Search This Blog

Friday, August 23, 2013

TATIZO LA MAN UNITED KUTOFANYA USAJILI MPAKA SASA: MSAIDIZI WA FERGIE ASEMA TATIZO NI CEO MPYA WA KLABU KUTOJUA VIZURI NAMNA YA KUDILI NA MASUALA YA USAJILI

Kocha msaidizi wa zamani wa Manchester United Mike Phelan anaamini CEO mpya wa klabu hiyo Ed Woodward yupo katika wakati mgumu wa kudili na masuala ya usajili kwa sababu hana uzoefu huo. 

Phelan ambaye aliondoka United mara baada ya Ferguson kustaafu mapema wakati kiangazi kilichopit, akiongea na BBC Radio Manchester, Phelan alisema: "Nadhani ili ofa iliyotumwa kwenda Everton haikuwa sawa. Sikudhani kama hata wangeifikiria.
"Ed Woodward huko nyuma alikuwa akifanya kazi za kibiashara zaidi na kuweka umakini katika kuingiza fedha ndani ya klabu na sio kutumia fedha za klabu. Anchofanya sasa ni kitu tofauti na alichozoea. Lakini atajifunza kadri muda unavyozidi kwenda. 

"Anajaribu kubana matumizi lakini itabidi atumie fedha kwa sababu klabu inataka kusajili wachezaji bora.

"Ed pamoja na klabu wamezungumza na kusema fedha za kutumia zipo. Hilo ni jambo zuri lakini soko la usajili linakaribia kufungwa na mpaka sasa hawajafanya biashara."

Maoni ya Phelan kwamba Ed Woodward ni mzuri zaidi katika kuingiza hela ndani ya klabu kuliko kutumia yanapewa nguvu na namba ya makampuni yaliyoingia mikataba na United katika siku za hivi karibuni baada ya Ed kuchukua madaraka kutoka kwa David Gill.

No comments:

Post a Comment