Search This Blog

Tuesday, September 3, 2013

MJADALA: USAJILI WA MESUT OZIL NI TIBA YA UGONJWA UNAOKABILI ARSENAL? JE NI ATATUMIKA VIPI NDANI YA KLABU HIYO??????? TOA MAONI

Klabu ya Arsenal jana imekamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Mesut Ozil kwa ada ya uhamisho ambayo imevunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo.

Arsene Wenger amewatimizia ahadi mashabiki wa klabu hiyo kwamba tasajili mchezaji bora mwenye jina kubwa katika dirisha la usajili ambao lilifunguliwa Julai na kufungwa September 2.

Lakini pamoja na usajili huo wa Ozil, wachambuzi wa mpira duniani wanasema kwamba Ozil ataisadia Arsenal, lakini klabu hiyo bado haijapata ufumbuzi wa matatizo yao makubwa ambapo ni kwenye ulinzi na ushambuliaji kidogo.

Arsenal pamoja na kushika nafasi ya nne kwenye ligi ni timu ambayo ilikuwa miongoni mwa vilabu vilivyokuwa vikiongoza kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kupitia viungo wake Aaron Ramsey, Rosicky, Santi Cazorla, Jacky Wilshare na mawinga kama Theo Walcott na Lukas Podolski. Tatizo kubwa la Arsenal katika misimu kadhaa iliyopita limekuwa kwenye nafasi ya kiungo cha kukaba na upande wa ukuta wao nyuma.

Lakini mpaka dirisha la usajili linafungwa timu hiyo haijasajili beki hata mmoja huku wakiwa na mabeki wao wale wale ambao kiukweli wamkeuwa wakiiangusha sana timu hii.

Ni sawa wamemsajili Ozil - lakini walikuwa na mahitaji makubwa kwenye nafasi ya kiungo cha ushambuliaji kama ilivyokuwa kwenye nafasi ya ulinzi kwa maana ya mabeki?

Ni namna gani Arsenal wataweza kumtumia vizuri Ozil ambaye ana sifa ya upishi wa mabao - ndani ya timu yao?

Je usajili wa Ozil uliogharimu fedha nyingi kuliko wowote katika Premier League msimu huu ni sahihi kwa mahitaji ya Arsenal?
***************TOA MAONI YAKO TUJADILI*************

   

16 comments:

  1. Mi naona ni sahihi kwa sababu wenger siyo muumini wa soka la kuzuia. So kupitia mpishi bora kabisa ulaya ataongeza idadi ya magori kitu ambacho kutayafunika yale ya kufungwa. So mi naona yuko sawa kabisa.

    ReplyDelete
  2. mechi 12 mfululizo bila kufungwa, bao 17 za Giroud geni wa Epl, mpira wa siku hizi hakuna viungo mkabaji ni holding midfilder ndo kila kitu.

    Mesut Ozil da new Denis Bergcamp /alivyokuwa anatumika Denis ndo atatumika huyu mchawi

    Arsenal hakuna ugonjwa wowote Ila wapika maneno wengi sana ulimwengun.

    ReplyDelete
  3. Wenger katufurahisha mashabiki duh Arsenal imekamilikaaaaa!!

    ReplyDelete
  4. Arsenal ni team ya pili kwa kufungwa maqgoli au kutokuruhusu magoli nyuma ya man city iloruhusu magoli 34 wakati arsenal imeruhusu 37............beki iko vizuri

    ReplyDelete
  5. wapenzi wa arsenal msisahau pamoja kuwa na attacking midfilders wa kutisha msisahau wamemsajili mchezaji ambae link iliyokosekana arsenal flamini . huyu jamaa ameongeza nguvu. tatizo la arsenal sasa ni mshmbuliaji mwenye uwezo mkubwa. wangempata suarez ingekua habari nyingine. maana hata mourino kawatolea nje ba dk za mwisho ili wakose straiker. sababu kaisha ona arsenal ni tishio.

