Search This Blog

Sunday, June 16, 2013

MJADALA: UNADHANI NINI KIFANYIKE KATIKA KUIBORESHA TAIFA STARS KUFANYA VIZURI MICHUANO YA KIMATAIFA???


Toa maoni yako kuhusu nini kifanyike katika kuiboresha timu ya Taifa ili iweze kufanya vizuri kwenye michuano ijayo ya kimataifa. Nini kifanyike tuweze kufuzu AFCON 2015 na Kombe La Dunia mwaka 2018???

22 comments:

  1. Tuimarishe ligi ya ndani ili timu zetu zinapoenda kwenye mashindano ya kimataifa ziwe bora ili tuweze kuuza wachezaji nje hasa ulaya wakapate uzoefu kisha warudi kuja kuisaidia timu yao, mfano tumeona kwa akina YAYA na SAMATA.Pia lingi za vijana under 18 ziimarishwe na timu za vijana za vilabu ziimarishwe ili zizalishe wachezaji wazawa kama SIMBA na AZAM badala ya kununua nje kama wafanyavyo YANGA

    ReplyDelete
  2. iundwe timu yetu ya taifa B chini ya makocha wazawa wachezaji wadogo wadogo tu halafu wacheze michezo ya kirafiki ya kimataifa ,wazawa ni umuhimu sana.

    ReplyDelete
  3. MECHI YA MWISHO NA GAMBIA IENDE TIMU YA SERENGETI BOYS WAKICHANGANYWA NA BARTEZ.....DOMAYO ETC TUWAPUMZISHE..KASEJA....KANAVARO..A. MORIS...YANI WALE TUNAWAONA WAKONGWE.....!!

    ReplyDelete
  4. Benchi la ufundi lifumuliwe kocha aendelee kim poulsen. Marsh .kibaden.boniface.pondamali.adolf.nsajigwa.nizar (huu ni mfano nikimaanisha timu izungukwe na watu waliocheza au kuwa karibu na mpira wetu kwa muda mrefu) wapo wachezaji tunaowaona kila siku kutokana na ligi yetu inayochezwa kila msimu lkn wapo wachezaji tusiowaona wapo hapa nchini kwetu wanafichika kutokana tu. Na aina ya mashindano tulionayo hayatoi nafasi mpira kuchezwa vijijini nje ya miji mikubwa. Ili tupate vipaji halisi kwa manufaa ya soka letu ni mpira upelekwe kusikochezwa mpira yaani mpira utoke uswahilini najua yote haya hayawezekani kwa kuwa jibu litakuwa hakuna FEDHA .baada ya jibu hilo ndio kusema hakuna mafanikio kamwe ya mpira ktk nchi hii. Lkn hayo yakitekelezwa na baada ya timu kupatikana tukiweka malengo wapi twende. Ligi ichezwe muda mfupi. Timu iondoke hapa nchini iende ziara ndefu ya mafunzo huku ikipata mechi nyingi za majaribio sina shaka CHAN.AFCON auWorldcup tutashiriki au moja ya vikombe hivyo tutabeba ni wavivu tu wakufikiria mbali hutupa lawama zao kwa yanga au simba hivi ni vilabu vinavyopaswa kuheshimiwa kwa walau kujaribu kulea wachezaji kwa kiwango cha kimataifa kiasi cha makocha kuona wachezaji wameiva na kuwateua timu ya taifa au vilabu hivyo kusajili na kuwakomaza wachezaji walioitwa timu ya taifa wakiwa hawana uzoefu.

    ReplyDelete
  5. Kwa kuwa hatuna wachezaji wengi wa kimataifa, tuboreshe ligi yetu ili tupate wachezaji wengi wa kiwango kizuri. Kocha mzuri na tunaelekea pazuri

    ReplyDelete
  6. KUNA UMUHIMU SASA KWA WADAU WA SOKA NAO KUWEKEZA KATIKA SOKA NA KUIMARISHA NA KUZIPA UWEZO TIMU AMBAZO ZINAMILIKI TIMU ZA WATOTO WADOGO KUANZIA UNDER 14 NA KUENDELEA IKIWEZEKANA PIA KUWEPO KWA MICHUANO YA KUANZIA UNDER 14, 17 ,21 KWA UMRI SAHIHI HAPA NADHANI TUNAWEZA KUPATA VIJANA WA KUWAANDAA KWA AJIRI YA MICHUANO IJAYO NA TUTAKUWA NA TIMU NZURI YA TAIFA KWANI MPAKA SASA HUWEZI SEMA UNATARAJIA KWENDA KOMBE LA DUNIA KWA WACHEZAJI WALIOJIFUNZA WAPI?

