wapo wenzetu Afrika wameweza, kwa nini sisi
tusiweze? Wao ni watu kama sisi, maadam
wameweza na sisi tutaweza.
Lakini
ili tuweze hatuna budi kuiga mfano hususani waliyofanya wenzetu na
wanayoendelea kufanya kuendeleza mpira wa miguu. Twende tukajifunze kutoka kwao. Lakini hata kabla ya kwenda huko, yapo mambo
hatuna budi kuyafanya. Naomba nitaje
baadhi yake:
1. Tuimarishe Uongozi, utendaji na uendeshaji wa vilabu vya
mpira. Mchezaji hufundishwa kucheza
mpira katika Klabu yake. Hapo ndipo
hufundishwa maarifa ya kucheza mpira na vipaji kuendelezwa. Hebu tujiulize hali ya vilabu vyetu vya soka
ikoje. Je vinaongozwa vizuri? Vinaendeshwa vizuri? Jibu tunalijua sote kuwa ni hapana. Lazima suala hili tulitafakari kwa makini na
kulipatia jawabu. Tukishindwa kupata
jawabu muafaka na mambo yakaachwa kuendelea yalivyo, mpaka mwisho wa dunia
hatutakuwa tunasogea popote.
2. Tupate walimu wenye uzoefu kufundisha timu zetu. Hii ndiyo njia ya uhakika ya kukuza na
kuendeleza vipaji na hivyo kupata wachezaji bora.
3. Tuwekeze katika kuibua na kuendeleza vipaji vya
wachezaji toka umri mdogo. Vilabu viwe
na timu za watoto na vijana. TFF isaidie
kuanzishwa kwa shule za mchezo wa mpira wa miguu kwa watoto na vijana. Mashuleni wapatikane walimu wa michezo walio
wazuri kufundisha.
4. TFF ionekane zaidi ya ilivyo sasa katika mipango ya
kuendeleza soka mashuleni, vijijini, mitaani na vilabuni. TFF ikiwa na mipango na kuisimamia na
kuwabana wadau kuitekeleza itasaidia.
Vinginevyo TFF itabakia kusimamia Ligi Kuu, kutoa adhabu kwa wachezaji
na kusimamia timu ya Taifa. Hiyo
haitoshi.’’
Mwisho wa kunukuu.
Ndugu zangu wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, wadau na wapenzi wa mpira wa
Miguu Tanzania tujiulize kuanzia kipindi hicho cha 2009 hadi leo hii katika
haya maagizo ya Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete tumetekeleza yapi zaidi ya kuwa wasindikizaji katika medani ya
kimataifa? Kipindi chote cha miaka
minane iliyopita Serikali imetoa sapoti kubwa katika sekta ya mpira wa miguu
kwa kulipia walimu wa timu za Taifa na kuhimiza makampuni kama NMB,Serengeti
Breweries,Airtel,Coca Cola na sasa Tanzania Breweries kudhamini timu zetu za taifa na mashindano
mbali mbali,matunda yake yako wapi? Ndo kwanza tunazidi kuporomoka kwenye
viwango vya FIFA. Iweje miaka ya nyuma timu zetu za Taifa zilifanya vizuri
wakati zinaweka kambi Salvation Army, leo zinakaa hotel za nyota tatu mafanikio
mbona hatuyaoni? Kama TFF imeondolewa
gharama za kulipa makocha,kuweka timu kambini,kununua vifaa vya timu,dawa,posho,malazi
pamoja na usafiri wa timu iweje leo TFF ishindwe kutumia vyanzo vyake vya
mapato zikiwemo fedha toka FIFA na CAF kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza
programmu ya vijana ya kitaifa? Kwa mujibu wa mtandao wa FIFA kati ya mwaka
2008 na 2012 TFF imepokea toka FIFA msaada wa jumla ya dola za kimarekani
milioni moja na lake nane na nusu (yapata shilingi bilioni tatu za kitanzania),
hizi fedha zimefanyia nini? Kwa nini
timu za vijana hazina udhamini? Ipi timu yetu ya taifa iwe ya wanaume wakubwa (senior team) ,
wanawake au za vijana inayoweza leo hii kujivunia mafanikio? Iko wapi ligi ya wanawake? Katika hili
tusilaumu Chama cha mpira cha wanawake, wakiwezeshwa wanaweza.Tutapataje timu
mahiri ya Twiga stars bila ligi ya wanawake? Katika ngazi ya klabu, hasa
zinazoendeshwa kwa mfumo wa kijamii kama
Toto Africa, Coastal Union, Yanga, Simba,Mbeya City n.k. hadi leo hii pamoja na
rasilimali za vilabu hivi ni klabu ipi imeweza kusimamia na kujiendesha yenyewe
tokana na vyanzo vyake yenyewe? Tuendelee kujiuliza:
Ø
Ni walimu wangapi wa mpira tumewaendeleza
kufikia kiwango cha kukabidhiwa majukumu ya kufundisha Taifa Stars. Fursa za mafunzo tunazopewa na FIFA na CAF
tunazitumiaje? Je tumeweza kuwa na angalau kocha mmoja anayefundisha mpira nje ya
nchi kama ilivyo kwa akina Sam Timbe ( wa Uganda), James Sianga ( wa Kenya) Jack Chamangwana ( wa Malawi) na wengine ambao waliweza kufundisha mpira Tanzania kwa
ufanisi?
Ø
Ni refa gani tumemuendeleza akafikia kiwango cha
kuchezesha mashindano ya fainali za dunia au AFCON au Klabu bingwa ya
Africa? Refa wa mwisho kuchezesha
fainali za Mataifa Africa (AFCON) ni Omar Abdulkadir huko Burkina Faso mwaka
1998.
Ø
Ni program ipi ya vijana ya kuibua vipaji na
kuviendeleza tuliyo nayo? Wale vijana wa
Copa Cocacola 2007 waliopelekwa kwa mbwembwe Brazil waliishia wapi? Tuna rekodi
zao?Tunajua wako wapi na wanafanya nini? Na hawa walioshinda majuzi Afrika
Airtel Rising Stars tumewatangenezea program gani ya maendeleo?
Ø
Tunaelewa matatizo ya vilabu vya mpira hususani
uhaba wa vifaa na pesa za uendeshaji, je vilabu vyetu TFF inavisaidiaje katika
kuendeleza programu zao za vijana?Au kazi yetu ni kudai kila klabu iwe na timu
ya under 20 bila kujali gharama za uendeshaji wa timu hizi?
Ø
TFF hadi sasa imebuni, kusimamia na kutekeleza
program endelevu ipi ya kuendeleza soka mashuleni, vijijini, mitaani au
vilabuni? Au mpaka tusubiri Airtel
rising Star na Copa Cocacola? Siku wakubwa
hawa wakisusa itakuwaje?
Ø
Ziko wapi juhudi za kuhimiza upatikani wa vifaa
vya kufundishia mpira watoto (kama mipira size 3/4) pamoja na kuimarisha miradi ya kuendeleza vijana
?
Ø
Hivi timu zetu za Taifa zinatumia mfumo upi wa
uchezaji? Au kila kocha wa taifa
tunayemleta anakuja na mfumo wake? Wenzetu wameweza kubuni mifumo ya uchezaji
ya timu zao za Taifa na wameushirikisha katika mfumo wa ufundishaji wa watoto. Lini Mwalimu wetu wa Taifa alikaa na walimu wa
vilabu (angalau vya Premier League) ili kujadili ufundishwaji wa mpira nchini,
hii ikiwa ni pamoja na kujadili masuala yahusuyo mbinu, lishe, huduma za afya
na ukakamavu wa mwili? Hivi mchezaji
akitoka katika klabu yake ambako amezoea kula dona na maharage ukampeleka kambi
ya Timu ya Taifa akapewa prawns ,kuku na samaki kwa siku nne za kambi itamsaidia kumbadili
siha? Ng’ombe hanenepeshwi siku ya mnada.Uratibu
wa programu za vilabu ni muhimu.
Ø
Raha ya mpira ni kelele na hoi hoi za
mashabiki. Wataalam wa mpira wanasema
umoja wa mashabiki wa mpira ni sawa na mchezaji wa 12 uwanjani. Zipo timu ambazo kihistoria zilikuwa ni za kijamii
na zilihamasisha sana ligi ya Taifa, na kuiongeza hamasa na ushindani,Mbeya
City ni mashahidi. Leo hii ziko wapi timu kama Ushirika ya Moshi, Bandari ya
Mtwara, Kariakoo Lindi, Balimi Bukoba, Reli Kiboko ya vigogo, Kahama United,
Mirambo ya Tabora, Tukuyu Stars, Nyota Korogwe, African Sports ya Tanga,Ujenzi
Rukwa,Mji Mpwapwa n.k. TFF imefanya juhudi gani kufufua ushidani huu
kwa kushirikiana na vyama vya Mikoa na Wilaya?
Ø
Wapo wachezaji wastaafu waliojitolea kwa moyo
mmoja kuiletea heshima nchi yetu. Leo
hii tunasikia kina Alfonce Modest na Jellah Mtagwa wanalalamika hawana msaada,
na hao ndio wale waliojitolea hadharani kutoa kilio chao. TFF hadi leo hii imewahi kuandaa mpango gani endelevu
wa kuwasaidia wachezaji wastaafu? Shirikisho la mpira barani Afrika CAF
wameanzisha ISSA HAYATOU TRUST FUND kusaidia wachezaji wastaafu waishio katika
mazingira magumu,sisi tumechukua hatua gani katika hili?
Ø
Iweje mpake leo hakuna mashindano yoyote ya wanawake
ya kitaifa yawe ya ligi au ya mtoano,angalau kwa ngazi ya kanda ? TFF itawezaje kuibua vipaji vipya vya timu ya
taifa ya wanawake TWIGA Stars bila mashindano ya aina hii?
Ø
Vilabu vya mpira, hususani vya Ligi Kuu, vimegeuka
kuwa kisima cha watu kuchota fedha.
Haiyumkiniki vilabu ambavyo vinaweka timu kambini, kuihudumai kuanzia
malazi, posho, vifaa, madawa na usafiri mwisho wa mechi jumla ya pesa
wanayopewa inakuwa chini ya nusu ya
mapato yote ya mechi. Hayo maendeleo ya mpira ambayo yametakiwa
yaanzie ngazi ya vilabu yatapatikanaje? Vilabu vimegeuka vitega uchumi vya watu
wengine wakati vyenyewe vinataabika na kujiendesha kwa mateso makubwa.
Ya
kusema ni mengi, kwa leo tuishie hapa.
Nini matokeo ya hali hii? Takwimu hazidanganyi. Matokeo ya hali hii ni
timu za Taifa kushuka viwango katika orodha ya FIFA siku hadi siku. Viwango vya
timu za taifa vinapimwa kwa kuangalia uwiano wa matokeo ya timu ya wakubwa
(senior) pamoja na yale ya timu nyingine za vijana za nchi husika. Miaka ya
mwanzo ya tisini tulishawahi kupanda hadi nafasi ya 65, leo hii kila kukicha
tuko kwenye 120.Kuporomoka huku kutaendelea hadi lini?
Ndugu zangu, tujiulize wapi tumetoka, tuko wapi na tunataka kuelekea
wapi? Jibu ni rahisi, kama alivyoagiza
Mh Rais Kikwete,tujipange upya, tubuni mkakati wa uendelezaji wa mpira, tuandae
program endelevu yenye malengo
yanayopimika na kwa pamoja tukishirikiana na Serikali, FIFA CAF na CECAFA,Halmashauri, Taasisi zisizo za
kiserikali, Sekta binafsi, Vyombo vya habari na wadau wengine wote wa mpira wa
miguu tutaweza kufanya vizuri na kuifanya Tanzania isifike duniani kote. Katika kutimiza azma hii sharti tuanzie kwa
kuleta mabadiliko ya uongozi wa juu wa TFF, tupate kiongozi ambaye sio
sehemu ya mapungufu ya TFF,hakuna njia ya mkato.Mimi Jamal Emil Malinzi,nimejipima na ninaamini nina uwezo wa kutosha
wa kubuni, kuratibu na kusimamia mabadiliko haya nikiwa Rais wa TFF.
Ndugu zangu, siku zote si vyema kukosoa bila kueleza njia mbadala ya
kufuata ili kutatua tatizo. Hapa
tunazungumzia mpira wa miguu na namna ya kuunasua toka kwenye janga la kushuka kiwango na timu zetu za Taifa
kuendelea kugeuzwa kichwa cha mwenda wazimu ambacho hadi majuzi vibonde Gambia
wamejifunzia kunyoa.
