Wanamichezo
wawili walioomba kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu wamewekewa
pingamizi.
Waliopingwa
ni Wallace John Karia anayeomba kupitishwa kuwania urais na Vedastus
Kalwizira Lufano anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda
Namba Mbili ambayo ni mikoa ya Mara na Mwanza. Anyempinga Karia ni
Shamsi Rashid Kazumari wa Dar es Salaam wakati Lufano anapingwa wa
Samwel Nyalla wa Mwanza.
Pamoja
na mambo mengine, Kazumari anampinga Karia kwa madai kuwa akiwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, aliwashawishi wajumbe wenzake kuingia
mkataba na Azam Tv wakati akijua kamati hiyo ni ya muda, hivyo haina
nguvu za kisheria kusaini mkataba huo.
Naye
Nyalla ambaye pia ni mmoja wa wanamichezo waliojitokeza kuwania ujumbe
kupitia Kanda hiyo anampinga Lufano kwa madai hana uzoefu wa miaka
mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbezeleni itakutana
kesho (Agosti 28 mwaka huu) saa 4 kamili asubuhi kusikiliza pingamizi
hizo ambapo wawekaji pingamizi na waliopingwa wanatakiwa kufika wenyewe
ndani ya muda kwa vile uwakilishi hautakiwi.
MAANDALIZI MKUTANO WA UCHAGUZI TFF
Sekretarieti
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inaendelea na maandalizi
ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 26 na 27 mwaka huu
jijini Dar es Salaam.
Awali
mkutano wa uchaguzi ulikuwa ufanyike Februari 23 na 24 mwaka huu lakini
tukauahirisha kusubiri maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA), hivyo tayari wajumbe wana taarifa rasmi kuhusu mkutano
huo.
Orodha
ya wajumbe iliyotumwa awali kwa ajili ya Mkutano tunayo, isipokuwa kama
kuna wanachama wetu wana mabadiliko ya majina ya wajumbe
watakaohudhuria wanatakiwa kutuma majina hayo kabla ya Septemba 30 mwaka
huu.
Wanachama wa TFF ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu 14 za Ligi Kuu ya Vodacom.
Pingamizi la kusema mkataba ina maana walitaka hivyo vilabu vipate wapi fedha za ziada za maandalizi?au ndio kutaka kuswe na ushindani wa kutosha kwenye ligi kuu yetu ya Vodacom?Wanasema wameharakisha je ni kampuni gani ya media imeenda kuomba kuonyesha ligi kwa dau walau hata hilo la Azam media ltd wanaosema yenye uzoefu wakakataliwa tatizo letu tunapenda kuongea sana kuliko utendaji,sasa kamati imethubutu na kupata mkataba unaosaidia timu zilizokuwa zinasadiwa na Vodacom peke yake mnaenda kuweka mapingamizi kabla ya kufanya kitu jamani tufikirie kwanza
ReplyDelete