Hatma ya Cristiano Ronaldo ndani ya Real Madrid imezidi kuleta mkanganyiko baada ya mshambuliaji huyo kugoma kuthibitisha taarifa kwamba amekubali kusaini mkataba mpya wa miaka mitano.
Ronaldo bado ana miaka miwili kwenye mkataba wake, lakini hivi karibuni amekuwa akihusishwa na kutaka kurejea kuitumikia klabu yake ya Manchester United.
Ronaldo alikaririwa akisema: "Sitothibitisha kitu chochote - nitaendelea tu kufanya kazi ambayo naifanya kila siku.
"Hatma yangu ndani ya Madrid - Sijui itakuwaje. Kwa muda huu mie bado ni mchezaji wa Real, kuhusu kitachotokea huko mbele sifahamu kwa kweli.
"Ngoja tusubiri tuone nini kitatokea - lakini kwa sasa nipo sawa na mahala nilipo."
Ronaldo apia alizungumzia Gareth Bale na tetesi za usajili wake kwenda Real.
Madrid wanaaminika wapo tayari kulipa kiasi cha £95m ili kumpata Gareth Bale lakini Ronaldo aliongeza: "Sitotaka kulizungumzia suala hilo kwasababu mimi sio mtu sahihi kusema kama anastahili kununuliwa kwa fedha hizo au la - au ni dili nzuri au hapana. Sitotaka kuzungumzia kuhusu wachezaji wengine."
No comments:
Post a Comment