Ili tuweze kuukwamua mpira wetu ni
vyema tukakumbushana kuwa ili mpira uendelee unahitaji vitu vinne:
- Vipaji;
- Walimu;
- Vifaa;
- Viwanja
1. Vipaji
Tanzania
ni nchi yenye watu zaidi ya milioni 44.
Nchi ya Cape Verde yenye watu 500,000 tu imeweza pamoja na uchache wake
kuvumbua vijana 11 ambao wameweza kuifikisha nchi yao fainali za Africa 2013
Afrika Kusini na majuzi nusura waende kombe la dunia kama sio tatizo la
utunzaji kumbukumbu. Sayansi ya uibuaji
vipaji (scouting) ni muhimu na si kila mtu anaijua. Watafutwe wanaoijua, watufanyie kazi ya
kutuibulia vipaji vipya, na katika hili ni sharti mpira wa ushindani uchezwe
nchini kote ili vipaji vionekane.
2. Walimu
Mpira
ni sayansi,mpira ni taaluma. Kipaji bila mwalimu wa kukiendeleza ni bure. Vijana mpira wanaanza kuucheza wakiwa wadogo
hususani wakiwa shule za msingi. Huko
ndiko Taifa linahitaji kusambaza walimu wenye taaluma ya kufundisha mpira ngazi
ya awali. Wakishakuzwa kimpira ni lazima wawepo walimu wa kutosha kuwaendeleza
ngazi ya wakubwa na Taifa. Leo hii Uingereza ina walimu 1100 wenye leseni daraja
A,Ujerumani wapo 5500 na Hispania
12,000,Tanzania tunaye mmoja tu,kwa mtaji huu tutafika kweli?Kwa mujibu wa
ripoti ya TFF nchi nzima ya Tanzania ina
walimu wa mpira wa madaraja yote elfu mbili tu na mia tano kati yao wako Dar es
salaam. Hawa walimu 2000 ndio wanategemewa wawafundishe mpira vijana wa
Kitanzania zaidi ya milioni kumi walio katika umri wa kufundishwa mpira!
3. Vifaa
Wachezaji,
walimu wa mpira, madaktari na waamuzi wote
wanahitaji vifaa vya msingi ili mpira uchezwe.
Nchini mwetu vijana walio wengi wanacheza pekupeku, jezi ni upande mmoja
kucheza kifua wazi, mpira ni wa kuviringisha matambara, refa anavaa suruali, filimbi
ni mluzi, magoli hayana nyavu, n.k. Hii
ndiyo hali halisi ya uchezwaji wa mpira maeneo mengi Tanzania hasa vijijini
ambako ndiko kunapaswa kuwa chimbuko kubwa la vipaji.
Gharama
za vifaa vya michezo ziko juu mno, mfano mpira mzuri unaofaa kuchezewa kwenye
ardhi ngumu (rough surface) bei yake ni shilingi laki tatu, shule ipi ya msingi
itaweza kuununua huu mpira? Kuna baadhi ya vyombo vya habari majuzi viliripoti
kuwa kuna mchezaji alifunga hat trick ngazi ya Ligi Taifa akanyimwa mpira kisa
ni wa thamani kubwa. Mamlaka husika, hasa za kodi zinapaswa kuliangalia hili,
ili upatikane unafuu katika bei za vifaa vya michezo maana karibia vyote
vinaagizwa toka nje. Lakini pia vifaa
vya michezo vya misaada vinavyopatikana kutokana na miradi mbalimbali ya TFF ni
juu ya TFF kuhakikisha vinafikishwa vijijini pia kupitia vyama vya mikoa na
wilaya.
- Viwanja
Wilayani Ngara mkoani Kagera kuna uwanja wa mpira unaitwa ‘’Uwanja wa
Changarawe’’ na ni kweli uwanja huo umejaa changarawe. Beki akikaba kwa mtindo wa kuteleza ardhini ‘sliding
tackle’ basi nyama ya paja anaiacha pale chini.
Hii ndiyo hali halisi ya viwanja vyetu vingi nchini, kama vipo ni vibovu
sana maana maeneo mengi viwanja vya mpira hakuna vimechukuliwa na wajanja
wachache na kugeuzwa makazi na majengo
ya biashara. Tunahitaji viwanja vyenye
ubora ili vijana wetu wafundishwe mpira wa kisasa kwa ufanisi, mpira wa kupiga
pasi ya chini. TFF kwa kushirikiana na
vyama vya Mikoa na Wilaya sharti wawe mstari wa mbele katika kulipigania hili.
AHADI YANGU
Endapo nitachaguliwa kuwa Rais wa TFF, kwa kushirikiana na viongozi wote
wa TFF kuanzia ngazi ya vilabu, Wilaya, Mikoa na Kamati ya Utendaji Taifa na
kwa kuhusisha kwa karibu Vyama vya kimataifa vya FIFA na CAF, Serikali, Halmashauri,Taasisi
zisizo za kiserikali, Vyombo vya habari, Sekta binafsi, Mashirika ya umma na
wadau wa mpira wa miguu Tanzania ninaahidi kuenzi mafanikio ya awamu inayomaliza muda
wake , kustawisha utulivu katika uendeshaji wa mpira, na kufanya jitihada za kubuni, kuboresha na kustawisha maendeleo
ya mpira wa miguu Tanzania. Jitihada kubwa zitawekwa kwenye maeneo makuu
yafuatayo:
1. Ufundi
(Technical)
1.1 Muundo wa Idara ya
Ufundi
Katiba
ya TFF imeainisha wazi kuwa TFF ndiye msimamizi mkuu wa mpira wa miguu
Tanzania, hivyo jukumu la kuleta maendeleo ya mchezo huu kwa kiasi kikubwa
linaiangukia TFF.Ni kwa msingi huu basi asilimia kubwa ya rasilimali za TFF
lazima iwekezwe katika kuleta maendeleo ya mpira. Kwa mfumo wetu wa uendeshaji, kichocheo kikuu
cha maendeleo ya mpira ni idara ya ufundi ya TFF. Hivyo idara hii ya ufundi inapaswa kuwa ndiyo
idara mama ya TFF ambayo inapaswa kuongoza kwa matumizi ya fedha, idadi ya
waajiriwa na matumizi ya rasilimali nyingine za TFF . Kwa sasa pale TFF hali sivyo ilivyo. Iwapo nitachaguliwa nitapendekeza jukumu la
kwanza la Kamati ya utendaji liwe ni kurekebisha na kuboresha mfumo wa
uendeshaji wa idara ya ufundi.
Nitapendekeza idara ya ufundi iendelee kuongozwa na Mkurugenzi wa Ufundi
na chini yake awe na wakurugenzi wasaidizi wa vitengo watatu Mkurugenzi Msaidizi
(ufundi), Mkurugenzi Msaidizi (Elimu na Mafunzo) ambaye kwa sasa anaitwa Education officer, na
Mkurugenzi Msaidizi (Maendeleo ya mpira).
Kitengo
cha Ufundi kitahusika na kubuni na kusimamia shughuli zote zinazohusu maendeleo
ya Timu za Taifa kuanzia za wakubwa hadi za vijana. Hii itakuwa ni pamoja na
kuandaa mitaala ya taifa (national football curriculum) ya ufundishaji wa mpira
Tanzania kuanzia umri wa miaka mitano
hadi watu wazima. Walimu wa Timu za Taifa wataripoti kwake.
Kitengo
cha Elimu na Mafunzo kitahusika na kubuni na kuratibu kozi zote na mafunzo yote
yanayohusiana na mpira kama vile kozi za Marefa, Makocha, Madaktari, Makamisaa,
Watawala, Waandishi wa Habari za Michezo, n.k.
Kitengo
cha Maendeleo ya mpira kitahusika na kubuni,kuratibu na kusimamia mpango wa maendeleo
ya vijana (grassroot) na kutafuta
vipaji (scouting). Kitengo hiki kitafanya kazi kwa kushirikiana kwa ukaribu na
idara za Serikali hasa idara za Elimu,Vijana na TAMISEMI, Halmashauri,Mashirika ya
umma,Sekta binafsi pamoja na Taasisi nyingine za kijamii.
Wakuu
wa vitengo hivi wataajiriwa kwa kufuata vigezo makini na bila upendeleo wala
kujuana.
1.2 Ujenzi wa Kituo cha Mpira (Football Centre of
excellency)
Hiki
ni Kituo Maalum cha mafunzo ya mpira wa miguu.
Katika kituo hiki kunakuwa na kila aina ya miundo mbinu, viwanja vya
kufundishia mpira, vituo vya tiba,madarasa ,maabara za utafiti,hosteli n.k Kituo hiki pia kinakuwa ndio sehemu kuu ya
kuweka kambi za timu za Taifa na kutoa mafunzo ya ufundi yakiwemo ya ukocha,
urefa, utawala na tiba. Wenzetu wa
Senegal na Ethiopia kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira Africa CAF wameweza
kujenga vituo hivi na matokeo yake tunayaona.Cameroon pia wana kituo hiki.
Pamoja
na gharama zake kuwa kubwa, cha muhimu hapa ni kuweka nia, kutafuta ardhi kwa
kushirikiana na Serikali na kuanza ujenzi taratibu.Kwa kuwa klabu ya Sunderland
ya Uingereza na kampuni ya kufua umeme ya Symbion wameonyesha nia ya
kushirikiana naSerikali kujenga kituo cha michezo itakuwa vyema iwapo TFF
itashirikiana na taasisi hizi muhimu ili kufikia azma ya kujenga kituo hiki cha
kisasa. Iwapo nitachaguliwa nitasimamia uanzishwaji wa mradi huu muhimu ikiwa
ni sehemu ya mkakati wa kulikomboa soka letu.
Aidha
uwanja wa Karume yalipo makao makuu ya TFF utazungushiwa jukwaa ili mechi
ambazo sio kubwa zifanyike pale, Hii itaiongezea TFF mapato na vilabu pia.
1.3 Timu
Kupanda Daraja
Ili
kuongeza ushindani na kupanua mpira uchezwe kona zote za nchini ( to spread the
game) ,mtindo wa kucheza kikanda ili kupata timu za kupanda daraja kuu utakuwa
ni wa kudumu na utaimarishwa kwa
kutafutiwa udhamini na kuboreshwa viwanja kwa kushirikiana na wamiliki wa
viwanja hivyo. Usimamizi wa mashindano ngazi hii utaimarishwa na kusimamiwa kwa
karibu zaidi ili timu itakayopanda daraja iwe imepanda kwa haki na hivyo kuleta
ushindani Ligi Kuu.
Hata
hivyo waraka uliotolewa na TFF ukiagiza mikoa ichezeshe ligi ili kupata bingwa
wa mkoa utafutwa kwa sababu hautekelezeki kutokana na hali ya uchumi na
uhalisia wa jiografia ya mikoa ya Tanzania.
Mathalani Mkoa wa Mtwara ukichezesha ligi ya mkoa (kwa maana ya nyumbani
na ugenini) ina maana bingwa wa Wilaya ya Masasi atasafiri vipi
akacheze Newala au Mkoani Lindi bingwa wa Liwale atasafiri vipi akacheze na bingwa
wa Kilwa , Pwani bingwa wa Mafia atasafiri kwa gharama za nani akacheze
Bagamoyo na wa Kibaha akacheze Utete? Pamoja na nia njema ya TFF uhalisia
hauruhusu. Kama Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Kagera nalijua hili, hakuna
haja ya TFF kuwa inatoa maelekezo ambayo hayatekelezeki, hasa ukizingatia kuwa
TFF hakuna msaada wanaopeleka kusaidia mikoa na wilaya ziandae mashindano yao.Vyama
vya mikoa na wilaya viachwe viendelee kutumia ubunifu wao kupata mabingwa wao
kulingana na hali halisi ya mazingira yao.
1.4 Kuanzisha mashindano
mapya na kufufua ya zamani
Wataalam
wa kandanda wanasema kuwa ili mchezaji awe katika kiwango bora inabidi acheze
kwa mwaka kimashindano wastani wa mechi 40.
Ligi yetu kuu,Vodacom premier league,inatoa fursa kwa mchezaji kucheza
michezo 26 kwa mwaka iwapo anapangwa kila mechi.Hii haitoshi. Namna pekee ya
kurekebisha hali hii ni kuongeza idadi ya mashindano kwa mwaka.Hili litafanyika
kwa kufufua kombe la Taifa (Taifa cup)
na kuanzisha kombe la shirikisho (kama FA cup ya Uingereza). Kombe la shirikisho
litashirikisha timu zote nchini kuanzia ngazi ya kata,tarafa,wilaya,mkoa hadi
Taifa na bingwa wake atawakilisha nchi
katika kombe la shirikisho la Afrika CAF confederation cup (kama ilivyo Kenya
kwa sasa).
