Search This Blog

Monday, September 30, 2013

UJENZI WA UWANJA WA YANGA: TAARIFA KUHUSU MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA UWANJA WA MPIRA


LEO tungependa kupitia kwenu kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wetu wa Uwanja wa kisasa wa mpira katika Jiji la Jangwani kama itakavyojulikana

Mara ya mwisho tuliongea ama kuonana ilikuwa mwezi wa tatu wakati Ndugu zetu wa BCEG walipokabizi Concept design ama Usanifu wa awali na kuanzia sasa tutakuwa tunatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu mradi huu. Wahenga walisema UKICHA KUSEMA HUTATENDA JAMBO lakini pia KUKAA KIMYA SANA kunajenga hisia mbaya na kutoa nafasi ya upotoshwaji wa habari.

Kwa kifupi napenda kuwakumbusha kuwa Makubalino ya Awali (Memorandum of Understanding) yalisainiwa 23 Novemba 2012. Pamoja na mengineyo YANGA inatakiwa:

· Kupata na kuwa na eneo la kutoshereza malengo ya mradi

· Kupata ushauri mzuri, michoro mizuri na mkandarasi mzuri wa mradi

· Kupata na kutenga fedha za kukamilisha usanifu na ujenzi wa mradi

Kwa upande wa BCEG wajibu wao ni kuwa na utaalamu na uzoefu wa kutosha. BCEG wameandaa na kukabidhi michoro ya usanifu wa awali kukidhi matakwa ya YANGA. YANGA tunatakiwa kutoa maoni yetu na na kuingia RASMI mkataba wa ujenzi.

Kutokana na kukua kwa Jiji la Dar es Salaam, na katika hali ya kutaka klabu iwe na vitega uchumi klabu imeonelea ni vyema kama ingekuwa na uwanja wa mpira wa karne ya sasa na baadaye ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na mioundombinu ifuatayo:-

1. Uwanja wa mpira wenye viti 40,000

2. Hostel ya wachezaji na football academy ya vijana

3. Viwanja vya mazoezi

4. Uwanja wa kutosha kuegesha magari

5. ­­­­­Hoteli na sehemu ya makazi

6. Ukumbi wa mikutano

7. Sehemu ya maofisi, benki, zahanati (sports clinic)

8. Maduka, supermarket na sinema

9. Sehemu za kubarizi, kupumzikia (Recretional and Open spaces)

Mara baada ya azma yetu kukamilika eneo hili litaitwa “Jangwani City” na kufanya wakazi wa maeneo ya Jangwani na sehemu za jirani wasiende maeneo ya mbali kutafuta huduma muhimu za kijamii. Eneo hili litaboresha mandhari nzima ya Jangwani kwa kukuza mazingira na miundombinu. Hii itahusu pamoja na mambo mengine ujazaji udongo (tuta kubwa), upandaji miti, bustani za kubarizi, kuboresha mifereji ya majitaka na kudhibiti mafuriko ya eneo la Jangwani na hivyo kulipatia sura ya kibiashara na kitalii.

Ili kukamilisha azma ya kuwa na Jangwani City itakayo kuwa na miundombinu yote hiyo, Uongozi ulipeleka maombi ya eneo la nyongeza Manispaa ya Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa barua zenye kumbukumbu namba YASC/ARDHI/MWK/YM/46/2012 na YASC/ARDHI/MWK/YM/47/2012 za 12 Desemba 2012, na mpaka sasa bado maombi yetu hayajajibiwa.

Mwezi wa saba, Wadhamini/Uongozi wa YANGA walimwandikia Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuomba msaada wake kufanikisha maombi ya nyongeza ya kiwanja yaliyowasilishwa Manispaa ya Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Klabu ya Yanga ina kiwanja chenye ukubwa wa hekta 3.59 eneo la Jangwani. Kiwanja hiki kina hati miliki kwa miaka 99 toka mwaka 1972 na katika eneo hilo, klabu ilifanikiwa kujenga uwanja wa mpira wa Kaunda na Jengo la klabu la ghorofa tatu. Jengo hili lilijengwa kwa ufadhili mkubwa sana wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume (Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi) na michango ya wanachama na wapenzi wa klabu ambao kila siku wamekuwa wakiamini kuwa haba na haba hujaza kibaba.

Ndugu Wandishi wa habari kwa kifupi tumefikia hapo, zoezi la kutoa maoni yetu kuhusu michoro ya usanifu wa awali na kuingia rasmi mkataba wa ujenzi na BCEG limesimama, likisubiri majibu ya nyongeza la eneo. Ni matumaini yetu zoezi hili litakamilika hivi karibuni na kuendelea na mradi.

YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO

Dar es Salaam, 30 September 2013

Francis Mponjoli Kifukwe

9 comments:

  1. KIU HAIJAKATIKA. Ahsanteni viongozi kwa taarifa ila bado hamjakata kiu ya wana yanga. Bado wana yanga tunajiuliza nini hatma ya mipango hii iwapo serikali itaendelea kukaa kimya. kwa nini kusiwe na alternative solution? Jangwanini City inaonekana ni project ya muda mrefu, kwa nini kusiwe na mpango wa muda mfupi ambao utawezesha angalau klabu kupata kiwanja cha mazoezi ambazo kwa hakika kinahitajika sana? Taarifa iliyotolewa bado haijaondoa hofu yetu juu ya uwezekano wa uongozi kuondoka madarakani kabla hamjafanya kitu. Please fanyeni angalau kidogo ambacho kitakuwa "tangible" angalau tuje tuwakumbuke kwa kutufanyia kitu kidogo kuliko kuwakumbuka kwa kuwa na mipango mizuri ambayo hamkuitekeleza."DAIMA MBELE NYUMA MWIKO".

    ReplyDelete
  2. Rushwa inatakiwa ndo wahusika washughulikie, hili ni tatizo kubwa kwenyenchi yetu, miezi 7 hawajibu?

    ReplyDelete
  3. Yanga acheni longolongo mtaombaji eneo la Viwanjani vya Jangwani ili kujenga kitegauchumi cha Manji kama kaeneo kenu kadogo nendeni nje ya mji.Mikutano ya siasa na dini ifanyikie wapi na watoto wetu awcheze wapi. Hilo ni eneo la watanzania wote msituletee utapeli. Serikali ikiwapa na sis tutaomba barabara ya msimbazi ifungwe tujenge Vitegauchumi vya simba.

    ReplyDelete
  4. Hizo zote ukisikia siasa za mpira ndyo hzi yaan wamekaa wametafuta sehm ya kutokea wameamua kuandka barua serikali iwapewe open space wajenge kitega uchumi kitu ambacho wanajua hakiwezekan, ktk hali ya kawaida hvi kila taasisi or mtu akitaka kuanzisha kitega uchumi chake na eneo lake halitoshi aandike apewe eneo kweli itakuwaje? Let me go 2 the point, kwanza hyo mipango yote wala cjackia where iz a source of income au ndyo hzo get collections? Yaan ili dogo tu lakudhibit matumiz holela ya nembo ya club kwa timu zote hzo za simba na yanga ambalo angalau linaonekana jepesi wanashindwa alafu leo wanatujia na maproposal ya pesa nyingi kama hizo hivi nyie viongoz kwan cc mnatuonaje? Suala la cc kununua mijez imetapakaa mtaan alafu club zetu hazifaidiki hata na senti tano mnadhani cc halituumizi? Achez upumbavu wenu uo na nyinyi wanachama hili hamlioni? Alafu watu wanacmama hapo mbele serikali inatukwamisha hovyo kanunueni eneo kubwa nje ya mji kama walivyofanya azam mnashndwa nn? Uwanja wa mazoezi tu unawashnda ndyo mnakuja na project kubwa kama hzo mtaweza wap et uwanja unafunguka kwa remote my black a***s kama utajengwa uo may b nt in dc life tym labda wakijtahd xana kama azam complex hata nayo am nt sure kwani hawa sio wakwanza tumeshawackia xana kina kaduga, rage, na wengine lakini adi leo hakuna lolote porojo tu! Ally mdau tms

    ReplyDelete
  5. Tatizo la young ni maneno memgi kuliko vitendo jaani lakini yebo yebo jitahidinii

    ReplyDelete
  6. Ntaishangaa sana serikali ikiwapa hilo eneo kwasababu ninauhakika wanakiona kinochoendelea mabarabarani bcoz of poor planning of gvnt offices na pia kwa ushauri tu,ili nchi iendelee lazma vitu visambazwe jamani.....UONGOZI WA YANGA HAPO MNACHEMSHA.
    Au ni mpango wa MANJI kweli kama mdau hapo juu alivyosema....!

    ReplyDelete
  7. Yanga acheni longolongo mtaombaji eneo la Viwanjani vya Jangwani ili kujenga kitegauchumi cha Manji kama kaeneo kenu kadogo nendeni nje ya mji.Mikutano ya siasa na dini ifanyikie wapi na watoto wetu wacheze wapi. Hilo ni eneo la watanzania wote msituletee utapeli wenu kwa mgongo wa Yanga. Serikali ikiwapa na sisi tutaomba barabara ya msimbazi ifungwe tujenge Vitegauchumi vya simba.
    CCM nao waombe viwanja vya mnazi mmoja wajenge waingie ubia wajenge vitegauchumi na ikiwezekana kila taasisi iombe eneo la wazi kama Yanga

    ReplyDelete
  8. Nadhan mmetoa maoni mkiwa munaumia "Why Yanga", huo ni uzembe tu wa kutofikiria. Unaposema utaishangaa serikali, mara nasisi tutaomba sijui barabara gani tujenge, watoto wetu watacheza wapi hayo yote ni uchakavu wa mawazo tu. Hata wakinyimwa wewe utakayefurahi utahamia hapo?. Kuna aliyekaukiwa mawazo anadai kitegauchumi cha Manji wewe nakuhurumia kwakuwa ni mzembe hadimu.
    Mnajiona wazima hamjui ujinga nao ni ugonjwa! Karibuni jamani mtoe maoni hapa nilikuwa nawasalimu tu mlio jisahau.

    ReplyDelete