Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi
kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji
wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The
Cranes) itakayofanyika Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Waamuzi
hao ni Thierry Nkurunziza atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake
watakuwa Jean Claude Birumushahu na Pascal Ndimunzigo. Mwamuzi wa akiba
(fourth official) ni pacifique Ndabihawenimana.
Kamishna
wa mechi hiyo Gebreyesus Tesfaye kutoka Eritrea. Tesfaye pia ni
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Eritrea na mjumbe wa Kamati
ya Maandalizi ya Mashindano ya CHAN.
FAINALI AIR RISING STARS ‘LIVE’ SUPERPORT
Fainali
za michuano ya Airtel Rising Stars kwa wavulana na wasichana
zinazochezwa kesho (Julai 6 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
Dar es Salaam zitaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha
SuperSport.
Mechi
za fainali ambazo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Amos Makala zitachezwa kuanzia saa 7.30 mchana kwa
wasichana wakati ile ya wavulana itaanza saa 9.30 alasiri.
Nusu
fainali za mashindano hayo ambazo pia zinaonekana moja kwa moja
SuperSport zinachezwa leo (Julai 5 mwaka huu). Kwa upande wa wasichana
ni kati ya timu za Kinondoni na Kigoma wakati Ilala inaumana na Temeke.
Kwa
upande wa wavulana nusu fainali ya kwanza ni kati ya Mwanza na Ilala
ambapo baadaye itafuatiwa na nyingine kati ya Morogoro na Kinondoni.
Mechi za kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa kesho asubuhi (Julai 6
mwaka huu).
28 KUSHIRIKI KOZI YA FIFA 11 FOR HEALTH
Jumla
ya makocha wa mpira wa miguu na walimu 28 kutoka Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) na shule za msingi na sekondari wameteuliwa
kuhudhuria kozi ya FIFA 11 For Health inayoanza keshokutwa (Julai 7
mwaka huu) Homboro mkoani Dodoma.
Kozi
hiyo itakayomalizika Julai 20 mwaka huu itakuwa chini ya ukufunzi wa
Rogasian Kaijage ambaye pia ni Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake
(Twiga Stars).
Washiriki
ni Abdul Mikoroti (Shule ya Msingi Nzasa), Baltazar Kagimbo (Shule ya
Msingi Tabata Jica), Baraka Baltazar (Shule ya Msingi Muhimbili), David
Kivinge (Shule ya Msingi Temeke), Dismas Haonga (Tambaza Sekondari),
Exuperus Kisaka (Shule ya Msingi Mavurunza) na Hadija Kambi (Shule ya
Msingi Karume).
Hamis
Chimgege (Shule ya Msingi Tusiime), Hobokela Kajigili (Shule ya Msingi
Buguruni), Issack Mhanza (Shule ya Msingi Airwing), Job Ndugusa (Shule
ya Msingi Upanga), John Sebabili (TFF), Lutta Rucharaba (Shule ya Msingi
Montfort), Maua Rahidi (Shule ya Msingi Uhuru Wasichana), Michael
Bundala (TFF) na Mussa Kapama (Shule ya Msingi Bunju ‘A’).
Priscus
Silayo (Shule ya Msingi J.K. Nyerere), Peter Manyika (TFF), Rajabu
Asserd (Shule ya Msingi Mtoni Kijichi), Raphael Matola (TFF), Raymond
Rupia (St. Anne Maria Academy), Renatus Magolanga (Ulongoni Sekondari),
Ruth Mahenge (Shule ya Msingi Chang’ombe), Said Pambaleo (TFF),
Sebastian Nkoma (TFF), Titus Michael (TFF), Wane Mkisi (Jangwani
Sekondari),
LIUNDA KUSIMAMIA MECHI YA CHAN
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa
Kamishna wa mechi kati ya Burundi na Sudan itakayochezwa jijini
Bujumbura.
Mechi
hiyo ya kwanza ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za
Ndani (CHAN) itafanyika keshokutwa (Julai 7 mwaka huu). Liunda
anatarajia kuondoka leo usiku (Julai 5 mwaka huu) kwenda Bujumbura..
No comments:
Post a Comment