1.5. Mpira wa Wanawake
Hadi
sasa hatuna mfumo imara na unaoeleweka wa kuendeleza soka la kinamama. Mpira wa wanawake umeanzia Wilaya ya
Kinondoni, ukakulia Wilaya ya Kinondoni na umegotea Wilaya ya Kinondoni ambako
kuna timu zenye majina kama Mburahati Queens na Sayari Queens. Mpira wa wanawake sharti usambae nchi nzima,
na ili kufanikisha azma hii lazima yaanzishwe mashindano ya kitaifa ya wanawake
ikiwemo Ligi ya taifa ya wanawake. Hii
itaendana na juhudi za kuongeza makocha, waamuzi na makamisaa wanawake na
kutafuta udhamini kwa timu ya Taifa ya wanawake TWIGA STARS.
1.6 Maandalizi ya Vijana
(Grassroot Programme)
Mpango
endelevu wa maendeleo ya soka la vijana sharti uandaliwe, uratibiwe na
kusimamiwa kwa makini. Program madhubuti
ya maendeleo ya mpira wa vijana lazima ibuniwe ,iratibiwe na kusimamiwa kwa
usatadi mkubwa.Mradi huu lazima ulenge ,kwa hatua,kufikia hatua ya kuingiza
timu zetu fainali za kombe la Afrika la vijana chini ya umri wa miaka 17 na
20,fainali za olimpiki, fainali za Afrika wachezaji wa ndani CHAN,fainali za
Afrika AFCON na mwisho fainali za kombe la dunia.Hii itakuwa ni pamoja na
kujiwekea utaratibu wa mzuri wa kuhakikisha vijana wetu wanapata fursa ya
kucheza mpira nje ya nchi ili kujiongezea umahiri.Na hii ni kwa wanawake na
wanaume.
Mpango
huu ni lazima ushirikishe Serikali Kuu (hasa Wizara zenye dhamana ya Michezo, Elimu
na Halmashauri), Taasisi zisizo za kiserikali,mashirika ya umma,sekta binafsi na
TFF,CAF na FIFA. Ushirikishwaji wa Serikali
na Halmashauri katika program hii ni muhimu sana kwa kuwa ndio wasimamizi na
wamiliki wa shule nyingi za msingi ambako ndiko vijana wetu wanakoanzia kucheza
mpira. Mpango kazi huu lazima uonyeshe:
1.
Nini tunataka kufanikisha.
2.
Utaratibu utakaotumika.
3.
Nguvu kazi inayotakiwa na sifa zake.
4.
Mwongozo wa kufuatilia kupima ufanisi wa programu.
5.
Kupambanua gharama za mpango na taratibu za uchangiaji
wake.
Hatua muhimu katika kufanikisha program hii zitakuwa ni:
-Kufundisha walimu wa walimu (instructors), hawa ndio watakuwa chachu ya
kupata walimu wa mpira mashuleni na mitaani.
-Walimu wa walimu (instructors) kufundisha walimu wa kutosha wa michezo
mashuleni na mitaani
-Kwa kushirikiana na wamiliki wa shule kuhakikisha viwanja vya kuchezea
vinakidhi viwango
-Kutafuta na kusambaza vifaa vya michezo mashuleni hasa mipira ya saizi
muafaka kwa mujibu wa viwango vya kimataifa.
-Kupata shule angalau moja kila mkoa itakayopokea watoto wenye vipaji
maalum vya kucheza mpira, pale ambapo wazazi hawataweza kuwalipia karo vijana
hawa basi TFF ihakikishe karo zao zinapatikana,huo ndio uwekezaji katika mpira.
-Kuandaa mashindano mbali mbali yatakayoshirikisha shule hizi ili kupata
timu za taifa za vijana wa umri mdogo wa kike na wa kiume.
-Kuhakikisha timu hizi za umri mdogo zinapata fursa ya kushiriki
mashindano mbali mbali ya kimataifa
- Kupata vikosi vizuri vya timu za taifa za vijana wa umri mdogo ambao
watakua pamoja, hao ndio watajenga msingi imara wa timu za Taifa za wakubwa kwa
miaka ya baadae.
Itakuwa ni muhimu sana program hii iendane vizuri na ratiba nyingine za
mashindano ya kitaifa kama Umitashumta, Umisseta, Airtel rising star, Copa Coca
Cola n.k.
-
Kuanzisha mashindano ya kitaifa ya kombaini za shule za
sekondari na ya kombaini za vyuo vikuu. Wachezaji mahiri wa timu ya taifa kama
Leodeger Chilla Tenga (Rais wa TFF) na Leopold Tasso Mkebezi (meneja wa Taifa
stars) waliibukia kwenye mashindano kama haya Mkebezi akiwa beki wa kombaini ya
sekondari za Bukoba,Ihungo,Kahororo na Nyakato.
Aidha
vituo vya michezo (sports academies) ambavyo tayari vipo vitatengenezewa utaratibu
wa usajili na kuwekewa utaribu wa kuviendesha.
Ili
kuondoa ulalamishi wa vituo vya mafunzo (Academies) kulalamikia malipo pindi
mchezaji akisajiliwa timu kubwa, vituo vyote vya vijana vitasajiliwa na vijana
wao wote wataingizwa kwenye kumbukumbu za TFF (data base) kwa majina, saini na
picha,hii itasaidia kuzuia sakata kama la Mbwana Samata na klabu yake ya utotoni
ya Mbagala maana kumbukumbu za TFF zitakuwa ndio jibu la maswali yote.
1.7 Tiba
1.
Tutaimarisha usalama uwanjani. Tutahimiza kila uwanja zinakochezwa mechi za
ligi kuwe na gari la wagonjwa na chumba cha dharura (emergency room).
Katika
kuimarisha usalama tutahakikisha vifaa muhimu vya dharura kama vifaa vya hewa
(oxygen) na vifaa vya kushtua moyo (defibulator) vinakuwepo. Kwa sasa hapa Tanzania uwanja pekee wenye
vifaa hivi ni Uwanja wa Azam Chamazi. Ni
jambo la kusikitisha kuona hata uwanja mpya wa Taifa hauna chumba cha tiba
dharura (emergency room) na kibaya zaidi makato ya uwanja hayaendi kuanzisha huduma hii
muhimu wakati viongozi mbalimbali wa kitaifa wanahudhuria mechi uwanjani.
2. Mradi wa Goal Project wa FIFA
unatoa pesa za tiba na
mradi huu uliweka lengo la kuwa na chumba cha kliniki pale uwanja wa Karume. Tutakifufua chumba hiki, tutakiwekea vifaa na
kuhakikisha huduma ya kliniki kwa wanamichezo iliyokuwa ikitolewa na madaktari kila
Jumapili inarudishwa. Posho itatafutwa
ili madaktari watoa huduma angalau wapate nauli na maji ya kunywa.
3. Wakati wa kujadiliana mikataba na wadhamini mbalimbali
tutahakikisha kipengele cha huduma za afya kinaingizwa katika mikataba.
Udhamini utatafutwa kwa ajili ya vipimo vya wachezaji kabla ya league (pre-league
medical test) kama vile vipimo vya uvumilivu (Yo-Yo test) na vipimo vya moyo
(cardiac tests). Hii ni kwa ajili ya usalama wa wachezaji na waamuzi.
4. Hadi leo chama cha Madaktari Tanzania, TASMA hakina
ofisi. Hii ni aibu kwa chama chenye
hadhi na umuhimu wa kipekee kama hiki.
Tutahakikisha TASMA inapata ofisi yake pamoja na chumba maalum cha
kliniki.
5. Huduma ya afya lazima iwe sehemu maalum ya mfumo wa
idara ya ufundi. Ni muhimu timu ya madaktari
wa Timu ya Taifa (National Medical team) ijulikane ni kina nani na wapewe mikataba
ya kazi. Hii tutalipigania.
6. Majeraha ya michezo huwa yanahitaji utaalam wake wa
tiba. Tutaiomba Serikali itupe
ushirikiano ili kipatikane kitengo maalum cha kutibu majeraha ya wanamichezo
(sports injuries wing) katika baadhi ya hospitali zetu wakati tunajiandaa kuwa
na kitengo cha tiba (Rehabilitation Centre) katika kituo cha michezo
kitakachojengwa.
7. Ili kuimarisha uwezo wa madaktari wetu kutoa huduma za
afya kwa wanamichezo, tutahakikisha madaktari wengi kadiri iwezekanavyo wanapata
kozi za msingi,kati na juu (preliminary,intermediate and advanced). Nafasi hizi
zitatolewa bila upendeleo wala kujuana.
- Utoaji wa ushauri nasaha kwa wachezaji utaongezeka hasa
kuhusu masuala ya ukimwi na madhara ya madawa ya kuongeza nguvu na ya
kulevya.
1.8 Waamuzi
Imepita miaka zaidi ya 15 toka Tanzania itoe mwamuzi wa kimataifa wa
kuchezesha fainali kubwa (mara ya mwisho AFCON 1998), hii si sawa. Utaratibu
uliopo sasa wa kuwapata na kuwaendeleza waamuzi ama una mapungufu au haufai
kabisa hivyo budi utafutwe utaratibu ulio mzuri zaidi katika kupata waamuzi
bora, tafiti zitafanywa ili kubaini ni njia zipi za kisayansi za kuwapata
waamuzi bora (Top referees).Semina za mara kwa mara za CAF na FIFA ni nzuri
lakini hazitoshi, TFF lazima iwekeze kwa kutoa mafunzo zaidi ya waamuzi kwa
gharama zake.
Aidha mradi wa maendeleo ya mpira kwa vijana (grassroot) utahusisha pia
mafunzo ya uamuzi wa mpira kwa vijana kama kinavyofanya kituo cha Jenerali Twalipo.
Utaratibu wa kutoa adhabu kwa waamuzi wanaosemekana wameboronga uwanjani
nao unahitaji marekebisho ya haraka sana. Uamuzi wa mpira ni taaluma kama
zilivyo taaluma nyingine,mwamuzi akikosea ni vyema akakosolewa na mwamuzi
mwenzie ambaye ni mwandamizi,na kama ni kuadhibiwa aadhibiwe na jopo la waamuzi
wenzie waandamizi lakini wastaafu na sio mtu mwingine ambaye hajawahi kupuliza
filimbi.
1.9 Makocha
Kumekuweko
na utamaduni usiofaa katika soka la Tanzania miaka ya karibuni wa kuona kuwa
makocha wa kigeni ndio bora zaidi na wanastahili mikataba,mishahara minono na
marupurupu ilhali makocha wazawa wanageuzwa ‘deiwaka’, jambo hili ni baya
sana,ajira ziheshimiwe kwa msingi wa taaluma na sio kwa msingi wa nchi atokayo
mtu.
Makocha
wetu wazalendo wana uwezo mkubwa kama wakipewa nyenzo kama wanazopatiwa wageni,
kama malipo mazuri, mikataba ya muda mrefu, vitendea kazi na kuheshimiwa
program zao bila kuingiliwa na viongozi.Iwapo nitachaguliwa ninaahidi:
- Kuwaendeleza
makocha kimafunzo ndani na nje ya nchi kwa wale wenye uwezo na utashi wa
kufanya hivyo.
- Kushawishi
taasisi za elimu nchini kama vyuo vikuu kufundisha taaluma ya ukocha
- Kuhakikisha
walimu wa mpira wa timu zetu za Taifa wanakuwa na mikataba stahiki, hii ni
pamoja na benchi zima la ufundi.
- Kuwajengea
uwezo makocha wetu wazalendo ili nao wapate fursa ya kufundisha mpira nje ya
nchi.
- Kuanzisha
tuzo za kila mwaka za makocha wazalendo ambao wamefanya vizuri katika
ufundishaji wa soka la vijana la wanawake na wanaume.
- Kuhakikisha
utaratibu wa leseni za CAF unazingatia vigezo vya kitaaluma, uzoefu na ushiriki
wa kocha mhusika katika ufundishaji. Makocha ambao wanafundisha (active
coaches) watapewa kipaumbele katika kupata kozi za kupanda madaraja kuliko wale
wanaofungia vyeti makabatini.Leseni za CAF ni muhimu katika kumfanya mwalimu wa
mpira atambulike kimataifa.
- Kuhakikisha
kanuni za ligi zinasimamiwa vyema ikiwemo kanuni itakayomlazimisha kila mwalimu
wa ligi kuu na daraja la kwanza awe mwanachama wa TAFCA (chama cha makocha
nchini), walimu wa kigeni watapewa uanachama wa muda.
