Search This Blog
Thursday, June 6, 2013
MAONI YA MDAU: WORLD CUP BRAZIL 2014 TANZANIA ISAHAU – PART 4
Watanzania wenzangu, hii ni part 4 ya maoni yangu niliyoanza tangia mwaka Jana November kabla Tanzania haijagusa mpira kwenye huu mzunguko wa pili wa Kombe la Dunia mtoano. Naandika leo ili isiwe kwamba namimi nilikumbwa na kile kihoma cha kuona mwanga mzima palipo giza katika soka letu la Tanzania. Nilianza kuandika part 4 siku chache baada ya Waziri wetu kuteua kamati ya kuipeleka Tanzania Brazil. Kabla ya hapo ni mara nyingi nimekuwa nikitaka kuandika kwenye kile tukio muhimu ambalo limepita tangia mwaka jana. Kwa kila tukio lipitalo naona sisi kama watanzania tunapoteza ile nafasi nyingine ya kweli na ya kwanza ya kujenga kitu cha muda mrefu.
Ukianza na programmu mpya ya miaka 3 ambayo TFF ya sasa iliona ni busara kuileta mbeleni kwetu wakati bado wanajua mabadiliko ya uongozi yalikuwa yanakuja sio chini ya miezi 2. Hii ilikuwa kabla ya FIFA kutuongezea muda. Tukatoka hapo tukasikia yale ya Copa CocaCola ambayo umri wa ushindani ulishushwa chini. Tukumbuke ingawa maamuzi yalikuwa ni mazuri sio TFF walioyoyaamua ni Copa CocaCola wenyewe. Tukapita tena kwenye maamuzi ya kumwongezea mkataba mpya Kocha wetu wa sasa ambaye kwa ukweli amefanya kazi nzuri na timu yake mpya.
Swali la kwanza niliuliza bila kupata jibu, vigezo alivyopewa kwa mkataba huu ni vipi maana hivi ndio vinamuamulia yeye maamuzi yake. Na hii ndio ishara nzuri kwetu sisi kujua TFF wana mpango gani na mpira wetu wa hapa nyumbani. Ukimsikia Kocha na la zaidi sana ukaangalia maamuzi yake ambayo amekuwa akiyafanya ya wachezaji ni dhariri kutambua kwamba ajira yake inategemea mafanikio ya karibuni na sio ya mbali. Inakuwa rahisi kujua anatagemewa alete raha kwa watanzania leo na sio kesho. Kwa swala la mpira (leo ni miaka 1-2 ijayo, wakati kesho ni miaka 3-6 years later).
Lakini nilianza kuandika hata kabla ya uteuzi huo, niliandika pale TBL walipotangaza udhamini mpya wa Taifa Stars ambao ni mnono. Nikawapongeza TFF kwa kupata mkataba mnono lakini hapo hapo ikaonekana TFF wakapoteza nafasi murua ya kujenga programmu ya muda mrefu kutumia hilo fungu. Mwenyekiti alizungumzia zaidi uwezo wa timu yetu kucheza mechi za kirafiki nyingi zaidi na kuwa kambini zaidi na kulipa wachezaji zaidi. Yote hayo ni mazuri sana kwa yule ambaye analenga leo na sio kesho na hiyo ndio TFF yetu. Mmeonyesha mnaangalia umbali gani katika swala la maendeleo ya mpira wetu.
Watanzania tunaupenda mpira na tunahamu sana na mafanikio na kwa ukweli vijana waliopo sasa hivi wanatia moyo. Sema tusidanganywe na TFF kwamba wingi wa vijana ni kutokana na falsafa fulani ya vijana iliyowekwa na TFF au Kocha. Generation X ya vikongwe imeisha, wamecheza mpaka miguu yao imeshindwa kucheza zaidi na ndio maana hawaonekani tena, sio tu kwenye Taifa Stars lakini hata kwenye ligi yetu. Vijana waliopo wako sio kwa sababu ni vijana, lakini kwa sababu mpira wao wa sasa (ambao bado mapungufu ni mengi sana) unasaidia timu yetu kuliko mpira wa wale Generation X. Hio sio falsafa ya vijana. Tuelewe hilo kwanza. Kwahiyo tuwashukuru Generation X, maana hao walikaa sana tangia ujana wao alipokuja Maximo. Nae harufu ya mafanikio ya haraka ilimponza maana alianza vizuri sana kwa kumjenga mtanzania kwamba mafanikio sio leo au kesho. Ile kosa kosa na mafanikio madogo ikambidi abadili agenda. Mengieno tunayajua. Kinachosikitisha ni kushindwa kwetu kuliona hilo.