    MPAKA SASA TANZANIA HAKUNA TIMU YENYE UNDER 14 INAYOSHIRIKI LIGI KUU WA DARAJA LA KWANZA.

    HATA SIMBA INAYOSIFIKA INATIMU YA VIJANA PIA NAYO VIJANA HAO HUWA INAWATAFUTA KIPINDI HIKI CHA USAJIRI

    NAVIPONGEZA VITUO HIVI KWA KUJARIBU KULEA VIJANA JAPO HASIUNGWI MKONO NA TFF WALA VYAMA VYA SOKA MKOA NA WILAYA

    SHEIN RANGERS MAKUMBUSHO TALENT SINZA ACADEMY BONDE FC MAGOMENI ACADEMY ZOTE HIZI NI ZA KINONDONI
    SIJUI KWA MIKOA MINGINE JAPO NA TEMEKE NA ILALA KUNA VITUO KAMA HIVI ILA VINAKOSA SAPOTI YA WADAU
    NAMPONGEZA (FATHER) WA DAYOSA KWA KUJITAHIDI KUWA ANAANDAA MICHUANA PALE KARUME YA VIJANA WADOGO JAPO HUWA ANAKOSA WADHAMINI.

    HII KAMATI ILIYOUNDWA KWA NINI SASA ISISAIDIE KUWEKEZA KWA VIJANA WADOGO

    ReplyDelete
  7. jamani nyoni atafutiwe mbadala tujitahidi kutafuta mwakala wa kueleweka kuna baadhi ya wachezaji watanzania kucheza bongo na afrika kwa ujumla wanajipotezea muda na kudumaza vipaji vyao

    ReplyDelete
  8. Tutafute Plan B,nasi tujaribu kuajili mkurugenzi wa ufundi kutoka nchi zilizoendelea kama walivyofanyaga Zambia,inaweza kusaidia badala ya kutegemea hawa wanaobebana kila siku.

    ReplyDelete
  9. Tuanze kwanza kwa kuacha tabia ya kujipanga kwa mashindano yajayo. Kwahio tuanze na wewe kuangaia mbali zaidi ya mashindano yafuatayo. Hatuko vizuri kihivyo. 2014 imetoka sasa tunaangalia 2015 maana ndio mashindano yajayo. Hatuwezi kwenda mbele namna hio. Kungangania 2014 ndio kunamfanya Kocha amchezeshe Kapombe beki 3 badala ya kutafuta natural beki tatu ambaye kwa sasa asingemudu lakini angepata uzoefu mzuri kwa mashindano yajayo. Ukishapanga mipango kwa miaka 5 ijayo haya mambo ya timu za vijana yatakuja yenyewe tu. Tuangalia mbali.

    Hatuna vipaji na hatuko level ya kuwa na jipanga kwa mashindanyo yanayofuata. Hio tuwaachie kina Ivory Coast. Hatuko level yao. TFF tambua hilo, na msimpe kocha vigezo vya mkataba vinavymlazimu kupiga short cut. Itakuwa yale yale ya kosakosa kama hizi. Kumbuka kosakosa hizi tumeanza wakati wa Maximo. Tujipange!!!

    ReplyDelete
  10. No shortcut jamani.Michezo yote ni taaluma kama taaluma nyingine.TUSIPOWEKEZA kwenye vijana hatufiki kokote.Haya matokeo ni ya kila siku.Na cocha aache uswahili kila siku anatudanganya tumeonewa,nani atuonee?kwa kip hasa?mipango endelevu inahitajika sana.Haya mambo kila siku team imejitahid,sema haikuwa bahati hayana tija.Mfano wa waliowekeza tu hapa Africa ni Mzee Bakhresa na matunda yake yanaonekana,Moise Katumbi DRC,.....tumerudisha michezo mashuleni nini hatma ya wanamichezo wanoshinda kla mwaka kwenye umiseta?We lack plans and we dont know the value of the trophies we compete for.