1.10 Timu za Taifa
Timu
zetu za Taifa, ziwe za wakubwa au za vijana ndio kioo cha mpira wa Tanzania. Jitihada zote lazima zifanyike kuhakikisha
tunakuwa na timu nzuri za Taifa kuanzia za wakubwa (wanawake/wanaume) hadi za
vijana. Pamoja na jitihada
zitakazofanyika kuboresha idara ya ufundi kama ilivyoanishwa hapo juu lakini
pia yafuatayo ni mambo ya ziada yatakayofanyika.
(a) Kuandaa fainali za Afrika za umri chini ya
miaka 17 (U-17) mwaka 2019
Hadi sasa hakuna nchi ambayo imekwisha pata uenyeji wa mashindano haya. Uenyeji
huu unatolewa na Shirikisho la vyama vya mpira Afrika CAF.Hii ni changamoto
kwetu Watanzania kuomba uenyeji huu.Tukipewa fursa hii itatusaidia sana
kutusukuma tuanze kuandaa programu ya nguvu ya miaka mitano ya kupata timu yetu
itakayocheza katika fainali hizi kama wenyeji.
Aidha kama nchi tutalazimika kuboresha miundo mbinu yetu hususani
viwanja vyetu vya mpira, jambo ambalo litatusaidia siku za usoni. Ninaamini uwezo wa kuandaa mashindano haya
kama nchi tunao. Nikichaguliwa nitalisimamia hili.
(b) Nidhamu
TFF itaandaa Kanuni za Nidhamu (code of ethics) kwa wachezaji, walimu na
viongozi wa Timu za Taifa mara wawapo ndani na nje ya uwanja. Hii itasaidia kujenga nidhamu ya timu. Kanuni
hizi zitaendana sambamba na kanuni za maadili za TFF.
(c) Walimu
Ni vyema siku za usoni timu zetu zote za Taifa zikafundishwa na makocha
wazawa.
Utaratibu utafanyika kuhakikisha makocha wasaidizi ambao ni wazawa wanaendelezwa
kufikia kiwango hicho, hii itakuwa ni pamoja na kuwapatia fursa za mafunzo
ndani na nje ya nchi.
(d) Zanzibar
TFF kwa kushirikiana na Chama cha
Mpira Zanzibar ZFA tutahakikisha kunakuwa na mahusiano ya karibu ya walimu wa
timu za Taifa Zanzibar na Bara ili kuhakikisha timu bora ya Taifa inaundwa na
vijana wa pande mbili za Muungano. Aidha jitahada za Zanzibar kuwa mwanachama
kamili wa CAF na FIFA zitaendelea kuungwa mkono.
2.
Utawala
Inabidi
tuendeleze utamaduni wa kuendesha shughuli za TFF kitaasisi (to have a corporate culture).Nguzo muhimu za uendeshaji
shirikisho kitaaluma ni pamoja na kujenga nidhamu ya wafanyakazi,heshima kwa
uongozi,utunzaji wa kumbukumbu,ukarimu kwa wageni,umakini katika manunuzi na
utunzaji wa fedha pamoja na kufanya kazi kwa malengo na kuhakikisha malengo
hayo yamefikiwa.
Maeneo yafuatayo yataboreshwa ili kuongeza
ufanisi:
2.1 Ofisi za Mikoa na Vyama
Shiriki
Kwa
kuzingatia vyama vya Mikoa kuwa ndio muendelezo mkuu wa shughuli za TFF Mikoani, ni muhimu ofisi za mikoa zikawa
kielelezo cha ufanisi wa utendaji wa TFF.
Ofisi za Mikoa zitaboreshwa hasa kwa kupewa vitendea kazi hususani vifaa
vya mawasiliano.
Vyama
shiriki hadi sasa havina ofisi zenye hadhi ya vyama hivi, tutahakikisha
tunaondoa aibu hii. Aidha kutokana na mapato ya TFF sehemu ya mapato haya
itatengwa kwa ajili ya ruzuku ya kupeleka kwenye vyama vya Mikoa na vyama
shiriki ili isaidie kupunguza makali ya kuendesha vyama vyetu.
2.2
Ofisi ya Rais
Kutakuwa na ofisi ya Rais wa TFF. Ofisi ya Rais wa TFF (office of the
President) lazima iimarishwe na iwe sehemu itakayoweza kukabiliana na
changamoto za maendeleo ya mpira wa miguu. Rais wa TFF ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za mpira wa
nchi hii,lazima awe na mahali stahili pa kufanyia kazi kulingana na hadhi
yake.Hii itakuwa ni pamoja na kuwa na wasaidizi wenye uweledi wa kutosha katika
shughuli za kila siku za kuongoza shirikisho.
Ofisi za TFF makao makuu uwanja wa Karume zitakarabatiwa na kuongeza
nafasi ya kufanyia kazi.
2.3 Maslahi
Maslahi
ya wafanyakazi wa TFF yataboreshwa ili kuwaongezea motisha. Hii itakuwa ni pamoja na kuwapa fursa ya
kuhudhuria mafunzo mbalimbali.
2.4 Vilabu vya Mpira
Vilabu
vitasaidiwa kupewa mwongozo wa kujiendesha kwa ufanisi zaidi. Aidha utaratibu wa mgawanyo wa mapato ya
milangoni utatazamwa upya kwa lengo la kuhakikisha vilabu vinapata mgao mkubwa
kuliko iliyo sasa. Hii ni kwa kuzingatia
gharama kubwa wanazoingia vilabu katika kuandaa timu ikiwemo malazi, usafiri,
vifaa, posho, dawa, mishahara n.k.
2.5
Wachezaji wastaafu
Hii
ni hazina ya Taifa,kustaafu kwao kucheza mpira sio mwisho wao wa kuchangia
maendeleo ya mpira wa nchi yetu.Jitihada zitafanyika kuanzisha mfuko maalum
(Trust Fund) ambao utachangiwa na wachezaji wenyewe wanapokuwa bado dimbani
pamoja na TFF, hii ni kwa ajili ya kuwasaidia hapo baadae wanapokuwa na
matatizo hasa ya ugonjwa. Aidha chama cha wachezaji wastaafu (SPUTANZA)
kitapewa ofisi na kitaimarishwa ili kiwe kiungo muhimu kati ya wachezaji na
TFF.Wachezaji watahimizwa watumie chama hiki kutatua matatizo yao na chama
kitapewa fursa kikanuni ya kuwa mtetezi mkuu na msimamizi wa maslahi ya
wachezaji.
2.6 Mikataba
Utaratibu
wa TFF kuingia mikataba na wadhamini mbalimbali utarekebishwa ili kuongeza
uwazi. Ipo mikataba ambayo imesainiwa na
TFF ambayo imesababisha vyama vya mikoa na wilaya, pamoja na uhaba wao wa pesa,
wahangaike kutafuta fedha za zaida kuandaa timu zao kwa ajili ya mashindano yanayobeba
jina la mdhamini kwa kuwa fedha anayotoa mdhamini haikidhi uendeshaji wa
mashindano yenyewe.
Aidha
vipengele tata vinavyokandamiza maslahi ya vilabu katika baadhi ya mikataba
inayosainiwa kati ya TFF na wadhamini vitarekebishwa kama sio kuondolewa kabisa
kwa maslahi ya ustawi wa mpira wetu. Haki za vilabu katika matangazo ya
biashara yahusuyo mpira zitalindwa kwa nguvu zote.
2.7 Utaratibu wa Mashindano
Yapo
mashindano ya vijana kama Umiseta na Umitashumta yanayoandaliwa na
Serikali. Kuna wakati mashindano kama haya
yanafanyika sambamba na mashindano yanayoandaliwa na TFF kama vile Copa Coca
Cola. Yote haya ni mashindano ya vijana,
na washiriki wanakuwa ni vijana toka shule hizo hizo. Kwa nini tugombee fito wakati tunajenga
nyumba moja? Ni vyema kalenda ya
mashindano ya vijana kitaifa ikaandaliwa kwa pamoja kati ya Serikali na TFF.
2.8 Usajili wa Vyama vya
Mpira vya Wanawake
Usajili
huu haujakamilika nchini nzima hususani ngazi ya wilaya. Juhudi zitafanyika kukamilisha zoezi hili ili
mpira wa wanawake uenee kote Tanzania.
2.9 Kitengo cha habari
Kitengo
hiki kitaboreshwa kwa kuongezewa nyenzo za kufanyia kazi na kukipatia fursa
zaidi za mafunzo. Aidha majukumu yake yataongezwa ili pia kishughulikie
mahusiano ya kimataifa.Hivyo kama nikichaguliwa nitapendekeza mkuu wake aitwe
‘Afisa habari na mahusiano ya kimataifa’.
1.
Masoko na
Uwekezaji
Mpira
unaendeshwa kwa fedha nyingi. TFF ili
iweze kujiendesha kwa ufanisi ni lazima iwe na vyanzo vya uhakikika vya
mapato. Ili kufanikisha azma hii kitengo
cha masoko na uwekezaji kitahakikisha kwamba:
UCHAGUZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) 2013
ILANI YANGU YA UCHAGUZI
Utangulizi
Ndugu zangu,
Nianze kwa
kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema aliyetulinda na kutuwezesha kufika
hapa tulipo.
Tarehe 19
Novemba 2009 Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati anazindua ziara ya Kombe la FIFA
la dunia uwanja wa Taifa, Dar Es Salaam pamoja na mambo mengine alisema,
namnukuu:
‘‘Kwa
Watanzania wenzangu tuichukulie ziara ya Kombe la Dunia nchini mwetu kama ni
changamoto kubwa kwetu inayotutaka tufanye vizuri zaidi katika soka ili
tulingane na heshima hii tuliyopewa.
Hasa ni changamoto kwa viongozi wa soka wa ngazi zote pamoja na
wachezaji na wapenzi wa mpira wa miguu nchini.
Kuja kwa kombe hili ni deni kwetu na kulilipa kwetu sisi ni kuzinduka,
tuendeleze kiwango chetu cha soka nchini ili na sisi siku moja TUSHIRIKI FAINALI ZA KOMBE HILI (msisitizo ni wa
kwangu). Hili jambo linawezekana. Wapo wenzetu Afrika wameweza, kwa nini sisi
tusiweze? Wao ni watu kama sisi, maadam
wameweza na sisi tutaweza.
Lakini
ili tuweze hatuna budi kuiga mfano hususani waliyofanya wenzetu na
wanayoendelea kufanya kuendeleza mpira wa miguu. Twende tukajifunze kutoka kwao. Lakini hata kabla ya kwenda huko, yapo mambo
hatuna budi kuyafanya. Naomba nitaje
baadhi yake:
1.
Tuimarishe Uongozi, utendaji na uendeshaji wa vilabu vya
mpira. Mchezaji hufundishwa kucheza
mpira katika Klabu yake. Hapo ndipo
hufundishwa maarifa ya kucheza mpira na vipaji kuendelezwa. Hebu tujiulize hali ya vilabu vyetu vya soka
ikoje. Je vinaongozwa vizuri? Vinaendeshwa vizuri? Jibu tunalijua sote kuwa ni hapana. Lazima suala hili tulitafakari kwa makini na
kulipatia jawabu. Tukishindwa kupata
jawabu muafaka na mambo yakaachwa kuendelea yalivyo, mpaka mwisho wa dunia
hatutakuwa tunasogea popote.
2.
Tupate walimu wenye uzoefu kufundisha timu zetu. Hii ndiyo njia ya uhakika ya kukuza na
kuendeleza vipaji na hivyo kupata wachezaji bora.
3.
Tuwekeze katika kuibua na kuendeleza vipaji vya
wachezaji toka umri mdogo. Vilabu viwe
na timu za watoto na vijana. TFF isaidie
kuanzishwa kwa shule za mchezo wa mpira wa miguu kwa watoto na vijana. Mashuleni wapatikane walimu wa michezo walio
wazuri kufundisha.
4.
TFF ionekane zaidi ya ilivyo sasa katika mipango ya
kuendeleza soka mashuleni, vijijini, mitaani na vilabuni. TFF ikiwa na mipango na kuisimamia na
kuwabana wadau kuitekeleza itasaidia.
Vinginevyo TFF itabakia kusimamia Ligi Kuu, kutoa adhabu kwa wachezaji
na kusimamia timu ya Taifa. Hiyo
haitoshi.’’
Mwisho wa kunukuu.
