Ilikuwa ndio mara ya kwanza wanakutana tangu walipocheza kwenye nusu fainali ya ligi ya mbingwa ya ulaya, ambapo Bayern waliidhalilisha FC Barcelona kwa kuifunga 7-0.
Na kama ilikuwa haitoshi hamu ya mchezo huo ilizidi kuongezeka kwa sababu ilikuwa ndio mechi ya kwanza ambayo Pep Guardiola amekutana na timu yake ya zamani. Kocha huyo alidumu Camp Nou kwa miaka minne na kushinda makombe 14.
Thiago Alcantara pia alicheza kwenye mchezo huo dhidi ya timu yake ya zamani kwa mara ya kwanza, siku chache baada ya kununuliwa kwa ada ya uhamisho wa 21.6 million switch to Bayern earlier this month.
Barca, ambao wiki hii walimtangaza Gerardo Martino kuwa kocha wao mpya, walicheza bila kocha mpya na jahazi na kocha msaidizi Jordi Roura na Rubi.
Mchezo ndio ulikuwa wa kwanza kwa Barca kucheza kwenye pre season na kwa Bayern ulikuwa wa saba - hii ni katika kuweka sawa miili ya wachezaji tayari kwa mapambano msimu unaofuatia.
Japokuwa mchezo huo ulikuwa wa kirafiki - lakini kuna vitu muhimu ambavyo tumejifunza kupitia mechi hiyo.
MBINU ZA PEP GUARDIOLA
Pep Guardiola tayari anaonekana kuanza kiurahisi maisha yake ndani ya Allianz Arena.
Jupp Heynckes alishinda makombe matatu msimu uliopita na kuacha vitu vikubwa kuvivaa, lakini Guardiola, anajiamini kwa uwezo alionao, na amekuwa sio muoga wa staili mpya ya kuiongoza klabu yake.
Akiwa tayari ameshajaribu mifumo ya 4-1-4-1 na 4-3-3 katika pre season, Guardiola anaongeza kitu cha ziada katika kikosi cha Bayern.
Tayari ameshamhamisha nafasi Philipp Lahm, ambaye huko mwanzoni alikuwa anacheza beki wa kulia.
Guardiola amemhamisha nahodha huyo na kumsogeza mbele kidogo, akicheza upande wa kulia mwa Thiago Alcantara katika kiungo, huku Rafinha akicheza kwenye nafasi ya beki wa kulia.
Lahm anaonekana kucheza vizuri kwenye nafasi yake mpya. Alifunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 14 na pia alifunga katika ushindi wa mabao 5-1 kwenye michuano ya Telekom Cup dhidi ya Borussia Monchengladbach jumapili iliyopita.
Kwanini amlete Lahm katika kiungo ambacho tayari kina wachezaji wengi wazuri ambao wanaleta ugumu katika kuwapanga? Guardiola anapenda kufanya majaribio.
Anaweza akawa anatengeneza safu ya kiungo ambayo inaweza kufanya kila kitu - kuzuia, kushambulia, kupiga pasi.
Bayern walicheza mechi sita kabla ya kucheza na Barca na walifunga mabao 35. Kama ni ishara ya kuonyesha namna mambo yatakvyokuwa huko mbele basi majaribio ya mbinu mpya za Guardiola yatakuwa mazuri sana....
LA MASIA BADO IPO IMARA SANA
Ni jambo ambalo linafahamika vyema kwamba La Masia ndio academy inayoongoza kwa kutoa vipaji vingi vya wachezaji wakubwa waliopo kwenye soka hivi sasa - ambao wana uwezo wa kuingia kwenye vikosi vya timu nyingi kubwa barani ulaya.
Barca walicheza mechi ya jana bila wachezaji wengi wa kikosi cha kwanz, Xavi, Andres Iniesta, Cesc Fabregas, Sergio Busquets, Gerard Pique, Dani Alves na Neymar wote wakiwa bado wapo mapumzikoni baada ya kutoka kushiriki michuano ya kombe la mabara huku Carles Puyol akiwa bado majeruhi, wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza walikuwa hawapo.
La Blaugrana walianza mchezo huo golini akiwa Pinto, huku Martin Montoya, Marc Bartra, Javier Mascherano na Adriano Correia wakiunfa safu ya ulinzi. Alex Song alicheza kiungo cha kati, huku Jonathan dos Santos akicheza kulia na Sergi Roberto akicheza kushoto. Alexis Sanchez, Lionel Messi na Cristian Tello waliunda safu ya ushambuliaji.
Kipindi cha kwanza chote kilitawalia na Bayern Munich na mpaka wanakwenda mapumziko walikuwa mbele kwa 1-0. Mascherano na Bartra walijipatia kadi za njano kwa kumchezea faulo Franck Ribery.
Kipindi cha pili ndipo angalau Barcelona walionekana kutulia na kusogeza timu mbele na kufanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi. Aliingia kipa wa Barca B Oier Olazabal na hivyo kuongeza idadi ya wachezaji wachanga ndani ya kikosi hicho na bahati mbaya wakaongezwa bao la pili lakini kwa kuangalia kwa jicho la tatu inaonekana hatma ya FC Barcelona huko mbele ni nzuri sana kwa vipaji walivyonavyo wachezaji wake wachanga.
THIAGO ALCANTARA
Thiago Alcantara ameanza kuzoea mfumo wa FC Bayern Munich bila tatizo tena kwa haraka.
Katika mchezo wake wa tatu wa pre season akiitumikia Bayern, alionekana kutulia na mwenye furaha. Kiungo huyo tayari ameshafunga bao la kwanza akiwa na timu yake mpya.
Katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Borussia Monchengladbach, alifunga bao lake akitumia kifua chake.
Katika safu ya kiungo ambayo tayari ina watu wenye vipaji kama Mario Gotze, Bastian Schweinsteiger, Toni Kroos, Arjen Robben, Franck Ribery na Javi Martinez, miongoni mwa hao, ilionekana wazi anaweza akapata shida kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza. .
Lakini kama kiwango alichoonyesha kwenye pre season kitaendelea kuimarika, then atakuwa amejihakikishia nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Guardiola.
FRANK RIBERRY NDIO MCHEZAJI BORA BARANI ULAYA?
Ribery—won the treble with Bayern Munich last season.Alex Grimm/Getty Images
Kiwango cha Franck Ribery dhidi ya Barcelona kilinikumbusha ubora wa mchezaji huyu.
Ingawa alikuwa anacheza na kikosi dhaifu cha Barca, lakini alicheza vizuri sana.
Dhidi ya Barca, krosi yake ilipelekea goli la kwanza lilofungwa kwa kichwa na Lahm. Ribery alicheza vizuri sana na kuwasumbua sana mabeki wa Barca kiasi cha kuwafanya Mascherano na Bartra kupewa kadi za njano wakijaribu kumsimamisha mfaransa huyo. .
Baada ya kushinda makombe matatu msimu uliopita, huu ndio muda muafaka wa Ribery kuwaashinda Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika tuzo ya uchezaji bora wa ulaya.
No comments:
Post a Comment