    ReplyDelete
  11. Mwalimu kaingia siasa za Bongo, haingii akilini umwache David Luhende ukamchukue Erasto Nyoni ambae hajacheza muda mrefu akiwa amefungiwa na club yake wakati amefungisha Morocco kitoto sana eti anamkimbia mchezaji awe OFFSIDE! na jana ndo yeye aliwapa kazi ngumu mabeki wenzie kina Kapombe, Yondani na Cannavoro, tena mi nilikuwa na wasiwasi na Cananvaro lakini wapi alijitahidi sana. Muda wa kufanya Sub kwa nini asingemuingiza Chuji mapema akawa anapiga pasi ndefu kwa Ulimwengu na Samata hali ingekuwa nyingine sasa hivi! Mwalimu ametuangusha Vijana wamefanya kazi kubwa sana!

    ReplyDelete
  12. Njia nzuri ni kuwekeza kwa vijana timu za vijana tena kuwapeleka nje Ulaya wakacheze huko na wakati huo huo waje kusaidia taifa tangu vijana wadogo wajengwe katika misingi hiyo, mfano mdogo tu angalia mechi ya jana hatukufungwa kwa sababu hatujui mpira tulifungwa kiakili, tulifungwa kinguvu na tulifungwa kinidhamu, Wenzetu Ivory Coast walikuja kugombania point Tatu, akili yao yote ilikuwa kwenye point tatu , wakati sisi ilikuwa kwenye kuhakikisha namkaba kolo au napiga visigino, kanzu chenga n.k wao kilichowaleta ni point tatu kwa kutumia akili nguvu na nidhamu wamechukua sisi tunabaki kwenye magazeti eti vijana wameonyesha uwezo wa hali ya juu, uwezo upi, unaouzungumzia? mimi sielewe kwani pale tulikuwa tunagombania uwezo au point? hiyo ndio nidhamu tunayoizungumzia kua SERIOUS mchezoni, kitu ambacho wachezaji wa Tanzania hawana kutokana wananavyoburuzwa na viongozi wajinga kabisa waliopo. Viongozi na Wadhamini ni watu ambao hawafai kabisa tena wapenda michezo msipoamka mtaendelea hivi hivi- chukuli aeti wanaunda kamati ya ushindi, hii kamati nini ? na ishinde nini? kazi kuiweka timu kambini na kuweka walinzi kulinda wakati wanzetu wachezaji wao hawalindwi wanajua jukumu lao hiyo ndio nidhamu tunayoizungumzia, Wadhamini wandhamini nini? mimi mpaka leo sielewi maana naona wanalipa kambi nauli za timu na mishahara labda wewe mdhamini hana programu yoyote ya maendeeleo anachojua mdhamini ni kua anatoa hicho tena ni pesa ya mtanzania maana anasemehewa kodi hivyo siyo pesa yake anatumia kivuli cha ufadhili ili kukwepa kodi sasa tuonyeshini hata maendeleo ya udhamini. wenzenu kama hawaoni maendeleo wanaacha kudjhamini sasa nyinyi hamna program za maendeleo na kama zipo basi chini kwa chini, technical director sijui anafanya nini masikini ya mungu yupoyupƄo tu kwa nuda mrefu hana lolote badilikeni angalieni Azam kila siku anaendelea tu kutokana mipango endelevu

    ReplyDelete
  13. MUMENIKERA ETI WAMEONYESHA VIWANGO VIWANGO GANI? KWANI TUNAGOMBANIA VIWANGO? WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO COMEON TUMEFUNGWA ANDIKENI UKWELI WALIONYESHA KIWANGO MIMI NADHANI WALIOSHINDA

    ReplyDelete
  14. kocha kim Paulsen afungashe virago hana sifa ya kufundisha timu yetu ya taifa.wachezaji wengi wa timu ya taifa hawana uchungu na timu.cha kufanya watafutwe wachezaji wenye maumbo makubwa futi sita na kuendelea na wafundishwe mpira miaka miwili then tutaweza kucompete na watu kama ivory coast..ukitazama vizuri mechi zote tatu tulizopoteza ni kwa ajili ya kuwa na wachezaji wenye maumbo madogo.mpira ni taaluma ,maximo alitaka kuwatafuta wachezaji wenye maumbo makubwa tz nzima lakini TTF wakapinga wazo hilo kwa kuwa na mapenzi na wachezaji wa ligi kuu ambao ni dwarfs,umeona wapi beki anakuwa na umbo dogo kupita forward anayemkaba? ndio maana tunapata aibu kila siku.nimewatazama vizuri waivory coast jana wengi hawana foot work nzuri ila walikuwa wanatuzidi kwa ajili ya kuwa na nguvu zaidi ya wachezaji wetu.la sivyo itakuwa ni ndoto za alinacha