Ndugu zangu wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, wadau na wapenzi wa mpira wa
Miguu Tanzania tujiulize kuanzia kipindi hicho cha 2009 hadi leo hii katika
haya maagizo ya Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete tumetekeleza yapi zaidi ya kuwa wasindikizaji katika medani ya
kimataifa? Kipindi chote cha miaka
minane iliyopita Serikali imetoa sapoti kubwa katika sekta ya mpira wa miguu
kwa kulipia walimu wa timu za Taifa na kuhimiza makampuni kama NMB,Serengeti
Breweries,Airtel,Coca Cola na sasa Tanzania Breweries kudhamini timu zetu za taifa na mashindano
mbali mbali,matunda yake yako wapi? Ndo kwanza tunazidi kuporomoka kwenye
viwango vya FIFA. Iweje miaka ya nyuma timu zetu za Taifa zilifanya vizuri
wakati zinaweka kambi Salvation Army, leo zinakaa hotel za nyota tatu mafanikio
mbona hatuyaoni? Kama TFF imeondolewa
gharama za kulipa makocha,kuweka timu kambini,kununua vifaa vya timu,dawa,posho,malazi
pamoja na usafiri wa timu iweje leo TFF ishindwe kutumia vyanzo vyake vya
mapato zikiwemo fedha toka FIFA na CAF kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza
programmu ya vijana ya kitaifa? Kwa mujibu wa mtandao wa FIFA kati ya mwaka
2008 na 2012 TFF imepokea toka FIFA msaada wa jumla ya dola za kimarekani
milioni moja na lake nane na nusu (yapata shilingi bilioni tatu za kitanzania),
hizi fedha zimefanyia nini? Kwa nini
timu za vijana hazina udhamini? Ipi timu yetu ya taifa iwe ya wanaume wakubwa (senior team) ,
wanawake au za vijana inayoweza leo hii kujivunia mafanikio? Iko wapi ligi ya wanawake? Katika hili
tusilaumu Chama cha mpira cha wanawake, wakiwezeshwa wanaweza.Tutapataje timu
mahiri ya Twiga stars bila ligi ya wanawake? Katika ngazi ya klabu, hasa
zinazoendeshwa kwa mfumo wa kijamii kama
Toto Africa, Coastal Union, Yanga, Simba,Mbeya City n.k. hadi leo hii pamoja na
rasilimali za vilabu hivi ni klabu ipi imeweza kusimamia na kujiendesha yenyewe
tokana na vyanzo vyake yenyewe? Tuendelee kujiuliza:
Ø
Ni walimu wangapi wa mpira tumewaendeleza
kufikia kiwango cha kukabidhiwa majukumu ya kufundisha Taifa Stars. Fursa za mafunzo tunazopewa na FIFA na CAF
tunazitumiaje? Je tumeweza kuwa na angalau kocha mmoja anayefundisha mpira nje ya
nchi kama ilivyo kwa akina Sam Timbe ( wa Uganda), James Sianga ( wa Kenya) Jack Chamangwana ( wa Malawi) na wengine ambao waliweza kufundisha mpira Tanzania kwa
ufanisi?
Ø
Ni refa gani tumemuendeleza akafikia kiwango cha
kuchezesha mashindano ya fainali za dunia au AFCON au Klabu bingwa ya
Africa? Refa wa mwisho kuchezesha
fainali za Mataifa Africa (AFCON) ni Omar Abdulkadir huko Burkina Faso mwaka
1998.
Ø
Ni program ipi ya vijana ya kuibua vipaji na
kuviendeleza tuliyo nayo? Wale vijana wa
Copa Cocacola 2007 waliopelekwa kwa mbwembwe Brazil waliishia wapi? Tuna rekodi
zao?Tunajua wako wapi na wanafanya nini? Na hawa walioshinda majuzi Afrika
Airtel Rising Stars tumewatangenezea program gani ya maendeleo?
Ø
Tunaelewa matatizo ya vilabu vya mpira hususani
uhaba wa vifaa na pesa za uendeshaji, je vilabu vyetu TFF inavisaidiaje katika
kuendeleza programu zao za vijana?Au kazi yetu ni kudai kila klabu iwe na timu
ya under 20 bila kujali gharama za uendeshaji wa timu hizi?
Ø
TFF hadi sasa imebuni, kusimamia na kutekeleza
program endelevu ipi ya kuendeleza soka mashuleni, vijijini, mitaani au
vilabuni? Au mpaka tusubiri Airtel
rising Star na Copa Cocacola? Siku wakubwa
hawa wakisusa itakuwaje?
Ø
Ziko wapi juhudi za kuhimiza upatikani wa vifaa
vya kufundishia mpira watoto (kama mipira size 3/4) pamoja na kuimarisha miradi ya kuendeleza vijana
?
Ø
Hivi timu zetu za Taifa zinatumia mfumo upi wa
uchezaji? Au kila kocha wa taifa
tunayemleta anakuja na mfumo wake? Wenzetu wameweza kubuni mifumo ya uchezaji
ya timu zao za Taifa na wameushirikisha katika mfumo wa ufundishaji wa watoto. Lini Mwalimu wetu wa Taifa alikaa na walimu wa
vilabu (angalau vya Premier League) ili kujadili ufundishwaji wa mpira nchini,
hii ikiwa ni pamoja na kujadili masuala yahusuyo mbinu, lishe, huduma za afya
na ukakamavu wa mwili? Hivi mchezaji
akitoka katika klabu yake ambako amezoea kula dona na maharage ukampeleka kambi
ya Timu ya Taifa akapewa prawns ,kuku na samaki kwa siku nne za kambi itamsaidia kumbadili
siha? Ng’ombe hanenepeshwi siku ya mnada.Uratibu
wa programu za vilabu ni muhimu.
Ø
Raha ya mpira ni kelele na hoi hoi za
mashabiki. Wataalam wa mpira wanasema
umoja wa mashabiki wa mpira ni sawa na mchezaji wa 12 uwanjani. Zipo timu ambazo kihistoria zilikuwa ni za kijamii
na zilihamasisha sana ligi ya Taifa, na kuiongeza hamasa na ushindani,Mbeya
City ni mashahidi. Leo hii ziko wapi timu kama Ushirika ya Moshi, Bandari ya
Mtwara, Kariakoo Lindi, Balimi Bukoba, Reli Kiboko ya vigogo, Kahama United,
Mirambo ya Tabora, Tukuyu Stars, Nyota Korogwe, African Sports ya Tanga,Ujenzi
Rukwa,Mji Mpwapwa n.k. TFF imefanya juhudi gani kufufua ushidani huu
kwa kushirikiana na vyama vya Mikoa na Wilaya?
Ø
Wapo wachezaji wastaafu waliojitolea kwa moyo
mmoja kuiletea heshima nchi yetu. Leo
hii tunasikia kina Alfonce Modest na Jellah Mtagwa wanalalamika hawana msaada,
na hao ndio wale waliojitolea hadharani kutoa kilio chao. TFF hadi leo hii imewahi kuandaa mpango gani endelevu
wa kuwasaidia wachezaji wastaafu? Shirikisho la mpira barani Afrika CAF
wameanzisha ISSA HAYATOU TRUST FUND kusaidia wachezaji wastaafu waishio katika
mazingira magumu,sisi tumechukua hatua gani katika hili?
Ø
Iweje mpake leo hakuna mashindano yoyote ya wanawake
ya kitaifa yawe ya ligi au ya mtoano,angalau kwa ngazi ya kanda ? TFF itawezaje kuibua vipaji vipya vya timu ya
taifa ya wanawake TWIGA Stars bila mashindano ya aina hii?
Ø
Vilabu vya mpira, hususani vya Ligi Kuu, vimegeuka
kuwa kisima cha watu kuchota fedha.
Haiyumkiniki vilabu ambavyo vinaweka timu kambini, kuihudumai kuanzia
malazi, posho, vifaa, madawa na usafiri mwisho wa mechi jumla ya pesa
wanayopewa inakuwa chini ya nusu ya
mapato yote ya mechi. Hayo maendeleo ya mpira ambayo yametakiwa
yaanzie ngazi ya vilabu yatapatikanaje? Vilabu vimegeuka vitega uchumi vya watu
wengine wakati vyenyewe vinataabika na kujiendesha kwa mateso makubwa.
Ya
kusema ni mengi, kwa leo tuishie hapa.
Nini matokeo ya hali hii? Takwimu hazidanganyi. Matokeo ya hali hii ni
timu za Taifa kushuka viwango katika orodha ya FIFA siku hadi siku. Viwango vya
timu za taifa vinapimwa kwa kuangalia uwiano wa matokeo ya timu ya wakubwa
(senior) pamoja na yale ya timu nyingine za vijana za nchi husika. Miaka ya
mwanzo ya tisini tulishawahi kupanda hadi nafasi ya 65, leo hii kila kukicha
tuko kwenye 120.Kuporomoka huku kutaendelea hadi lini?
Ndugu zangu, tujiulize wapi tumetoka, tuko wapi na tunataka kuelekea
wapi? Jibu ni rahisi, kama alivyoagiza
Mh Rais Kikwete,tujipange upya, tubuni mkakati wa uendelezaji wa mpira, tuandae
program endelevu yenye malengo
yanayopimika na kwa pamoja tukishirikiana na Serikali, FIFA CAF na CECAFA,Halmashauri, Taasisi zisizo za
kiserikali, Sekta binafsi, Vyombo vya habari na wadau wengine wote wa mpira wa
miguu tutaweza kufanya vizuri na kuifanya Tanzania isifike duniani kote. Katika kutimiza azma hii sharti tuanzie kwa
kuleta mabadiliko ya uongozi wa juu wa TFF, tupate kiongozi ambaye sio
sehemu ya mapungufu ya TFF,hakuna njia ya mkato.Mimi Jamal Emil Malinzi,nimejipima na ninaamini nina uwezo wa kutosha
wa kubuni, kuratibu na kusimamia mabadiliko haya nikiwa Rais wa TFF.
Ndugu zangu, siku zote si vyema kukosoa bila kueleza njia mbadala ya
kufuata ili kutatua tatizo. Hapa
tunazungumzia mpira wa miguu na namna ya kuunasua toka kwenye janga la kushuka kiwango na timu zetu za Taifa
kuendelea kugeuzwa kichwa cha mwenda wazimu ambacho hadi majuzi vibonde Gambia
wamejifunzia kunyoa.
Ili tuweze kuukwamua mpira wetu ni
vyema tukakumbushana kuwa ili mpira uendelee unahitaji vitu vinne:
- Vipaji;
- Walimu;
- Vifaa;
- Viwanja
1.
Vipaji
Tanzania
ni nchi yenye watu zaidi ya milioni 44.
Nchi ya Cape Verde yenye watu 500,000 tu imeweza pamoja na uchache wake
kuvumbua vijana 11 ambao wameweza kuifikisha nchi yao fainali za Africa 2013
Afrika Kusini na majuzi nusura waende kombe la dunia kama sio tatizo la
utunzaji kumbukumbu. Sayansi ya uibuaji
vipaji (scouting) ni muhimu na si kila mtu anaijua. Watafutwe wanaoijua, watufanyie kazi ya
kutuibulia vipaji vipya, na katika hili ni sharti mpira wa ushindani uchezwe
nchini kote ili vipaji vionekane.
2.
Walimu
Mpira
ni sayansi,mpira ni taaluma. Kipaji bila mwalimu wa kukiendeleza ni bure. Vijana mpira wanaanza kuucheza wakiwa wadogo
hususani wakiwa shule za msingi. Huko
ndiko Taifa linahitaji kusambaza walimu wenye taaluma ya kufundisha mpira ngazi
ya awali. Wakishakuzwa kimpira ni lazima wawepo walimu wa kutosha kuwaendeleza
ngazi ya wakubwa na Taifa. Leo hii Uingereza ina walimu 1100 wenye leseni daraja
A,Ujerumani wapo 5500 na Hispania
12,000,Tanzania tunaye mmoja tu,kwa mtaji huu tutafika kweli?Kwa mujibu wa
ripoti ya TFF nchi nzima ya Tanzania ina
walimu wa mpira wa madaraja yote elfu mbili tu na mia tano kati yao wako Dar es
salaam. Hawa walimu 2000 ndio wanategemewa wawafundishe mpira vijana wa
Kitanzania zaidi ya milioni kumi walio katika umri wa kufundishwa mpira!
3.
Vifaa
Wachezaji,
walimu wa mpira, madaktari na waamuzi wote
wanahitaji vifaa vya msingi ili mpira uchezwe.
