Search This Blog

Wednesday, October 2, 2013

JOHN BARNES NA LUCAS RADEBE WAWASIHI VIJANA KUWA NA MAPENZI YA MCHEZO KABLA YA KUANZA KUWAZA PESA.

Lucas Radebe na John Barnes walipokuwa wanahojiwa na mtangazaji wa Supersport Carol Tshabalala.

Wanasoka wa zamani John Barnes na Lucas Radebe wamesema siri kubwa ya mafanikio yao katika mchezo wa soka ilikuwa ni kutoweka mbele masilahi binafsi kama ilivyo kwa vijana wa sasa, wameyasema maneno hayo leo hii kwenye kongamano la SOCCEREX linalofanyika kwenye uwanja wa Moses Mabhida jijini Durban.
Beki wa zamani wa vilabu vya Kaizer Chiefs,Leeds Utd ya England pamoja na kikosi cha Bafana Bafana Lucas Radebe amesema wakati anachipkia kwenye mitaa ya Soweto yeye na vijana wenzake walikuwa wakiugombania mpira mmoja uliokuwa unamilikiwa na kijana mwenzao mtaani kwao, '' hatukuwa tunacheza ili tupate pesa pamoja na umaskini mkubwa uliokuwa unatukabili,bali mapenzi tuliyokuwa nayo juu ya mchezo wa soka ndio yalitusukuma sana kuucheza mchezo huo ''.

Naye kiungo wa zamani wa kimataifa wa England na vilabu vya Watford na Liverpool John Barnes amesema kinachowasukuma vijana wengi siku hizi kucheza soka ni ndoto zao za kuvichezea vilabu vikubwa ulimwenguni kama vile FC BARCELONA na CHELSEA, '' siku hizi vijana wengi wanacheza ili wasajiliwe na vilabu vikubwa,ikitokea hajasajiliwa basi wanaamua kuachana na mchezo wa soka''.

No comments:

Post a Comment