Search This Blog

Tuesday, July 2, 2013

OFFICIAL: FC TWENTE YAMKANA RASMI SHOMARI KAPOMBE.

                                                      RICHARD PETERS

KLABU ya FC Twente ya Uholanzi usiku huu imemkana rasmi mchezaji wa Simba na Taifa Stars, Shomari Kapombe ambaye alitangazwa kuwa na mipango ya kujiunga na kalbu hiyo.

Kwa muda wa wiki mbili sasa, vyombo mbalimbali vya habari vya Tanzania viliripoti taarifa za Kapombe kutakiwa na klabu hiyo ya Uholanzi ambayo ambayo ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uholanzi katika msimu wa 2009-10, pia ilifanikiwa kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika msimu huo.

Afisa Habari wa FC Twente, Richard Peters amekiambia kipindi cha michezo cha redio Clouds FM usiku huu kwamba, klabu yaje haijawahi kumuhitaji mchezaji huyo na hana taarifa zozote kuhusu Kapombe.

“Kwa sasa hatuhitaji mchezaji yeyote kutoka Afrika na hata kama ingekuwa hivyo ingefahamika. Nasisitiza hatuna mpango na mchezaji huyo,” amenukuliwa Peters akikataa kumtambua Kapombe.

Kwa upande wa viongozi wa Simba mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Swed Nkwabi alikaririwa na gazeti la Mwananchi hivi karibuni akisema kwamba, “Timu atakayokwenda kufanya majaribio Kapombe huko nchini Uholanzi ni FC Twente, suala la ataondoka lini kwenda kufanya majaribio tutawaambia safari itakapokuwa tayari.”

Na kwa upande wa mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alikaririwa akizungumza kwenye kipindi cha michezo cha redio moja hapa jijini, akisema kwamba amekwishatoa kibali kwa Kapombe kuondoka nchini siku yoyote kuanzia sasa kwa ajili ya kufanya majaribio nchini Uholanzi.

Lakini baada ya kuwepo kwa taarifa hizi mtandao huu ulijaribu kufanya utafiti kidogo kuhusu suala la usajili wa mchezaji huyu kwenda FC Twente na kugundua vitu kadhaa vya utata kuhusu ukweli wa taarifa za Kapombe kutakiwa na klabu hiyo ya Uholanzi.

Miongoni mwa vitu vya kushangaza ni mtandao uliotangazwa kuandika habari hizo pia majibu ya wakala wa mchezaji huyo aitwaye Denis Kadito ambaye alithibitisha ni ukweli kwamba alikuwa katika mpango wa kumpeleka Kapombe Uholanzi ili aanze kumtafutia timu ndani ya bara la ulaya, na alipoulizwa kuhusu taarifa za Kapombe kutakiwa na FC Twente, Dennis alisema hana taarifa zozote za Kapombe kutakiwa na FC Twente hivyo hawezi kutoa maoni yoyote kuhusu suala hilo.

6 comments:

  1. Mbona waibania comment yangu? Mpango mzima ni wazee wa sembe walitaka mtumia!!

    ReplyDelete
  2. Waliosema Shafii/mtoa mada wa juzi kuwa anawivu waje waseme hapa sasa.....soka la tanzania halitaenedelea kwa kuendekeza unazi....mkutano mkuu wa simba unakaribia mnadahni viongozi watatafuta sympathy ipi toka kwa wanachama...?

    Wagosi wanasema "Kalagabaho"

    Muulizeni Rage hela ya Okwi iko wapi na FIFA wamesema nini....?

    Uwanja wa Bunju umeishia wapi.....?

    Na ule uwanja walioitiwa na mdau kule Kigamboni yeye na kaburu wameufanya nini...?

    ReplyDelete
  3. Hivi viongozi wa simba wanaeleza umma kwa habari ambayo siyo rasmi? kwa kufikirika au kuangalia mtandao ili wapate sifa kuwa klabu yao inauza wachezaji? duh kweli hatuna viongozi

    ReplyDelete
  4. http://googlehabari.blogspot.com/2013/07/shaffih-dauda-apingana-na-supersport.html

    ReplyDelete
  5. hayo n maneno yako wewe kiukwel supersport imeconfirm na pia footytube.com na hata account yao ya twitter ila wewe unapinga bila ushahidi

    ReplyDelete
  6. Anaondoka leo na timu atakazofanyiwa majaribio ni fc twente na nyinginezo.

    ReplyDelete