Nchini mwetu vijana walio wengi wanacheza pekupeku, jezi ni upande mmoja
kucheza kifua wazi, mpira ni wa kuviringisha matambara, refa anavaa suruali, filimbi
ni mluzi, magoli hayana nyavu, n.k. Hii
ndiyo hali halisi ya uchezwaji wa mpira maeneo mengi Tanzania hasa vijijini
ambako ndiko kunapaswa kuwa chimbuko kubwa la vipaji.
Gharama
za vifaa vya michezo ziko juu mno, mfano mpira mzuri unaofaa kuchezewa kwenye
ardhi ngumu (rough surface) bei yake ni shilingi laki tatu, shule ipi ya msingi
itaweza kuununua huu mpira? Kuna baadhi ya vyombo vya habari majuzi viliripoti
kuwa kuna mchezaji alifunga hat trick ngazi ya Ligi Taifa akanyimwa mpira kisa
ni wa thamani kubwa. Mamlaka husika, hasa za kodi zinapaswa kuliangalia hili,
ili upatikane unafuu katika bei za vifaa vya michezo maana karibia vyote
vinaagizwa toka nje. Lakini pia vifaa
vya michezo vya misaada vinavyopatikana kutokana na miradi mbalimbali ya TFF ni
juu ya TFF kuhakikisha vinafikishwa vijijini pia kupitia vyama vya mikoa na
wilaya.
- Viwanja
Wilayani Ngara mkoani Kagera kuna uwanja wa mpira unaitwa ‘’Uwanja wa
Changarawe’’ na ni kweli uwanja huo umejaa changarawe. Beki akikaba kwa mtindo wa kuteleza ardhini ‘sliding
tackle’ basi nyama ya paja anaiacha pale chini.
Hii ndiyo hali halisi ya viwanja vyetu vingi nchini, kama vipo ni vibovu
sana maana maeneo mengi viwanja vya mpira hakuna vimechukuliwa na wajanja
wachache na kugeuzwa makazi na majengo
ya biashara. Tunahitaji viwanja vyenye
ubora ili vijana wetu wafundishwe mpira wa kisasa kwa ufanisi, mpira wa kupiga
pasi ya chini. TFF kwa kushirikiana na
vyama vya Mikoa na Wilaya sharti wawe mstari wa mbele katika kulipigania hili.
AHADI YANGU
Endapo nitachaguliwa kuwa Rais wa TFF, kwa kushirikiana na viongozi wote
wa TFF kuanzia ngazi ya vilabu, Wilaya, Mikoa na Kamati ya Utendaji Taifa na
kwa kuhusisha kwa karibu Vyama vya kimataifa vya FIFA na CAF, Serikali, Halmashauri,Taasisi
zisizo za kiserikali, Vyombo vya habari, Sekta binafsi, Mashirika ya umma na
wadau wa mpira wa miguu Tanzania ninaahidi kuenzi mafanikio ya awamu inayomaliza muda
wake , kustawisha utulivu katika uendeshaji wa mpira, na kufanya jitihada za kubuni, kuboresha na kustawisha maendeleo
ya mpira wa miguu Tanzania. Jitihada kubwa zitawekwa kwenye maeneo makuu
yafuatayo:
1.
Ufundi
(Technical)
1.1 Muundo wa Idara ya
Ufundi
Katiba
ya TFF imeainisha wazi kuwa TFF ndiye msimamizi mkuu wa mpira wa miguu
Tanzania, hivyo jukumu la kuleta maendeleo ya mchezo huu kwa kiasi kikubwa
linaiangukia TFF.Ni kwa msingi huu basi asilimia kubwa ya rasilimali za TFF
lazima iwekezwe katika kuleta maendeleo ya mpira. Kwa mfumo wetu wa uendeshaji, kichocheo kikuu
cha maendeleo ya mpira ni idara ya ufundi ya TFF. Hivyo idara hii ya ufundi inapaswa kuwa ndiyo
idara mama ya TFF ambayo inapaswa kuongoza kwa matumizi ya fedha, idadi ya
waajiriwa na matumizi ya rasilimali nyingine za TFF . Kwa sasa pale TFF hali sivyo ilivyo. Iwapo nitachaguliwa nitapendekeza jukumu la
kwanza la Kamati ya utendaji liwe ni kurekebisha na kuboresha mfumo wa
uendeshaji wa idara ya ufundi.
Nitapendekeza idara ya ufundi iendelee kuongozwa na Mkurugenzi wa Ufundi
na chini yake awe na wakurugenzi wasaidizi wa vitengo watatu Mkurugenzi Msaidizi
(ufundi), Mkurugenzi Msaidizi (Elimu na Mafunzo) ambaye kwa sasa anaitwa Education officer, na
Mkurugenzi Msaidizi (Maendeleo ya mpira).
Kitengo
cha Ufundi kitahusika na kubuni na kusimamia shughuli zote zinazohusu maendeleo
ya Timu za Taifa kuanzia za wakubwa hadi za vijana. Hii itakuwa ni pamoja na
kuandaa mitaala ya taifa (national football curriculum) ya ufundishaji wa mpira
Tanzania kuanzia umri wa miaka mitano
hadi watu wazima. Walimu wa Timu za Taifa wataripoti kwake.
Kitengo
cha Elimu na Mafunzo kitahusika na kubuni na kuratibu kozi zote na mafunzo yote
yanayohusiana na mpira kama vile kozi za Marefa, Makocha, Madaktari, Makamisaa,
Watawala, Waandishi wa Habari za Michezo, n.k.
Kitengo
cha Maendeleo ya mpira kitahusika na kubuni,kuratibu na kusimamia mpango wa maendeleo
ya vijana (grassroot) na kutafuta
vipaji (scouting). Kitengo hiki kitafanya kazi kwa kushirikiana kwa ukaribu na
idara za Serikali hasa idara za Elimu,Vijana na TAMISEMI, Halmashauri,Mashirika ya
umma,Sekta binafsi pamoja na Taasisi nyingine za kijamii.
Wakuu
wa vitengo hivi wataajiriwa kwa kufuata vigezo makini na bila upendeleo wala
kujuana.
1.2
Ujenzi wa Kituo cha Mpira (Football Centre of
excellency)
Hiki
ni Kituo Maalum cha mafunzo ya mpira wa miguu.
Katika kituo hiki kunakuwa na kila aina ya miundo mbinu, viwanja vya
kufundishia mpira, vituo vya tiba,madarasa ,maabara za utafiti,hosteli n.k Kituo hiki pia kinakuwa ndio sehemu kuu ya
kuweka kambi za timu za Taifa na kutoa mafunzo ya ufundi yakiwemo ya ukocha,
urefa, utawala na tiba. Wenzetu wa
Senegal na Ethiopia kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira Africa CAF wameweza
kujenga vituo hivi na matokeo yake tunayaona.Cameroon pia wana kituo hiki.
Pamoja
na gharama zake kuwa kubwa, cha muhimu hapa ni kuweka nia, kutafuta ardhi kwa
kushirikiana na Serikali na kuanza ujenzi taratibu.Kwa kuwa klabu ya Sunderland
ya Uingereza na kampuni ya kufua umeme ya Symbion wameonyesha nia ya
kushirikiana naSerikali kujenga kituo cha michezo itakuwa vyema iwapo TFF
itashirikiana na taasisi hizi muhimu ili kufikia azma ya kujenga kituo hiki cha
kisasa. Iwapo nitachaguliwa nitasimamia uanzishwaji wa mradi huu muhimu ikiwa
ni sehemu ya mkakati wa kulikomboa soka letu.
Aidha
uwanja wa Karume yalipo makao makuu ya TFF utazungushiwa jukwaa ili mechi
ambazo sio kubwa zifanyike pale, Hii itaiongezea TFF mapato na vilabu pia.
1.3 Timu
Kupanda Daraja
Ili
kuongeza ushindani na kupanua mpira uchezwe kona zote za nchini ( to spread the
game) ,mtindo wa kucheza kikanda ili kupata timu za kupanda daraja kuu utakuwa
ni wa kudumu na utaimarishwa kwa
kutafutiwa udhamini na kuboreshwa viwanja kwa kushirikiana na wamiliki wa
viwanja hivyo. Usimamizi wa mashindano ngazi hii utaimarishwa na kusimamiwa kwa
karibu zaidi ili timu itakayopanda daraja iwe imepanda kwa haki na hivyo kuleta
ushindani Ligi Kuu.
Hata
hivyo waraka uliotolewa na TFF ukiagiza mikoa ichezeshe ligi ili kupata bingwa
wa mkoa utafutwa kwa sababu hautekelezeki kutokana na hali ya uchumi na
uhalisia wa jiografia ya mikoa ya Tanzania.
Mathalani Mkoa wa Mtwara ukichezesha ligi ya mkoa (kwa maana ya nyumbani
na ugenini) ina maana bingwa wa Wilaya ya Masasi atasafiri vipi
akacheze Newala au Mkoani Lindi bingwa wa Liwale atasafiri vipi akacheze na bingwa
wa Kilwa , Pwani bingwa wa Mafia atasafiri kwa gharama za nani akacheze
Bagamoyo na wa Kibaha akacheze Utete? Pamoja na nia njema ya TFF uhalisia
hauruhusu. Kama Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Kagera nalijua hili, hakuna
haja ya TFF kuwa inatoa maelekezo ambayo hayatekelezeki, hasa ukizingatia kuwa
TFF hakuna msaada wanaopeleka kusaidia mikoa na wilaya ziandae mashindano yao.Vyama
vya mikoa na wilaya viachwe viendelee kutumia ubunifu wao kupata mabingwa wao
kulingana na hali halisi ya mazingira yao.
1.4 Kuanzisha mashindano
mapya na kufufua ya zamani
Wataalam
wa kandanda wanasema kuwa ili mchezaji awe katika kiwango bora inabidi acheze
kwa mwaka kimashindano wastani wa mechi 40.
Ligi yetu kuu,Vodacom premier league,inatoa fursa kwa mchezaji kucheza
michezo 26 kwa mwaka iwapo anapangwa kila mechi.Hii haitoshi. Namna pekee ya
kurekebisha hali hii ni kuongeza idadi ya mashindano kwa mwaka.Hili litafanyika
kwa kufufua kombe la Taifa (Taifa cup)
na kuanzisha kombe la shirikisho (kama FA cup ya Uingereza). Kombe la shirikisho
litashirikisha timu zote nchini kuanzia ngazi ya kata,tarafa,wilaya,mkoa hadi
Taifa na bingwa wake atawakilisha nchi
katika kombe la shirikisho la Afrika CAF confederation cup (kama ilivyo Kenya
kwa sasa).
1.5. Mpira wa Wanawake
Hadi
sasa hatuna mfumo imara na unaoeleweka wa kuendeleza soka la kinamama. Mpira wa wanawake umeanzia Wilaya ya
Kinondoni, ukakulia Wilaya ya Kinondoni na umegotea Wilaya ya Kinondoni ambako
kuna timu zenye majina kama Mburahati Queens na Sayari Queens. Mpira wa wanawake sharti usambae nchi nzima,
na ili kufanikisha azma hii lazima yaanzishwe mashindano ya kitaifa ya wanawake
ikiwemo Ligi ya taifa ya wanawake. Hii
itaendana na juhudi za kuongeza makocha, waamuzi na makamisaa wanawake na
kutafuta udhamini kwa timu ya Taifa ya wanawake TWIGA STARS.
1.6 Maandalizi ya Vijana
(Grassroot Programme)
Mpango
endelevu wa maendeleo ya soka la vijana sharti uandaliwe, uratibiwe na
kusimamiwa kwa makini. Program madhubuti
ya maendeleo ya mpira wa vijana lazima ibuniwe ,iratibiwe na kusimamiwa kwa
usatadi mkubwa.Mradi huu lazima ulenge ,kwa hatua,kufikia hatua ya kuingiza
timu zetu fainali za kombe la Afrika la vijana chini ya umri wa miaka 17 na
20,fainali za olimpiki, fainali za Afrika wachezaji wa ndani CHAN,fainali za
Afrika AFCON na mwisho fainali za kombe la dunia.Hii itakuwa ni pamoja na
kujiwekea utaratibu wa mzuri wa kuhakikisha vijana wetu wanapata fursa ya
kucheza mpira nje ya nchi ili kujiongezea umahiri.Na hii ni kwa wanawake na
wanaume.
Mpango
huu ni lazima ushirikishe Serikali Kuu (hasa Wizara zenye dhamana ya Michezo, Elimu
na Halmashauri), Taasisi zisizo za kiserikali,mashirika ya umma,sekta binafsi na
TFF,CAF na FIFA. Ushirikishwaji wa Serikali
na Halmashauri katika program hii ni muhimu sana kwa kuwa ndio wasimamizi na
wamiliki wa shule nyingi za msingi ambako ndiko vijana wetu wanakoanzia kucheza
mpira. Mpango kazi huu lazima uonyeshe:
1.