    ReplyDelete
  15. Naona TFF waondokane na Usimba na Uyanga ili isimamie soka kikamilifu kufanya ligi iwe bora zaidi ya hapa. Pia TFF ijifunze kucheza nje ya uwanja yani mbinu za nje ya uwanja mbona wenzetu wanafanya hivyo na kupata matokeo, sisi zetu kusimamia mapato tu ambayo ni kamradi kawachache.

    ReplyDelete
  16. Shaffih Dauda vocha yangu coz nilitabili sahihi kikosi cha stars jana 0716383102

    ReplyDelete
  17. kuna umuhimu wa viongozi wa soka katika ngazi za klabu,wilaya,mkoa na taifa kila mmoja kuwajibika ipasavyo katika maendeleo ya soka ya eneo lake.Kuwepo na mafunzo ya makocha katika ngazi zote hasa ya awali,kuwepo kwa viwanja vya kutosha vya soka mitaani na mashuleni,kuandaa mazingira bora ya kendesha vituo vya soka vya watoto na timu za soka za watoto mitaani na mikakati ya kuibua vipaji na kuviendeleza na kuwa na mawakala wa uhakika wa kuwatafutia timu wachezaji wetu nje ya nchi katika vilabu vya kueleweka badala ya kwenda Vietnam.Haya yote yanahitaji ushirikiano wa wadau wote badala ya kuiachia TFF peke yake ambayo ni ngazi ya kitaifa.Mwisho timu ziwe na makocha wa kueleweka kama Yanga na Azam badala ya kuendekeza deiwaka kama wafanyavyo Simba

    ReplyDelete
  18. 1.ligi yetu iwe bora kwa mdhamini kutoa fedha ya kutosha kwa timu zote ili mpira wetu uwe na ushindani mkubwa na sahihi
    2.tuwekeze kwenye soka la watoto kuanzia 10,12,14,16,18 na 21,pia,tuwe na sera ya kupeleka wachezaji wetu nchi za nje kucheza mpira kwa wingi tu
    3.tusitarajie matunda ya muda mfupi katika mpira,tujipe muda sio chini ya miaka mitano (5) na kuendelea
    4.tufundishe kwa wingi tu makocha wazawa kwa ngazi mbalimbali ndani na nje ya chi ili kocha wa timu ya taifa awe na kazi ya kuchagua wachezaji wengi wazuri ambao wameandaliwa kimpira tangu ngazi ya chini kabisa

    ReplyDelete
  19. VIONGOZI WAACHIE NGAZI WANAJAZANA TU TFF BILA KAZI MAALUMU WAPOWAPO TU KUPIGA MAJUNGU YA YANGA NA SIMBA, WAKINA KAYUNI ANAFANYA KAZI GANI? HEBU NIAMBIENI WATANZANIA HUYU TECHNICAL DIRECTOR WETU NINI ANAKIFANYA KUNA MTU ANAWEZA KUTUELEZEA? MDAU HAPO JUU KAELEZA VIZURI SANA HAWANA MIPANGO ENDELEVU, HII KAMATI YA USHINDI NI KITU GANI? SASA KABLA YA HAYO YOTE TUNAYOONGEA YA KUBORESHA LIGI YETU NA KUWEKEZA ZAIDI KWENYE SOKA LA VIJANA, MIMI NAONA TUISAFISHE KWANZA TFF NA TENA TUANZIE KWENYE WIZARA HUSIKA MAANA WAMESHINDWA KAZI , HAWANA PROGRAM YOYOTE YA MAANA ZAIDI YA KUTEGEMEA KAMATI ZA USHINDI AMBAZO WANAZITUMIA KUPATA ULAJI, UKITAKA KUANGALIA WALE VIJANA WA TSA WAKO WAPI? KAMA SI THOMAS ULIMWENGU PEKE YAKE AMMBAYE ANAONEKANA HAYA VIJANA WANAO CHAGULIWA KWENYE COPA COCACOLA WANAENDA WAPI? NDIO UTAONA UOZO WA CHAMA CHETU CHA MPIRA FUKUZA WOTE HAO HAWANA MAANA KABISA