    ReplyDelete
  6. ...Je mfumo wa Arsenal unategemea mshambuliaji mmoja?..ukiangalia starts za mwaka jana..Arsenal haikutegemea mtu mmoja kwenye ufungaji....Santi 12, Podoski 11, Walcot 11, Grioud 17...unweza ona hiyo distribution ya magoli. Inanikumbusha ile Arsenal ya akina Denis, Fredririck, Pires, Henry, Viera wakati wachezaji wa kiungo walikuwa wna contribute zaidi ya magoli 40 kwa msimu mmoja pekee...yes TH14 alikuwa na nafasi yake.
    ..Kujibu swali la msingi...Ozil atachangia sana kuongeza idadi ya magoli...hasa kwenye formation yetu ya 4-3-3 kwani tutakuwa tunahitaji striker mmoja tu kwa game...
    a) Je tuhahitaji beki?
    So far tuna mabeki wa 3 wazuri sana VM, Per, Konck, na woote wame improve sana recently.. wanatakiwa wacheze wa 2 tu kwa game..mie naona kwa idara hito tupo OK...na pia Sagna anaweza cheza hapo..when needed...sioni km pana shida sana!
    b) Giroud akiumia?..inaweza onekana ni tatizo, in fact, hata mie nilitegemea boss angesajili world class striker...lakini having misssed Suarez ...still naona tupo OK...Podoski anaweza cheza km striker....na tumemrudisha Betner in case tunamuhitaji though nakubali kabisa kuwa hana kiwango cha Arsenal kwa sasa..

    Perosnally, nimefurahishwa na usjali kwani kibiashara itaongeza mapato, ila pia inaongeza depth tatizo kubwa sana kwa Arsenal kwa muda mrefu

    ReplyDelete
  7. Nilidhani arsenal inatatizo la namba sita kiungo mkabaji, pia tatizo la striker ambaye atamfanya Theo Walcott kurudi kwenye nafasi yake kama winger. Lakini cha kushangaza Wenger sijui washauri wake wanafanya kazi gani maana timu inaumwa kichwa wao wanatibu kiuno!!

    ReplyDelete
  8. shafi acha porojo. nani alisema safi ya ulinzi ya arsenal ina matatizo. beki ya arsenal msimu uliopita ilikua ni ya pili kwa uimara ktk ligi. pamoja na kuumia diaby. ambae ni very strong player na uwezo wa hali juu. yuko flamini na arteta . kama uliangalia mechi ya spurs. nadhani kila mtu alimuona flamini s back. pia kuna the most improving player in epl. box 2box midfielder aaron ramsey. bila kusahau flamini ni kiraka. sagna kaonekana anauwezo mkubwa wa kucheza centerback. wataalam wa mpira wanasema anauwezo mkubwa wa kusoma mashambulizi. na kuzuia. usisahau thomas v karibu anakua fit

    ReplyDelete
  9. Maoni ya nini, arsenal ndo wameishasajili, maoni ya mtu yeyote hayawezi kubadili chochote, Wabongo tunapenda kujadili vitu ambavyo havina tija.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ubwege kilichokufanya U comment ni nini kama sio shobo,kama unaona haina tija ungechuna tu.

      Delete
  10. Arsenal ni timu imara na inayoelewana hata kabla ya ujio wa Ozil.Karibu kikosi chote cha mwaka jana kiko palepale.Kweli mashabiki wanahesabu makombe lakini tukubaliane kwamba kuwa kwenye top 4 kwa miaka 16 si mafanikio kidogo (Man united pekee wameweza hilo).Tatizo kubwa la Arsenal limekuwa ni(1) wembamba wa kikosi (2)kutopenda kununua nyota waliokwisha kamilika (isipokuwa Dennis Berkamp,labda na Sol campbell) (3)Kutoweza kurudia enzi za invicibles.(4) kutokuwa na wachezaji wabishi (combative) mfano wa Viera,Tony Adams na wengine.Angalia baada ya kupoteza kwa A.Villa,Arsenal wamerudi kwa nguvu zote.Ujio wa Flamini una maana kubwa hasa akiunganisha nguvu na Ramsey,na Wilshire.Hapo Arsenal watakuwa wamerudisha ubishi waiopoteza.Sitashangaa Arsenal kuchukua ubingwa.