Nini tunataka kufanikisha.
2.
Utaratibu utakaotumika.
3.
Nguvu kazi inayotakiwa na sifa zake.
4.
Mwongozo wa kufuatilia kupima ufanisi wa programu.
5.
Kupambanua gharama za mpango na taratibu za uchangiaji
wake.
Hatua muhimu katika kufanikisha program hii zitakuwa ni:
-Kufundisha walimu wa walimu (instructors), hawa ndio watakuwa chachu ya
kupata walimu wa mpira mashuleni na mitaani.
-Walimu wa walimu (instructors) kufundisha walimu wa kutosha wa michezo
mashuleni na mitaani
-Kwa kushirikiana na wamiliki wa shule kuhakikisha viwanja vya kuchezea
vinakidhi viwango
-Kutafuta na kusambaza vifaa vya michezo mashuleni hasa mipira ya saizi
muafaka kwa mujibu wa viwango vya kimataifa.
-Kupata shule angalau moja kila mkoa itakayopokea watoto wenye vipaji
maalum vya kucheza mpira, pale ambapo wazazi hawataweza kuwalipia karo vijana
hawa basi TFF ihakikishe karo zao zinapatikana,huo ndio uwekezaji katika mpira.
-Kuandaa mashindano mbali mbali yatakayoshirikisha shule hizi ili kupata
timu za taifa za vijana wa umri mdogo wa kike na wa kiume.
-Kuhakikisha timu hizi za umri mdogo zinapata fursa ya kushiriki
mashindano mbali mbali ya kimataifa
- Kupata vikosi vizuri vya timu za taifa za vijana wa umri mdogo ambao
watakua pamoja, hao ndio watajenga msingi imara wa timu za Taifa za wakubwa kwa
miaka ya baadae.
Itakuwa ni muhimu sana program hii iendane vizuri na ratiba nyingine za
mashindano ya kitaifa kama Umitashumta, Umisseta, Airtel rising star, Copa Coca
Cola n.k.
-
Kuanzisha mashindano ya kitaifa ya kombaini za shule za
sekondari na ya kombaini za vyuo vikuu. Wachezaji mahiri wa timu ya taifa kama
Leodeger Chilla Tenga (Rais wa TFF) na Leopold Tasso Mkebezi (meneja wa Taifa
stars) waliibukia kwenye mashindano kama haya Mkebezi akiwa beki wa kombaini ya
sekondari za Bukoba,Ihungo,Kahororo na Nyakato.
Aidha
vituo vya michezo (sports academies) ambavyo tayari vipo vitatengenezewa utaratibu
wa usajili na kuwekewa utaribu wa kuviendesha.
Ili
kuondoa ulalamishi wa vituo vya mafunzo (Academies) kulalamikia malipo pindi
mchezaji akisajiliwa timu kubwa, vituo vyote vya vijana vitasajiliwa na vijana
wao wote wataingizwa kwenye kumbukumbu za TFF (data base) kwa majina, saini na
picha,hii itasaidia kuzuia sakata kama la Mbwana Samata na klabu yake ya utotoni
ya Mbagala maana kumbukumbu za TFF zitakuwa ndio jibu la maswali yote.
1.7 Tiba
1.
Tutaimarisha usalama uwanjani. Tutahimiza kila uwanja zinakochezwa mechi za
ligi kuwe na gari la wagonjwa na chumba cha dharura (emergency room).
Katika
kuimarisha usalama tutahakikisha vifaa muhimu vya dharura kama vifaa vya hewa
(oxygen) na vifaa vya kushtua moyo (defibulator) vinakuwepo. Kwa sasa hapa Tanzania uwanja pekee wenye
vifaa hivi ni Uwanja wa Azam Chamazi. Ni
jambo la kusikitisha kuona hata uwanja mpya wa Taifa hauna chumba cha tiba
dharura (emergency room) na kibaya zaidi makato ya uwanja hayaendi kuanzisha huduma hii
muhimu wakati viongozi mbalimbali wa kitaifa wanahudhuria mechi uwanjani.
2.
Mradi wa Goal Project wa FIFA unatoa pesa za tiba na
mradi huu uliweka lengo la kuwa na chumba cha kliniki pale uwanja wa Karume. Tutakifufua chumba hiki, tutakiwekea vifaa na
kuhakikisha huduma ya kliniki kwa wanamichezo iliyokuwa ikitolewa na madaktari kila
Jumapili inarudishwa. Posho itatafutwa
ili madaktari watoa huduma angalau wapate nauli na maji ya kunywa.
3.
Wakati wa kujadiliana mikataba na wadhamini mbalimbali
tutahakikisha kipengele cha huduma za afya kinaingizwa katika mikataba.
Udhamini utatafutwa kwa ajili ya vipimo vya wachezaji kabla ya league (pre-league
medical test) kama vile vipimo vya uvumilivu (Yo-Yo test) na vipimo vya moyo
(cardiac tests). Hii ni kwa ajili ya usalama wa wachezaji na waamuzi.
4.
Hadi leo chama cha Madaktari Tanzania, TASMA hakina
ofisi. Hii ni aibu kwa chama chenye
hadhi na umuhimu wa kipekee kama hiki.
Tutahakikisha TASMA inapata ofisi yake pamoja na chumba maalum cha
kliniki.
5.
Huduma ya afya lazima iwe sehemu maalum ya mfumo wa
idara ya ufundi. Ni muhimu timu ya madaktari
wa Timu ya Taifa (National Medical team) ijulikane ni kina nani na wapewe mikataba
ya kazi. Hii tutalipigania.
6.
Majeraha ya michezo huwa yanahitaji utaalam wake wa
tiba. Tutaiomba Serikali itupe
ushirikiano ili kipatikane kitengo maalum cha kutibu majeraha ya wanamichezo
(sports injuries wing) katika baadhi ya hospitali zetu wakati tunajiandaa kuwa
na kitengo cha tiba (Rehabilitation Centre) katika kituo cha michezo
kitakachojengwa.
7.
Ili kuimarisha uwezo wa madaktari wetu kutoa huduma za
afya kwa wanamichezo, tutahakikisha madaktari wengi kadiri iwezekanavyo wanapata
kozi za msingi,kati na juu (preliminary,intermediate and advanced). Nafasi hizi
zitatolewa bila upendeleo wala kujuana.
- Utoaji wa ushauri nasaha kwa wachezaji utaongezeka hasa
kuhusu masuala ya ukimwi na madhara ya madawa ya kuongeza nguvu na ya
kulevya.
1.8 Waamuzi
Imepita miaka zaidi ya 15 toka Tanzania itoe mwamuzi wa kimataifa wa
kuchezesha fainali kubwa (mara ya mwisho AFCON 1998), hii si sawa. Utaratibu
uliopo sasa wa kuwapata na kuwaendeleza waamuzi ama una mapungufu au haufai
kabisa hivyo budi utafutwe utaratibu ulio mzuri zaidi katika kupata waamuzi
bora, tafiti zitafanywa ili kubaini ni njia zipi za kisayansi za kuwapata
waamuzi bora (Top referees).Semina za mara kwa mara za CAF na FIFA ni nzuri
lakini hazitoshi, TFF lazima iwekeze kwa kutoa mafunzo zaidi ya waamuzi kwa
gharama zake.
Aidha mradi wa maendeleo ya mpira kwa vijana (grassroot) utahusisha pia
mafunzo ya uamuzi wa mpira kwa vijana kama kinavyofanya kituo cha Jenerali Twalipo.
Utaratibu wa kutoa adhabu kwa waamuzi wanaosemekana wameboronga uwanjani
nao unahitaji marekebisho ya haraka sana. Uamuzi wa mpira ni taaluma kama
zilivyo taaluma nyingine,mwamuzi akikosea ni vyema akakosolewa na mwamuzi
mwenzie ambaye ni mwandamizi,na kama ni kuadhibiwa aadhibiwe na jopo la waamuzi
wenzie waandamizi lakini wastaafu na sio mtu mwingine ambaye hajawahi kupuliza
filimbi.
1.9 Makocha
Kumekuweko
na utamaduni usiofaa katika soka la Tanzania miaka ya karibuni wa kuona kuwa
makocha wa kigeni ndio bora zaidi na wanastahili mikataba,mishahara minono na
marupurupu ilhali makocha wazawa wanageuzwa ‘deiwaka’, jambo hili ni baya
sana,ajira ziheshimiwe kwa msingi wa taaluma na sio kwa msingi wa nchi atokayo
mtu.
Makocha
wetu wazalendo wana uwezo mkubwa kama wakipewa nyenzo kama wanazopatiwa wageni,
kama malipo mazuri, mikataba ya muda mrefu, vitendea kazi na kuheshimiwa
program zao bila kuingiliwa na viongozi.Iwapo nitachaguliwa ninaahidi:
- Kuwaendeleza
makocha kimafunzo ndani na nje ya nchi kwa wale wenye uwezo na utashi wa
kufanya hivyo.
- Kushawishi
taasisi za elimu nchini kama vyuo vikuu kufundisha taaluma ya ukocha
- Kuhakikisha
walimu wa mpira wa timu zetu za Taifa wanakuwa na mikataba stahiki, hii ni
pamoja na benchi zima la ufundi.
- Kuwajengea
uwezo makocha wetu wazalendo ili nao wapate fursa ya kufundisha mpira nje ya
nchi.
- Kuanzisha
tuzo za kila mwaka za makocha wazalendo ambao wamefanya vizuri katika
ufundishaji wa soka la vijana la wanawake na wanaume.
- Kuhakikisha
utaratibu wa leseni za CAF unazingatia vigezo vya kitaaluma, uzoefu na ushiriki
wa kocha mhusika katika ufundishaji. Makocha ambao wanafundisha (active
coaches) watapewa kipaumbele katika kupata kozi za kupanda madaraja kuliko wale
wanaofungia vyeti makabatini.Leseni za CAF ni muhimu katika kumfanya mwalimu wa
mpira atambulike kimataifa.
- Kuhakikisha
kanuni za ligi zinasimamiwa vyema ikiwemo kanuni itakayomlazimisha kila mwalimu
wa ligi kuu na daraja la kwanza awe mwanachama wa TAFCA (chama cha makocha
nchini), walimu wa kigeni watapewa uanachama wa muda.
1.10 Timu za Taifa
Timu
zetu za Taifa, ziwe za wakubwa au za vijana ndio kioo cha mpira wa Tanzania. Jitihada zote lazima zifanyike kuhakikisha
tunakuwa na timu nzuri za Taifa kuanzia za wakubwa (wanawake/wanaume) hadi za
vijana. Pamoja na jitihada
zitakazofanyika kuboresha idara ya ufundi kama ilivyoanishwa hapo juu lakini
pia yafuatayo ni mambo ya ziada yatakayofanyika.
(a) Kuandaa fainali za Afrika za umri chini ya
miaka 17 (U-17) mwaka 2019
Hadi sasa hakuna nchi ambayo imekwisha pata uenyeji wa mashindano haya. Uenyeji
huu unatolewa na Shirikisho la vyama vya mpira Afrika CAF.Hii ni changamoto
kwetu Watanzania kuomba uenyeji huu.Tukipewa fursa hii itatusaidia sana
kutusukuma tuanze kuandaa programu ya nguvu ya miaka mitano ya kupata timu yetu
itakayocheza katika fainali hizi kama wenyeji.
Aidha kama nchi tutalazimika kuboresha miundo mbinu yetu hususani
viwanja vyetu vya mpira, jambo ambalo litatusaidia siku za usoni. Ninaamini uwezo wa kuandaa mashindano haya
kama nchi tunao. Nikichaguliwa nitalisimamia hili.
(b) Nidhamu
TFF itaandaa Kanuni za Nidhamu (code of ethics) kwa wachezaji, walimu na
viongozi wa Timu za Taifa mara wawapo ndani na nje ya uwanja. Hii itasaidia kujenga nidhamu ya timu. Kanuni
hizi zitaendana sambamba na kanuni za maadili za TFF.
(c) Walimu
Ni vyema siku za usoni timu zetu zote za Taifa zikafundishwa na makocha
wazawa.
Utaratibu utafanyika kuhakikisha makocha wasaidizi ambao ni wazawa wanaendelezwa
kufikia kiwango hicho, hii itakuwa ni pamoja na kuwapatia fursa za mafunzo
ndani na nje ya nchi.
