Kiungo wa Bayern Munich Thiago Alcantara amesema kwamba ssio kweli kwamba alikataa kujiunga na Manchester United kama ilivyokuwa ikiripotiwa bali klabu hiyo ya England haikuwahi kumtaka hata siku moja.
Thiago alihusishwa sana kutakiwa na United kwenye dirisha hili la usajili kabla ya kuamua kujiunga na mabingwa wa ulaya mapema mwezi huu.
Jana jumatano, baba yake Thiago, Mazinho aliiambia La Xarxa kwamba mtoto wake alikuwa anakaribia kwenda Old Trafford, lakini Thiago mwenyewe leo amekanusha taarifa hizo.
"Ukweli ni kwamba hakuna muda wowote ambao Manchester United walikuja kuongea na sisi. Mambo yote yalikuwa yakiandikwa na vyombo vya habari, ulikuwa niuongo dhahiri," aliiambia radio RAC1.
Akizungumzia uamuzi wake wa kuondoka Barcelona, alisema: "Sio sahihi kusema kwamba sikuwa mvumilivu. Klabu ilielewa hali yangu. Niliwasubiria wao, lakini hawakuwa wanawasiliana nami. Sikuhisi kwamba nina thamani kwao.
"Nilitaka kushindana. Klabu ilitambua kwamba nataka kuondoka na hawakufanya lolote kubadilisha hilo.
"Kila mtu anaangalia maslahi yake, nilitaka kuona nathaminiwa na nilitaka kushindana hivyo niliamua kuondoka na kujiunga na Bayern.
"Niliwasubiri sana kipindi chote cha kiangazi na mwishowe nikaamua kufanya uamuzi mgumu.
"Anachokitaka kila mwanasoka ni kucheza soka na nilitaka kucheza, wao [Barcelona] hawakufanya chochote kunihakikishia hilo, hivyo ndio maana sasa nipo hapa."
No comments:
Post a Comment