Search This Blog

Monday, August 5, 2013

MANCHESTER UNITED YATHIBITISHA KUKATAA OFA MPYA YA CHELSEA KWA WAYNE ROONEY

Manchester United wamethibitisha kwamba wamekataa ofa ya pili ya Chelsea kwa ajili ya kumsaini mshambuliaji wao Wayne Rooney.
Jose Mourinho tayari alishaona ofa yake ya kwanza inayokadiriwa kuwa £20m kwa jili ya mshambuliaji huyo wa England  ikikataliwa lakini pia ofa yake mpya inayokadiriwa kuwa £30m nayo imepigwa chini.
Mourinho alikiri mwezi uliopita kwamba Rooney ndio chaguo lake pekee la usajili lilobaki, wakati mchezaji husika akiripotiwa kuwa tayari kulazamisha kuuzwa kwa kuandika ombi la kuuzwa rasmi.  

Boss United David Moyes ameshasema mara kwa mara kwamba mshambuliaji wake mwenye miaka 27 hauzwi na msemaji rasmi wa klabu hiyo amezungumza tena leo asubuhi. 

"Jana tulipokea ofa kutoka kwa helsea, na kwa haraka ilikataliwa," alisema msemaji huyo wa United. "Msimamo wetu bado haujabadilika kwamba Rooney hauzwi."
Rooney, ambaye bado ana miaka miwili iliyobaki kwenye mkataba wake, anategemewa kusafiri na timu mpaka Sweden leo jioni, kuelekea mchezo wa kirafiki dhidi ya AIK jijini Stockholm kesho jumanne.
Moyes ameripotiwa kumuudhi sana Rooney wakati aliporipotiwa akisema kwamba Rooney atakuwa back up ya Van Persie ikiwa mshambuliaji huyo aliyehamia kutoka Arsenal angepata majeruhi.

Graeme Souness anaamini Manchester United wamejiweka kwenye sehemu mbaya na namna wanavyoshughulikia suala hilo, lakini kamwe hawatomuuza kwa klabu ya England. 

Alisema: "Maneno ya Moyes yamemfanya Rooney akasirike sana. Kuambiwa kwamba atakuwa chaguo la pili baada ya Van Persie kumeumiza hisia zake.
"Manchester United wamejiweka kwenye nafasi mbaya kwenye suala hili, lakini sidhani kama watamuuza kwa klabu ya Premier League."

No comments:

Post a Comment