Search This Blog

Wednesday, July 3, 2013

KOCHA WA ZAMANI YANGA APEWA KAZI YA KUIPELEKA MALAWI KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Malawi wamempa aliyekuwa kocha wa Yanga Tom Saintfeit kazi kwenye benchi la ufundi, baada ya kukubaliana kwa mkataba wa mkataba wa miaka mwili na Mbelgiji huyo. 

Saintfeit alitimuliwa kwenye klabu ya Yanga muda mfupi baada ya kuipa klabu hiyo ubingwa wa Kagame alisema: "Lengo ni ni kujaribu kuisadia Malawi kufuzu kwenda kwenye World Cup 2014 nchini Brazil. Nitafanya kazi na timu nzuri ya makocha wa ndani." 

Malawi watacheza mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya  Nigeria tarehe 6 September, wakijua kwamba ushindi utawpa nafasi ya kwenda kucheza hatua ya mtoano.
Super Eagles wanaongoza kundi wakiwa na pointi tisa, 2 mbele ya Malawi.
"Naijua Nigeria na naijua Malawi, nina imani kubwa kwamba Malawi ina uwezo wa kufuzu," aaliongeza Saintfeit, ambaye ataenda Malawi siku ya Alhamisi kwenda kuona mchezo wa kirafiki na Msumbiji mnamo tarehe 6.

No comments:

Post a Comment