Isha Johansen - Raisi wa Shirikisho la Soka la Sierra Lione |
Johansen alikuwa Zurich wiki iliyopita kukutana na raisi wa Fifa Sepp Blatter wakati wajumbe wa kamati kuu ya SLFA wakiwa busy kutafuta suluhisho la matatizo na kuianzisha upya ligi, ambayo imesimama tangu mwezi Julai.
Utawala wa Johansen umedhamiria kuianzisha ligi hata kama ikiwa vilabu vitaendelea na uamuzi wao wa kuisusa ligi hiyo ya juu kabisa katika mfumo wa soka wa nchi hiyo. Vilabu 10 kati ya 14 vinavyoshiriki katika Premier League vimegomea kucheza ligi hiyo katika kupinga uamuzi wa iliyokuwa kamati ya uchaguzi ya SLFA kumuondoa gwiji wa soka wa nchi hiyo Mohamed Kallon, Rodney Michael na Foday Turay katika kugombea nafasi ya uraisi katika uchaguzi ambao umemleta Johansenkwenye madaraka.
Hili lilisababisha waandaji wa ligi kuisimamisha ligi hiyo.
Uongozi wa Johansen tayari umeshafanya vikao kadhaa na pande zote zenye malalamiko, vikiwemo vilabu lakini mpaka sasa hakuna kilichoeleweka.
Hata raisi wa nchi hiyo Ernest Bai Koroma amefanya vikao vitatu tangu ulipofanyika uchaguzi baina yake na watu wenye madai lakini kuingilia kwake hakujaleta mabadiliko yoyote.
Upande wa watu wenye malalamiko unataka kufukuzwa kazi kwa katibu mkuu wa sasa wa chama hicho cha SLFA Abdul Rahman Swarray pamoja na afisa uhusiano Sorie Ibrahim Sesay, ambaye kwa sasa yupo chini ya ulinzi wa polisi kutokana na matatizo yasiyohusiana na soka.
Swarray na Sesay wote wametuhumiwa kutoa majina ya uongo ya wawikilishi katika kikao cha uchaguzi ili kuunda kikundi cha kuweza kumpatia madaraka bila kupingwa raisi wa sasa wa SLFA Isha Johansen.
Wote wamekataa madai hayo au kujihusisha na jambo lolote lisilokuwa sahihi.
Mchezaji wa zamani wa Sierra Leone Brima Mazola Kamara. ambaye ni makamu wa raisi wa SLFA, aliviambia vyombo vya habari kwamba wameomba muda zaidi kuangalia namna ya kushughulikia masharti waliyotoa upande wa watu wenye madai.
Alisema: "Tunaamini tulichaguliwa kwa haki kabisa. Hatuwezi kufukuza tu watu bila sababu za msingi na ndio maana tumeomba muda wa kuangalia zaidi haya madai yao."Tutakuwa na mkutano na vilabu vyote vilivyogoma jumanne wiki hii na kuangalia ni namna gani wanaweza kurudi kuendelea kucheza ligi.
"Ikiwa watakataa basi tutaendelea na ligi na timu ambazo zipo tayari kucheza.
"Wachezaji wanateseka kutokana na hii hali ya ligi kusimama. Maisha yao ya kisoka pamoja na hali ya kimaisha kwa watatengeneza vipat vyao kama hawachezi mpira."
No comments:
Post a Comment