Search This Blog

Monday, September 30, 2013

UCHAMBUZI - SIMBA SC 2-0 JKT: SIMBA SC NI WAZITO SANA, JAPO WANASHINDA


Na Baraka Mbolembole Mabadiliko yakumtoa nje kiungo Amri Kiemba na kumuingiza uwanjani chipukizi RamadhaniSingano, awali yalionekana kama yangeipa wakati mgumu zaidi timu ya Simba mchezoni. Ila kocha Abdallah ‘King’ Kibadeni aliendelea kuwaamini kundi la wachezaji wake vijana alionao kikosini na kupata pointi nyingine tatu muhimu na kujitanua katika kilele cha msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.

Emmaneul Switta alionekana bora zaidi kwa karibu muda wote wa kipindi cha kwanza, na kiungo wa timu ya JKT Ruvu alionekana kuwa na kasi zaidi, ujanja zaidi, na uamuzi wa haraka kuliko wale viungo wa Simba. Katika mfumo wa 4-4-2 ambao , kocha ‘ King’ aliamua kuanza nao, Simba ilijikuta ikibanwa kwa muda mrefu na timu ya JKT Ruvu, huku timu hiyo ya kocha Mbwana Makatta ikionekana kuwa na kasi zaidi kuliko Simba.

Mpira mrefu usiotarajiwa uliokuwa umepigwa na mlinzi wa kulia, Haruna Shamte ulizaa mkwaju wa penati, ambao mshambuliaji Amis Tamwe alifunga bao la kuongoza katika dakika ya 24, huku likiwa bao lake la saba katika michezo mitatu iliyopita. Lakini bado Switta alionekana kutawala eneo hilo la katikati ya uwanja ambalo kwa upande wa timu ya Simba, Said Ndemla na Abdulhalim Humud walianza katika eneo hilo lakini walikuwa ni wazito.

King, akaamua kumtoa Kiemba ambaye alikuwa akicheza chini ya kiwango chake cha kawaida, Kiemba ambaye alipangwa upande wa kushoto na wakati mwingine akicheza upande wa kulia, alikuwa mzito sana na wakati Humud alikuwa akitumia muda mwingi kukaa na mipira. Viungo hawa wawili hawakuwa na kasi kabisa na hilo lilipelekea walinzi wa pembeni wa JKT Ruvu, Nashon Naftal na Stanley Nkomolla kupanda na kuwapa kazi zaidi walinzi wao wa pembeni.

Mabadiliko ya kwanza ya mchezo huo kutoka kwa Kiemba yaliwapa, Simba kasi tofauti na alivyokuwepo Kiemba uwanjani. Na baada ya kutoa matunda mazuri, King akaamua kumuingiza uwanjani Martin Kaeza, mahali kwa Haruna Chanongo na dakika 25 kabla ya mchezo kumalizika, akamuingiza mshambuliaji kinda, Miraj Athuman kuchukua nafasi ya Betram Mombeki. Timu ikaoneka kupata kasi zaidi, na hata Humud aliongeza kasi yake uwanjani na kusadia kutengeneza bao la pili, baada ya kukimbia na mpira kwa kasi na kupiga pasi ndefu na Singano alitumia kasi yake kufunga bao la pili. Hii ilikuwa ni dakika ya 50 ya mchezo.

KIUNGO BADO DHAIFU 
Jonas Mkude hakuwepo katika mchezo wa leo, hivyo alipata nafasi, Ndemla. Katika michezo iliyopita safu ya kiungo ilikuwa ikianza na Mkude, Ibrahim Twaha, Chanongo na Kiemba na timu ikaweza kuonesha kasi mchezoni. Ila katika mchezo na JKT Ruvu, Switta alionekana kuwa na kasi zaidi, na mchezaji ambaye alionekana kuichezesha timu yake vilivyo. Ukuta wa Simba ulifanya kazi, walimzima kabisa mshambuliaji, Shaaban Kondo pamoja napatna wake Emmanuel Pius, lakini walinzi wao wa pembeni walikimbizwa kwamuda mwingi wa mchezo na mawinga, Haji Zege na Salum Machaku.

