Makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Arsenal na chama cha soka cha England bwana David Dein amesema kuwa bara la Afrika litapata mafanikio makubwa kwenye medani ya soka siku ambayo litaacha udanganyifu wa umri kwa wachezaji wake.
Dein pamoja na raisi wa SAFA,Danny Jordaan walikuwa wakifanya mazungumzo na mtangazaji Thomas Kwenaite wa kituo cha Super Sport kwenye kongamano la siku mbili lililoandaliwa na SOCCEREX jijini Durban nchini Afrika Kusini.
Dein amesema kuna mambo mengi yaliyofanya mapinduzi makubwa ya mchezo wa soka ndani na nje ya bara la Afrika lakini waafrika wengi hawayajui,mfano suala la udanganyifu wa umri limekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo ya soka barani Afrika.
'' Siku moja nilitaka kumnunua mchezaji wa kiafrika,ikabidi nimuulize wakala umri wa mchezaji wake,yule wakala akanijibu nataka kufahamu umri halisi au kufahamu umri wa kazi,huwezi amini nilijihisi kuchoka papo kwa hapo,ndipo nilipogundua kumbe wanasoka wa Afrika wana umri wa aina mbili ''
Ili kuepukana na mambo ya kudanganya umri hizi ndio sifa mchezaji anatakiwa kuwa nazo ili aweze kusajiliwa na klabu ya Arsenal na pia vilabu vingine vikubwa barani ulaya.
1. TECHNIQUE
Kwenye kipengele hiki David Dein amesema mabara ya Afrika na Amerika Kusini ni migodi ya vipaji vya wanasoka.
anasisitiza Umri wa kijana kujifunza mbinu za soka ni kuanzia umri wa miaka 8 hadi 12 lakini kwenye umri huo vijana wengi wa kiafrika hawahitaji kufundisha hizo mbinu kutokana na vipaji vikubwa walivyozaliwa navyo.
2. PHYSIQUE
David Dein anasema sifa namba moja ya wachezaji wa kiafrika ni kuwa na nguvu za asili,umri mzuri wa kujiandaa na mazoezi ya kujenga mwili ni kuanzia umri kati ya miaka 12-16 mpaka miaka 18,lakini wachezaji wengi wa kiafrika katika umri huo wanakuwa tayari na nguvu za kutosha
3. AWERENESS
Dein amesema mchezo wa soka unahitaji maamuzi mengi ndani ya muda mfupi na hiki ndio haswaa kikwako kikubwa cha wanandinga kutoka barani Afrika,kitendo cha wanasoka wengi kutoka barani Afrika kutokuwa na uwelewa wa kutosha juu ya mchezo wenyewe kimekuwa kikiwaghalimu mno,
'' mchezaji yeyote mwenye kufahamu mambo mengi yanayohusu mchezo wa soka ni rahisi kwake kufanya maamuzi ya haraka''
4. FOOTBALL INTELLIGENCE
‘Football intelligence’ ni moja ya sifa muhimu ambayo kila mwanasoka anapaswa kuwa nayo,
5. FOOTBALL DESIRE/HUNGRY
Hapa alikuwa anasisitiza kuweka mapenzi na uchu wa kucheza kwanza kabla ya kufikilia pesa,anasema ni kosa la jinai kwa kijana mwenye umri wa kuanzia miaka 16 kufikilia zaidi kipato,moja ya changamoto kubwa ya wanasoka wa kiafrika ni kuridhika mapema.
6. BEHAVIOUR/ATTITUDE
Tabia njema ndio humjenga mchezaji,wanasoka wengi wa kiafrika wanapenda sana starehe wanapofika barani ulaya,hutumia muda mwingi kula starehe kitendo ambacho huwapelekea kupunguza muda wa mazoezi.
Ndugu zangu wabongo,tujiulize kama sifa hizo zipo kwa wachezaji wetu,km hazipo kwa nini wanajfanya nao ni profeshno players? Jamani soka lina kanuni na tartibu zake,tuache siasa tufuate misingi ya soka. Wabongo tunataka kuwafundisha wachezaji wakishakuwa wazee,wapi na wapi hiyo!
ReplyDelete