Nirudi kwenye Mada, nayo ni Brazil 2014 tusahau. TBL wadhamini wetu wametoa hela nyingi na kibiashara ni lazima wapate chao na kwa sasa wanapata sana chao kutokana na mafanikio ya vijana wetu. Lakini TBL hawawezi kuipangia TFF na serikali mpango wa maendeleo ya mpira wetu. Hawawezi kuwasukuma TAIFA zima tukaingia kwenye programmu ambayo kiukweli hatuna nyenzo ya kuiendeleza kwa spidi hiyo hiyo pale tushindwapo kuingia Brazil na nafasi ya kushindwa kwenda bado ni kubwa mno. Tusidanganyane na mafanikio yetu ya karibuni.
Ni kweli mpira ni duara na hali ya timu yetu tunaweza kuwa surprise na tukaenda. Lakini kwa vijihela tudogo tulivyonavyo kwanini tusivitumie zaidi kujenga timu hii ili kweli 2018 tuwe na timu ambayo nafasi ya kwenda Kombe la Dunia itakuwepo kutokana na uwezo wa timu yenyewe?
TFF kama mnauelewa mpira hamuwezi kuweka kigezo cha renewal ya mkataba kwa kocha kuwa kushiriki 2014. Kuna timu zisizofika 10 Africa hii ambazo zinaweza kufanya hivyo maana kweli zinategemea hilo, kama nchi na timu kwenda 2014 kuko mikononi mwao. Tegemeo la dua sio kubwa sana kama kina sisi.
Kwa nini tunawapa vijana wetu pressure yote hii? Mheshimiwa Waziri, kamati ya mechi tatu ijayo ni kamati gani maana nao mnawaweka kwenye pressure ya bure ya kuleta mafanikio wakati ni ngumu sana. Tunakuwa kama tunarudi kwenye kamati zinaozoundwa kabla watani hawajacheza tu. Tunatambua vyema kabisa tukitumia historia yetu kwamba baada ya kushindwa hizi kamati zinakufa maana msukumo unaisha. Zinarudi tena pale tunaponusa kanafasi ka miujiza tena kama hii sasa ya 2014 ambayo mimi naiita nafasi ya miujiza. Huwezi kuwalaumu maana msukumo unaendana na muda. Ukiwapa target ya 2018 basi watajipanga ipasavyo. Haimaanishi hawatajaribu kuweka nguvu kwa 2014 lakini hiyo nguvu itatumika kwa busara maana watakuwa wanatambua mipango/fungu watakalotengeneza ni la kutimiza project ya miaka 5 ijayo sio miezi mitatu ijayo.
TFF kwa bahati mbaya hamna cha kupoteza na mwenendo huu, maana mnachoangalia ni kuonyesha tu kwamba mlitusogeza mpaka tukaanza kufikiria kwamba kweli tunaweza kwa 2014. Lakini mnachokosea ni kwamba mnafanya hivyo kwa kutowajali wale wanaokuja maana mnawaweka kwenye mazingira ya kuanza upya kwa kiasi fulani, kama mngekuwa mmeweka system yetu ambayo mnajua ikiendeshwa vizuri 2018 tutaweza kushindana kabisa kuchukua moja ya hizo nafasi.
Hamna nafasi nzuri kama hii ya kuweka mipango mizuri ya timu zetu za Taifa. Tusiende kwa pupa ambayo kushindwa kwetu 2014, kutaathiri nafasi yetu ya kushindana mbeleni. Tumeshapitia situation hizi tayari ingawa mtanzania mwenye hamu ya kufarijika anaweza kusema amesahau. Lakini nyie TFF hamuwezi kusema mmesahau kwahiyo inasikitisha sana kuona mnaelekea barabara hiyo hiyo bila tahadhari yoyote.
TFF mmefanya maamuzi mengi magumu hizi sekunde chache za mwisho bila kutuelimisha hizo programmes tofauti zilizopo zinakutania wapi? Kuna Umisseta, Umitashumta, Copa Coca Cola, Airtel Rising na wengineo. Tunajua macho na masikio kwenu ni kwenye hizi zenye mvuto wa fungu. Tunachoomba ni mtuelimishe baada ya yote mnakutania wapi na lini?