    ReplyDelete
  11. MAJANGA YA KUTOKA KAPA KILA MSIMU YATAENDELEA: Timu haina Beki wa maana wa kupambana mechi 38 za ligi, UEFA, FA na Capital Cup.. Mabeki iliyo nao ni gari za mkaa tupu, Holding Midfilder ndo Kansa ya Gunners hapa wanajaribu kuitibu kwa Panadol wamemrudisha Mathieu Flamini na hana namba ya huakika ambaye kiwango chake kwa sasa hata Swanchea haanzi kikosi cha kwanza, Kwenye attaking ndo mmejaza wehu kibao akina Arteta, Diaby, Ramsey...., sekta hii wenye akili watakua Ozil na kidogooo Carzola, Foward ndo Jahu kabisaa eti Giroud ambaye hamuezi hata straika wangu wa mtaa Salehe Kisoki au hafiki hata nusu ya Samatta...??? Pamoja na kumsajili Ozil ila bado tatizo Wenger hajalitibu tutalajie yale yale ya misimu 8 iliyopita.. Kwa ushauri tu mashaki wa Gunners bora washabikie Orlando Pirates au Coastal mara 100 lakini sio Arsenal.. Wakati wao wanashika bunduki za kupamabana na Stoke City, wenzao wanatengeneza atomic za kuangamiza UEFA..

    ReplyDelete
    Replies
    1. unamaanisha epl imeshapangwa . yani kila timu ina nafasi yake. tunajua mnapata makombe kwa msaada wa marefa na fa. haujasikia hata fa wamefanya mabadiliko. kaa ww na ushamba wako. kwanza hata kuandika haujui. usituchafulie mpira .kacheze netball na madada wenzako. sisi tuna macho yetu na tunaona mpira. mchezaji akia na uwezo ana uwezo tu. hata hiyo tv unayoangalia wanaotoa matangazo wanasema kuhuusu sifa za mchezaji anaecheza vizuri. au huko unako kaa hakuna hata chanels za azam tv. pole

      Delete
  12. Ha ha haaaaa...Arsenal na matatizo yote waliyonayo safari hii wakiweza kubaki nafasi ya nne mpaka msimu unamalizika Wenger atakuwa kiumbe mwenye bahati zaidi Duniani. Ninachoamini ni kwamba amefanya usajili wa kisiasa ili kuwaziba midomo mashabiki. Wenyewe tunajikanganya humu maana mtu umeishasema Diaby yupo vizuri pale kati alafu ukiorodhesha matatizo ya Arsenal unasema hawana wachezaji wabishi (combative) hapo ni tayari umeishaelezea kwamba Diaby pamoja na uzuri wake na wenzie lakini ni maronyaronya.
    Wote tumeangalia sana ligi hii ngumu lakini timu bila ya wachezaji wabishi wapambanaji likes of Dennis Wise, Roy Keane, Patrick Viera, Lamps na SG ni ngumu kuchukua ubingwa sababu pale kati hakuchezi mpira tu. Ni uwanja wa vita!
    Na ukiwa mwepesi mtu kama Joy Barton hana mpira kihivyo lakini atakusumbua.

    Kila lakheri Arsenal lakini nusu ya msimu wa kwanza majibu mtakuwa nayo tayari sababu mimi binafsi siamini kama Ozil ndio mtatuzi wa matatizo yenu.

    Wasalaam.

    ReplyDelete
  13. .in my view
    ..let me clarify why Ozil is very important to arsenal depth!
    Kumbukeni Santi alikua anacheza as a creative midfielder to supply assists to the attacking players,but ukweli ni kwamba we never used the left flank that much.tumemtumia walcot zaidi kulia..podolski has not been that active at left ukiachia recent perfomance..that means podolski is the main striker,he will be changed to a cf na amekubali.Giroud,podolski,bendtner and sanogo..mainly podolski and giroud.so cazorla atahama to the left,his most effective position,ozil covering central but attacking midfielder and rosicky as the sub,infront of arteta and ramsey,leaving ramsey to do what he can do(box to box) diaby as the sub while arteta playing deep wilshere as the sub...what i can see on december,is wenger going for a striker and a center back...but Gooners,dont ever complain about the midfield.
    Squad!
    1.szczesny
    2.bacary
    3.gibbs
    4.mertesacker
    5.koscielny
    6.arteta
    7.walcot
    8.ramsey
    9.giroud
    10.ozil
    11.cazorla

    subs
    1.fabianski
    2.jenkinson
    3.monreal
    4.vermaelen
    5.wilshere
    6.diaby
    7.chamberlain
    8.rosicky
    9.podolski

    SO ATLAST WE HAVE GAME CHANGERS KWA BENCH..!THATS MY POINT

    ReplyDelete
  14. ndugu yangu wilshere hawezi kukaa benchi ni mchezaji bora kuliko arteta na ramsey

    ReplyDelete