Siku chache tu baada ya kutumia kitita kikubwa
kumsajili Gareth Bale kutoka klabu ya Tottenham hotspurs ya England Real
Madrid imetangaza kupanda kwa faida katika mapato yake na punguzo la
asilimia 27.4 ya deni lake katika kipindi cha msimu wa mwaka 2012/13.
Magwiji hao wa soka ya Uhispania mapato yao yakipanda hadi
Euro milioni 520.9
Mapato hayo hayahusishi udhamini mkubwa wa Fly
Emirates wa jezi za klabu unaokadiriwa kua euro milioni 29 kwa kila
mwaka kuanzia msimu huu.Pamoja na usajili wa Bale, Real ilitumia euro milioni 70 kwa kuwapata Isco na Asier Illarramendi.
Vilevile klabu hio ilirejesha takriban euro milioni 100 katika kuwauza wachezaji wake Mesut Ozil aliyejiunga na Arsenal kunako siku ya mwisho wa usajili na Gonzalo Higuain, Raul Albiol na Jose Maria Callejon waliojiunga na Napoli mwezi julai.
Uamuzi wa Kaka kuondoka Real Madrid na kurudi AC Milan pia kulipunguza kiwango cha mishahara ya klabu hiyo kwa mshahara wake wa euro milioni 10 kwa mwaka wake wa mwisho lau kama angehitimisha mkataba wake.
No comments:
Post a Comment