Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi na baba yake Jorge wamelipa kiasi cha £4.2million kwa mamlaka ya kodi nchini Hispania baadaya kutuhumiwa kujaribu kukwepa kodi - taarifa ya mahakama imesema jana Jumatano.
Wawili hao walitoa mkwanja huo mwezi uliopita kama na walikuwa wakitakiwa kuhudhuria mahakamani kwenye kesi mnamo September 17, ingawa wakili wao aliomba keshi hiyo iharishwe kwa sababu walikuwa na majukumu mengine siku hiyo.
Mchezaji huyo bora wa dunia na baba yake, wote waligoma kufanya makosa hayo, walituhumiwa kuficha zaidi euro millioni 4 wakati walipopeleka taarifa zao za mapato yao katika miaka ya 2006 mpaka
2009.
Uuzwaji wa haki za taswira ya Messi umekuwa ukifichwa kwa kutumia mtandao fulani katika nchi za
Uruguay, Belize, Switzerland na United Kingdom, mwendesha mashtaka ya jinai huko Catalonia alisema.
'Sijawahi kuhusika na suala kama hili hata baba yangu pia,' Messi alisema mwezi July.
No comments:
Post a Comment