Ndemla alionekana kuwa na kasi lakini kila mpira ulipokuwa ukifika kwa Humud ‘ ulipoa’. Humud ni kiungo anayependa kuuchezea mpira kabla ya kupiga pasi kwa mchezaji mwenzake, hilo lilifanya muda mwingi safu ya mashambulizi kushindwa kupata mipira katika wakati sahihi, Ila napenda kuwasifu JKT Ruvu namna walivyoweza kucheza. Walikuwa na kasi nzuri, pengine mbinu zao ndogo za kulazimisha matokeo ziliwanyima walau pointi moja. Ambayo ilikuwa ndani ya uwezo wao kuipata. Kutokuwepo kwa Mkude, hakukuwa na tatizo , ila wachezaji ambao wanakuwa wakipata nafasi wanatakiwa kucheza kwa kiwango cha juu kama yeye au zaidi yake.. Namna Humud alivyosonga mbele na mpira ambao ulizaa bao la pili la Simba ni dalili kuwa wachezaji vijana waliweza kuongeza kasi ya timu nzima.

Baadae, kocha Makatta akamtoa Switta baada ya kuonekana kuchoka na kumuingiza Richard Msenya, na hata walipokuja kuingia wazoefu, Amos Mgissa na Paul Ndauka bado Simba walionekana kutulia na kucheza vizuri. Simba wameshinda, Ndiyo, ila hawatakiwi kubweteka sana kwakuwa bado wanakasi ndogo mchezo. Mara mbili timu ya Rhino Rangers ilisawazisha mabao ya Simba, mwezi uliopita na wiki iliyopita Mbeya City pia ilisawazisha mara mbili. Hiyo ni ishara kuwa pamoja na mafanikio yao ya kuongoza ligi bado wanaweza kufungwa na timu ambazo hutumia mbinu, ufundi na kasi zaidi yao. Kuwa na safu ya mashambulizi ya wachezaji kama Tambwe na Mombeki ni vizuri, ila ni namna gani wanaweza kunufaika nao ni kurejea katika michezo iliyopita na kutazama wamewezaje kufunga mabao 15 katika michezo sita iliyopita. Tambwe ana umbo zuri, ni mrefu na ana uwezo wa kuruka juu, ukichunguza kwa makini utagundua kuwa amekuwa akifunga mabao yake akiunganisha krosi za Chanongo, Singano na mipira ya kupenyezewa. ILa yote hayo yanawezekana ikiwa timu inakuwa katika kasi . Alibanwa sana na walinzi, Damas Makwaya na Jamal Mtaki kwa kuwa timu ilikuwa ikicheza taratibu mno. Simba inashinda, ndiyo, ila Kasi yao bado ni ndogo. 0714 08 43 08

3 comments:

  1. Kama ruvu jkt walikua bora kuliko simba na switta alikua bora zaidi mwepesi zaidi na kasi zaidi mbona vyote hivyo havikusaidia timu yake kupata ushindi.unakuwaje na kiungo bora na mwenye kasi zaidi ya viungo wote ws upinzani halafu ushindwe kupata matokeo au kiugo wako bora alicheza na majukwaa au wewe unakasoro katika uchambuzi wako

    ReplyDelete
  2. nyie waandishi wa yanga acheni unazi timu ikifungwa mnaponda hata ikishinda mnaponda mnatakaje kitu gni zaidi ya ushindi kwenye game umekosa cha kuandika mtasubiri sana mwisho mtaipenda tu nyekundu

    ReplyDelete
  3. Tambwe sio mrefu kiivo bana ila ni tu ni mjanja sana na fundi mkali wa positioning +timing + target!! Otherwise naunga mkono ni ushauri wa kweli+ wa manufaa kwetu msimbazi!!

    ReplyDelete