Ukiangalia magazeti, na sehemu nyingi zote, imani ya vijana wetu kufanikiwa iko vizuri. Tumetokea mbali sana na hii imani sio imani hewa tu, tumeona maendeleo ya mpira ya timu yetu na inatia moyo. Siandiki haya kuwavunja moyo watanzania wenzangu, natoa tahadhari kwamba na nyie mnachangia sana sana sana kwa hali yetu duni ya mpira hapa. Bila nyie kwanza kuwa na subiria, viongozi wetu mtawayumbisha maana wengi wanafanya maamuzi kwa kusikilizia maswala ya leo na sio kwa lile wanaloliona la msingi kufanywa kesho na keshokutwa.
Media, tunawahitaji sana sana kwenye swala la kuwahamasisha vijana wetu lakini lazima liwe na uwiano. TBL wasiwaburuze na nyie mkaanza kuimba wimbo huo huo bila tahadhari yoyote. Huu ni muda mzuri kwa wadau wa mpira kushirikiana na kuweka mikakati ya mpira wetu kwa siku za mbeleni. Msibakie kusukumia 2014.
Tuwaombee Taifa Stars mafanikio mema kwenye mechi zijazo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
NUDGU MWANDISHI UNAYEJIITA MDAU NA BILA KUTAJA JINA LAKO.......PAMOJA NA MAKALA YAKO NZURI PAMOJA NA MAPUNGUFU YA TFF.....NAONA MAKALA YAKO INAUPUNGUFU NA INALENGA KATIKA CHUKI KWA TFF NA TAIFA STARS NA HIVYO WATANZANIA KWA UJUMLA NA SIDHANI KAMA UNA NI NJEMA NA NCHI YETU.....!!
ReplyDeleteALIPOKUJA MAQXIMO LENGO LILIKUWA W CUP 2014 NA HILI NDIYO LIMEKUJA NA TIMUN ALIYOIANDAA MAXIMO WAKATI POLSEN ANAANDAA VIJNANA WALIOPOSASA NA KUCHANGANYA NA WALE WA MAXIMO UNATAKA NINI.....MFANO KASEJA, CHUJI, CANAVARO NA WENGINEO NI KIZAZI CHA MAXIMO MSUVA DOMAYO DIDA NA WENGINEO NI KIZAZI CHA PALSEN JE WEWE ULITAKA TUWE NA KIZAZI MAALUMU CHA W CUP PASIPOKUWA NA SUCCESSION..?
KUHUSU KAMATI MIAKA 7 KWENDA W CUP 2018 UNATAKA KAMATI IFANYE NINI KAMA SIYO KUWA NA PROGRAMME KABISA.....KAMATI IMEWEKWA KWAAJILI YA KUWEKA PRESSURE NA KUWAHAMASISHA SIYO WACHEZAJI TU BALI HATA WA TZ WOTE.....!!
'STEERING COMMITTEE' HUWEZI KUIWEKA MADARAKANI KWA MIAKA ZAIDI YA 5 HAPANA NA HAIWEZEKAANI NILITARAJIA UNGESEMA SERIKALI INGEUNDA KAMATI SIKU YA KWANZA WAKATI MECHI ZA MTOANO ZINAANZA HAPO TUNGEONA 'IMPACT' YAKE......!!
NAKUOMBA USITUCHANGANYE WA TZ KWA MAKALA YAKO INAYOONYESHA CHUKI KWA TFF NA TBL......!!
TULIPO HAPA NI PROGRAMME YA SIKU NYINGI NA NDIYO MAANA SERIKALI ILIAMUA KUINGILIA KATI KWA KULIPA MAKOCHA NA INAWAAJILI WAO....!!
PENGI HUELEWI MAANA YA 'PROGRAM'
KATIKA PROGRAM NI VIZURI UKAFIKIRIA KUFANIKIWA KWA JUU 'YOU NEED TO AIM HIGH' ILI UKIPATA PUNGUFU UNAFARIJIKA.....TAIFA STARS ILIPOFIKIA SIJAONA MANTIKI YA KAULI YAKO KWA SASA NA SAMAHANI KAMA NITAKUITA SIYO MZALENDO KWA ANDIKO LAKO...!!
"VIVA TAIFA STARS...........VIVA TANZANIANS HERE WE GO 2014 IS HERE AROUND THE CORNER AND TOGETHER WE CAN"