Akizungumza jijini Dar
es Salaam leo (Jumatano Sept 4), Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane
Matinde alisema wachezaji hao chipukizi watashughulikia na kukamilisha
hati zao za kusafiria kati ya kesho, Alhamisi na Ijumaa. “Kwa upende
wetu kila kitu kimekamilika kwa ajili ya safari kuelekea kwenye
mashindano hayo ya kimataifa ambayo yatashirikisha timu kutoka sehemu
mbali mbali barani Afrika,” alisema.
Jumla ya wavulana na
wasichana 32 walifuzu kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano
hayo baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu wakati wa
fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zilizofanyika jijini Dar es
Salaam mwezi Juni. Mashindano haya ya kimataifa yanafanyika kwa mara ya
pili mwaka huu yakiwa na lengo la kutoa fursa zaidi kwa wachezaji
chipukizi kuendeleza vipaji vyao.
Kwa mara ya kwanza
mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yalifanyika jijini
Nairobi mwaka jana ambapo Tanzania iliwakilishwa na timu ya wavulana
pekee ambayo hata hivyo ilitolewa hatua za awali huku timu ya Nigeria
ikitawazwa kuwa mabingwa.
“Kulingana na kiwango
cha kuridhisha cha wachezaji waliochaguliwa mwaka huu nina imani kwamba
timu zetu za Tanzania – wasichana na wavulana – wana nafasi nzuri ya
kufanya vizuri,” anasema Matinde ambaye ni mmoja wa maofisa wa Airtel
Tanzania waliongoza na timu kwenye mashindano hayo.
Airtel imeanzisha
mashindano haya ya vijana barani Afrika kwa nia ya kusaidia upatikanaji
wa vijana wenye vipaji vya soka kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ngazi
ya Taifa. Airtel Rising Stars inatoa fursa kwa vijana kudhihirisha
uwezo wao kwa makocha wa Taifa na kimataifa na kuweza kujiendeleza zaidi
kisoka.
Hivi sasa Airtel Rising
Stars ni moja ya matukio muhimu ya kisoka kwenye kalenda ya Shirikisho
la Mpira wa miguu nchini (TFF). Huanzia katika hatua ya usajili
ikifuatiwa na mechi za mtoano ili kupata wachezaji nyota wa kuunda timu
za mikoa ambazo huchuana katika ngazi ya Taifa.
Airtel inaendesha
muchuano hii kwa kushirikiana na klabu maarufu duniani ya Manchester
United ambayo hutoa ushauri wa kiufundi na michuano hii imekuwa na
hamasa kubwa katika nchi zote zinazoshiriki.
No comments:
Post a Comment