Search This Blog

Tuesday, September 10, 2013

MAKALA: NI KWENYE NAFASI GANI MAROUNE FELLAINI ATAFITI NA KUINUFAISHA ZAIDI MANCHESTER UNITED?


fellaini

Manchester United hawakuwa na vurugu kubwa kwenye soko la usajili lilofungwa hivi karibuni. David Moyes alijaribu kuwasajili wachezaji kadhaa wakiwemo Cesc Fabregas na Thiago Alcantara, lakini mpaka siku y mwisho ya dirisha la usajili, mashabiki wengi wa United waliachwa wakiwa na huzuni baada ya klabu yao kusajili mchezaji mmoja tu kutoka Everton Marouane Fellaini kwa ada ya uhamisho ya £27 million. United imekuwa na matatizo yanayofahamika kwenye safu ya kiungo kwa muda sasa, lakini ni wapi hasa Fellaini katika kikosi cha Moyes?

Ni wapi Moyes alimtumia vizuri zaidi Fellaini walipokuwa Everton?
Msimu uliopita mechi 28 kati ya 31 alizoanza Fellaini alicheza kama mshambuliaji wa pili au kama kiungo mshambuliaji huku mechi nyingine 3 akicheza kama kiungo mkabaji akicheza eneo la chini ya uwanja zaidi.  Tunachoweza kupata kutoka kwenye takwimu hizi ni kwamba, wakiwa Everton, Moyes alimuona Fellaini kama mchezaji wa kucheza mbele zaidi kuliko nyuma kwa maana ya kiungo mlinda ukuta wa nyuma. Everton walionekana mara nyingi wakitumia mipira mirefu iliyokuwa ikielekezwa kwa Fellaini aliyekuwa akisimama eneo la ndani ya au nje kidogo ya lango. Aidha apige shuti au kujaribu kumchezesha mchezaji mwingine.

Katika kufanya hivi Fellaini alikuwa akiisadia timu - alifunga mabao 11 na kutoa assists 5. Kwa kifupi alikuwa na msaada zaidi kwa kuwapa taabu sana mabeki na magolikipa kwa staili yake ya uchezaji.
Picha ya chini inaonyesha maeneo ambayo Fellaini alicheza kwenye ushindi wa 3-0 wa Everton dhidi ya Reading,  ambapo alichezeshwa kwenye kama mshambuliaji wa pili nyuma kidogo ya  Nikica Jelavic, mechi ambayo Fellaini alifunga:

fel

Fellaini alitumia muda mwingi katika tatu ya mwisho ya uwanja, akitumia muda mchache sana katika maeneo ya ulinzi. Pamoja na kuwa 18.70% ya mchezo wake kuwa katika eneo la kati Fellaini alifanya tackling moja tu lakini hii ilitokana kwamba alikuwa na jukumu la kucheza kwa kushambulia zaidi ya nyuma ya Jelavic. Jukumu lake alilopewa kucheza mbele alilitendea haki baada ya kucheza mipira 11 kati ya 16 ya juu.

Fellaini kama kiungo mkabaji. 


Huku Shinji Kagawa, Wayne Rooney na Danny Welbeck wote wana uwezo wa kucheza kama washambuliaji wa pili/viungo wa kushambulia katika set up ya kikosi cha United na kwa maana hiyo inaonekana Moyes hatomtumia Fellaini mbele. Hivyo atamtumia kwa pamoja na Micheal Carrick katika kiungo cha kukaba.

Msimu huu Roberto Marinez aliona ni vyema kumtumia Fellaini kama kiungo mkabaji. Fellaini alicheza nyuma na alionekana kufurahia kucheza nafasi hiyo kuliko msimu uliopita, akiwa na wastani 73.3 kwa mchezo akiwa na usahihi wa 89% ( msimu uliopita alikuwa na wastani wa pasi 52.3 kwa mchezo na usahihi wa 79% ). Dhidi ya Cardiff alicheza vizuri akipiga pasi 66 passes:

fella2

Fellaini alikuwa na usahihi wa kupiga pasi kwa 91% na kwa kuwa alicheza cha kukaba nusu ya pasi zake zilikuwa kwenye nusu ya uwanja ya goli la Everton. Kwa maana inaonekana Martinez ameweka msisitizo kwenye kumiliki zaidi mpira, lakini pia hii inaonyesha kwamba Fellaini anaweza kucheza vizuri kiungo cha kukaba akiwa atahitajika kufanya hivyo.

Fellaini pia ameweza kucheza vizuri sana kwenye kukaba, jambo ambalo ndio udhaifu wa United. Mbelgiji huyu alikuwa na wastani wa kufanya tackling kwa  4.3 kwa mchezo (hii ni zaidi ya Carrick na Tom Cleverley) akiwa na usahihi wa 85%:
fella
Sio tu kwamba tunaweza kuona namna alivyo imara kwenye mipira ya juu 0 jambo ambalo litaisadia kupambana na mipira iliyokufa kwenye eneo lao la penati. Lakini pia Fellaini ana udhaifu wa kucheza sana rafu. Alipochezeshwa kama kiungo mkabaji msimu uliopita alicheza faulo kwa wastani wa 2.6 kwa mchezo, huu ni wastani mkubwa kuliko mchezaji yoyote katika premier league msimu uliopita. Hili inabidi lifanyiwe kazi katika kuepuka kutoa faulo za ajabu ajabu ambazo huleta madhara langoni.

HITIMISHOWakati Fellaini anaweza kutumika kama mshambuliaji wa pili/kiungo wa kushambulia, inaonekana wazi hatotumika namna hii ndani ya Manchester United. Anaweza kutumika kama ‘Plan B’ kwa kutumia mipira mirefu katika mechi ngumu. Lakini pia atakuwa anagombea namba na Tom Cleverley kucheza pamoja na  Michael Carrick. Fellaini sio mchezaji mwenye kasi lakini ni mzuri katika kuzuia na kupora mipira. Wasiwasi utakuwa kwenye udhaifu wake wa kucheza sana rafu, ikiwa anataka kufanikiwa sana akiwa na United itabidi ajitahidi kuepeukana na mchezo huu. Ikiwa ataendelea kutawala safu ya kiungo, akipora sana mipira na kuendelea na rekodi yake nzuri ya utoaji wa pasi, then kutakuwa hakuna sababu kwanini asing'are akiwa na jezi nyekundu ya United.

2 comments:

  1. tumechoka na huo umanchester wenu

    ReplyDelete
  2. that is gud but itakuwa gud kama mzee atamtumia ktk 4 2 3 1

    ReplyDelete