    ReplyDelete
  20. HATA WADHAMINI WATOE PESA VIPI HAITA SAIDIA KABISA NI KUWAPA PESA TU WALIPO MADARAKANI, LA MSINGI IWEKWE PROGRAM MAALUMU LA SOKA , HASA VIJANA KUWAPELEKA NJE AMBAKO AWATASAIDIWA KIELIMU, NGUVU NA NIDHAMU ACADEMY ZILIZOPO HAZISAIDIWI KABISA HAO WADHAMINI WANGEANGALIA ACADEMY ZILIZOPO HAPO BADALA YA KUZISAIDIA SIMBA NA YANGA TU .MFUMO WA LIGI UMEJAA UOZOO TU MITIMU YA JESHI MINGI NA HAINA USHINDANI WOWOTE VIWANJA VIBOVU MIKOANI HATA HAKUNA ANAYESHITUKA KUIKARABATI , MABENKI YAPO HAPO BADALA YA KUYASHAWISHI MAKAMPUNI KUJENGA VIWANJA VIZURI TUNAUNDA KAMATI ZA USHINDI UTADHANI NDIO ZINACHEZA

    WHY MNB AU CRDB NA MAKAMPUNI MENGINE YASI INVEST KWENYE VIWANJA VYA MIKOANI ILI KUWEKA USHINDANI? KAMA MAKAPUNI YANAWEZA KUWALIPA SEATLE SOUNDERS MABILIONI KWA NINI WATENGENEZE VIWANJA VYETU NA KUTENGENEZA MATANGAZO YAO KAMA WANAWEZA KULIPA MABILIONI KWENYE ENGLAND PRIMIER LEAGUE KWANINI WASHINDWE KUTENGENEZA YA KWETU UNAMJENGEA JIRANI MWENYE UWEZO UNASHINDWA KUJENGA CHAKO SIJAWIAHI KUONA, NA SISI TUNAKUBALI. KUNA WATANZANIA WANGAPI WAKO KWENYE HIZO TIMU AU LIGI TUNAZOLIPA MABILIONI KILA MWAKA? KWA NINI TUSIWAPELEKE NA KUWAWEKEZE VIJANA WETU BASI ILI BAADAE WAJE KUUTANGAZA HUO UTALII , SIO TUNAWAPA MABILIONI ETI TUNATANGAZA UTALII TIMU YETU YA TAIFA KUINGIA KOMBE LA DUNIA NI TANGAZO TOSHA KABISA LA UTALI TENA KWA KARNE, WACHEZAJI WETU WAKICHEZA KWENYE MALIGI MAKUBWA NI TANGAZO TOSHA KABISA KUITANGAZA NCHI TUNACHOTA MAJI KISIMANI TUNAMWAGA MTONI UOOZOOOO MTUPU

    ReplyDelete
  21. Kwanza tupate wadhamini wataotoa pesa ya kutosha kwa timu zetu za ligi kuu kuweza kujigharamia kila kitu kwa msimu mzima bila ya wasiwasi wowote. hiyo itasaidia ligi yetu kuwa na ushindani kukuza kiwango chetu na kuweza kuuza wachezaji nchi zilizoendelea kimpira na hatimaye kuwa na wachezaji wengi wa kulipwa watakaokuwa wanacheza nje.

    Pili Zianzishwe academy za kutosha na za kudumu za watoto kuanzia miaka nane na kuendelea.

    Kuwe na mafunzo ya kutosha kwa makocha wetu itasaidia kuwapa mafunzo wachezaji wetu tangu wakiwa na umri mdogo mashuleni na mitaani.

    Timu za taifa kuanzia U 16 na kuendelea ziwe na ufadhili wa kudumu kuziwezesha kushiriki mashindano yote ya kimataifa

    ReplyDelete
  22. wachezaji wazuri hafu wadogo wajikaze na kujituma tunakoemda sio kubaya ni dalili nzuri ya kuendelea...

    ReplyDelete