(d) Zanzibar
TFF kwa kushirikiana na Chama cha
Mpira Zanzibar ZFA tutahakikisha kunakuwa na mahusiano ya karibu ya walimu wa
timu za Taifa Zanzibar na Bara ili kuhakikisha timu bora ya Taifa inaundwa na
vijana wa pande mbili za Muungano. Aidha jitahada za Zanzibar kuwa mwanachama
kamili wa CAF na FIFA zitaendelea kuungwa mkono.
2.
Utawala
Inabidi
tuendeleze utamaduni wa kuendesha shughuli za TFF kitaasisi (to have a corporate culture).Nguzo muhimu za uendeshaji
shirikisho kitaaluma ni pamoja na kujenga nidhamu ya wafanyakazi,heshima kwa
uongozi,utunzaji wa kumbukumbu,ukarimu kwa wageni,umakini katika manunuzi na
utunzaji wa fedha pamoja na kufanya kazi kwa malengo na kuhakikisha malengo
hayo yamefikiwa.
Maeneo yafuatayo yataboreshwa ili kuongeza
ufanisi:
2.1 Ofisi za Mikoa na Vyama
Shiriki
Kwa
kuzingatia vyama vya Mikoa kuwa ndio muendelezo mkuu wa shughuli za TFF Mikoani, ni muhimu ofisi za mikoa zikawa
kielelezo cha ufanisi wa utendaji wa TFF.
Ofisi za Mikoa zitaboreshwa hasa kwa kupewa vitendea kazi hususani vifaa
vya mawasiliano.
Vyama
shiriki hadi sasa havina ofisi zenye hadhi ya vyama hivi, tutahakikisha
tunaondoa aibu hii. Aidha kutokana na mapato ya TFF sehemu ya mapato haya
itatengwa kwa ajili ya ruzuku ya kupeleka kwenye vyama vya Mikoa na vyama
shiriki ili isaidie kupunguza makali ya kuendesha vyama vyetu.
2.2
Ofisi ya Rais
Kutakuwa na ofisi ya Rais wa TFF. Ofisi ya Rais wa TFF (office of the
President) lazima iimarishwe na iwe sehemu itakayoweza kukabiliana na
changamoto za maendeleo ya mpira wa miguu. Rais wa TFF ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za mpira wa
nchi hii,lazima awe na mahali stahili pa kufanyia kazi kulingana na hadhi
yake.Hii itakuwa ni pamoja na kuwa na wasaidizi wenye uweledi wa kutosha katika
shughuli za kila siku za kuongoza shirikisho.
Ofisi za TFF makao makuu uwanja wa Karume zitakarabatiwa na kuongeza
nafasi ya kufanyia kazi.
2.3 Maslahi
Maslahi
ya wafanyakazi wa TFF yataboreshwa ili kuwaongezea motisha. Hii itakuwa ni pamoja na kuwapa fursa ya
kuhudhuria mafunzo mbalimbali.
2.4 Vilabu vya Mpira
Vilabu
vitasaidiwa kupewa mwongozo wa kujiendesha kwa ufanisi zaidi. Aidha utaratibu wa mgawanyo wa mapato ya
milangoni utatazamwa upya kwa lengo la kuhakikisha vilabu vinapata mgao mkubwa
kuliko iliyo sasa. Hii ni kwa kuzingatia
gharama kubwa wanazoingia vilabu katika kuandaa timu ikiwemo malazi, usafiri,
vifaa, posho, dawa, mishahara n.k.
2.5
Wachezaji wastaafu
Hii
ni hazina ya Taifa,kustaafu kwao kucheza mpira sio mwisho wao wa kuchangia
maendeleo ya mpira wa nchi yetu.Jitihada zitafanyika kuanzisha mfuko maalum
(Trust Fund) ambao utachangiwa na wachezaji wenyewe wanapokuwa bado dimbani
pamoja na TFF, hii ni kwa ajili ya kuwasaidia hapo baadae wanapokuwa na
matatizo hasa ya ugonjwa. Aidha chama cha wachezaji wastaafu (SPUTANZA)
kitapewa ofisi na kitaimarishwa ili kiwe kiungo muhimu kati ya wachezaji na
TFF.Wachezaji watahimizwa watumie chama hiki kutatua matatizo yao na chama
kitapewa fursa kikanuni ya kuwa mtetezi mkuu na msimamizi wa maslahi ya
wachezaji.
1.
TFF inatengeneza utaratibu mzuri wa kuuza bidhaa zake ndani na nje ya
nchi kwa kupitia uuzaji wa kawaida na wa mtandao.Mikataba itaandaliwa ili kudhibiti
uuzwaji holela wa bidhaa za TFF.
2.
Vyumba vya Maduka vinajengwa kuzunguka uwanja wa Karume
na kukodishwa.
3.
Jengo la kitega cha uchumi litajengwa kwenye ardhi ya
Uwanja wa Karume.Pia jukwaa la watazamaji litajengwa uwanja wa Karume
ili mechi ambazo sio kubwa ziweze kufanyika pale, hii itaviongezea vilabu
mapato.
4.
Juhudi za
kuboresha ukusanyaji, usimamizi na mgawanyo wa haki wa mapato ya milangoni
yatokanayo na ligi yetu utaboreshwa ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya
kupitia njia mbali mbali zikiwemo za udhamini mbadala kwa vilabu.Aidha jitihada
ambazo tayari zimekwisha anza za kuunda bodi ya kuendesha ligi na uanzishwaji
wa utaratibu huru wa kuendesha ligi zitaendelezwa ili kuongeza ufanisi,kuinua
mapato ya vilabu na kuongeza msisimko wa ligi.Ninaunga mkono juhudi hizi.
5. Viwanja
vingi vya mpira nchini vinamilikiwa aidha na Halmashauri,Serikali kuu au vyama
vya siasa.Viwanja hivi vingi viko katika hali mbaya kuanzia nyasi ,hali ya
uzio,vyumba vya kubadilishia nguo,mageti,vifaa vya kuzimia moto n.k.ni vyema
TFF na vyama vya mikoa kwa kupitia utaratibu wa PPP (Public Private Sector
Partnership) vikaingia ubia na wamiliki wa viwanja hivi ili TFF na washirika
wake wachukue jukumu la kuviboresha,kuvisimamia na kuviendesha ili kuhakikisha
vinakuwa katika viwango stahili kwa mujibu wa kanuni za FIFA na CAF.Hii
itaongeza usalama wa wachezaji na watazamaji na kuinua mapato yatokanayo na
viwanja hivi
Ushiriki wa wadau
Kwa sasa taswira ya mpira wa miguu inawafungia nje wadau
wengi ambao kama wangepewa fursa ya kushiriki nao wangetaka wachangie maendeleo
ya mpira wa miguu.Juhudi kubwa inabidi zitumike kurudisha imani hii ili kuleta
hisia za umoja wa kitaifa katika kuendesha mpira wetu (sense of belongingness)
.Ni muhimu taasisi muhimu za kitaifa zishirikishwe katika sekta hii ya mpira wa
miguu ,hii ni pamoja na taasisi kama Tacaids,Mashirika ya utalii kama TANAPA na
TTB,Umoja wa wafanyabiashara kama TPSF,CTI na TCCIA ,Kituo cha uwekezaji TIC n.k.Ushirikiano
huu utasaidia kujenga jina la Tanzania pale tunapoandaa michuano ya kimataifa
na pia kuhamasisha vijana wetu waepuke maisha hatarishi kama vile kujihusisha
na ngono isiyokuwa salama,madawa ya kulewa (kutumia na kusafirisha),ulevi wa
kupindukia n.k.
HITIMISHO
Ndugu zangu,nihitimishe
kwa kusisitiza kuwa maendeleo ya mpira Tanzania kwa hapa yalipofikia yanahitaji
ubunifu,ujasiri na msukumo mpya ili tuweze kuunyanyua mpira wetu na kuupa
mwelekeo mpya,mwelekeo wa matumaini ,mwelekeo wa kulipeleka soka letu katika
kushinda vikombe vikubwa barani mwetu Afrika na Duniani.
Shime wapiga kura nipeni fursa hii
ya kuwa Rais wa TFF ili kwa pamoja tukishirikiana na wadau wote muhimu katika
sekta yetu tuweze kulisikuma gurudumu hili ili hatimae soka iweze kuiletea nchi
yetu sifa na kuwapa raha mamilioni ya watanzania wapenda mpira.
Pamoja tutaweza
Chagua MALINZI
Chagua MABADILIKO
Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Jamal Malinzi
Mgombea nafasi ya Urais
TFF
2013
Mpira ni afya, mpira ni burudani, mpira ni ajira kwa vijana!
MAELEZO BINAFSI YA JAMAL
EMIL MALINZI MGOMBEA URAIS TFF
Tarehe ya kuzaliwa : 08 Agosti, 1960
Elimu: 1974-1977 : Sekondari O-Level
Mwanza
Secondary School
1978-1981 : A-Level
Ilboru
High School
1980-1981 : JKT – Ruvu
Operesheni TIJA
1981-1985 : Chuo Kikuu Dar Es Salaam
Digrii
ya Uhandisi (Upper 2nd Class)
1986-1993
: Ajira -Coopers
and Lybrand
Tanzania
Industrial Research
and Development
Organization
1993-Hadi Leo : Mjasiriamali
Mkurugenzi
– Cargostars Limited
Michezo : Nimekuwa promota wa mchezo wa ngumi
za kulipwa
kuanzia kipindi
cha 1995-2001. Baadhi ya mabondia wangu
walifikia kiwango cha kimataifa hadi kusaini mkataba na Promota maarufu duniani
Don King.
: Nimekuwa Seneta wa
Yanga na baadae nikawa Mkurugenzi na mwisho nikawa Katibu Mkuu wa Klabu ya
Yanga kati ya mwaka 1999 na 2005.
: Nimekuwa Mkurugenzi na
Msimamizi Mkuu wa Timu ya Mkoa wa Dar Es Salaam ya Mzizima United. Timu hii ndiyo ya mwisho kushinda Kombe la
Taifa mwaka 2007 ikiwa timu moja ya Mkoa wa Dar Es Salaam.
: Nimekuwa mjumbe wa
Baraza la michezo la mkoa wa Dar es salaam 2009-2011
: Nimekuwa Mwenyekiti wa
kamati ya mashindano mkoa wa Pwani 2009-2011
: Hadi sasa mimi ni
mwenyekiti wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Kagera
: Kikampuni, Kampuni yetu
ya Cargostars Limited ina uzoefu wa muda mrefu wa kudhamini michezo
mbalimbali. Kwa kipindi cha miaka saba
Cargostars Limited iliidhamini mbio za marathon za wabunge. Aidha Cargostars Limited ina rekodi ya
kudhamini michezo mingine kadhaa ikiwemo mpira wa miguu, ngumi, Tennis na Golf.
Hizi zote mbwembwe mkipewa ofisi mtasema kuwa ROMA pia haikujengwa kwa siku moja.Sasa ndugu yangu MALINZI (mtani wangu) mimi langu moja kila timu iwakatie bima wachezaji wake hata kama ni kwa bei ya chini kupitia NHIF.Hili suala liwe compulsory kinyume na hapo timu haishiriki ligi kuu.Pia wachezaji wakati wa kusajiliwa wafanyiwe vipimo vya afya ikiwemo pamoja na kuwapima mifupa ili kujua umri wao(MRI).Pia kukazia ujenzi wa viwanja kuanzia na kanda ili angalau uwepo uwanja mmoja ambao ni wa kutolea mfano ambapo timu zote za ligi kuu za kanda husika zitakuwa zinacheza hapo.Sasa kwenye hili inabd baadhi ya mapato yatokane na asilimia fulani kwenye mapato ya mechi za taifa stars na mapato ya mechi za ligi kuu kwenye mikoa ambayo ipo kwenye kanda pamoja na kufanya harambee.Haya mambo yanawezekana na sisi wananchi wenyewe tupo tayari.Mambo ya kujenga viwanja jirani hatutaki kabisa ONA taifa na uhuru hauwezi kuchezewa mechi siku moja.Uwanja mmojawapo hapo ungepelekwa mkoa mwingine.Ni kama vile kwenda kujenga hospital mpya ya muhimbili KIBAMBA ili hali TUMBI ipo jirani na KIBAMBA na kujenga TAIFA ili hali UHURU ipo usoni mwa TAIFA.Viongozi wetu nawalaumu kwa kufanya mambo kwa maslahi ya kisiasa bila kufanya tafiti.
ReplyDeleteVyombo vya habari sijui mmenunuliwa na huyu Malinzi,mbona hatuwasikii wagombea wengine?au anagombea peke yake
ReplyDelete