Search This Blog

Thursday, June 6, 2013

MALIPO YA DA YA UHAMISHO YA NEYMAR: SANTOS WADAIWA KUWADANGANYA WAWEKEZAJI KIASI HALISI WALICHOLIPWA NA BARCA

Mmoja wa wawekezaji wa Neymar amewaambia FIFA wahunguze uhamisho wa wa mshambuliaji wa huyo wa Brazil aliyehamia Barcelona, akidai kwamba hajapata mgao wake kwenye ada ya uhamisho ya kiasi cha €57 million waliyolipwa Santos na Barcelona. 

Wakati wa utambulisho wa Neymar kule Camp Nou siku ya Jumatatu, makamu wa Raisi wa Barca Jose Maria Bartomeu alisema kwamba klabu yake imelipa jumla ya €57 million iliyogawanywa kwa Santos na na wawekezaji wengine wa Neymar.

Bartomeu pia alithibitisha kwa waandishi kwamba Barca walishatoa 'kishika uchumba' cha €10 million huko nyuma, fedha ambazo zimejumlisha kwenye €57 million.
Mmoja wa wawekezaji waliohusika na Neymar ilikuwa kampuni ya uwekezaji ya DIS, ambayo mkurugenzi wake ni Roberto Moreno ameiambia radio ya Catalan iitwayo RAC1 kwamba Barca wamevunja sheria za FIFA kwa kulipa €10 million kabla, wakati mchezaji huyo akiwa bado na mkataba na Santos.

"Barca wanatambua kwamba walilipa malipo ya €10 million wakati Neymar akiwa bado ni mchezaji wa Santos," Moreno alisema. "Huu ni uvunjaji mkubwa wa Kanuni za FIFA kwa sababu mchezaji huyo alikuwa bado kwenye mkataba na Santos." 

Kampuni ya DIS iliripotiwa kuwa na umiliki wa 40% ya haki za usajili wa Neymar mpaka wiki hii, hivyo walitegemewa kupokea kiasi cha €22.8 million kama mgao kwenye ya uhamisho. Japokuwa, Moreno amesema DIS wameambiwa watapokea kiasi cha €9.6 million kutoka Santos [40% ya €17 million].
"Tumeona kwenye TV kwamba Barca wamesema uhamisho ulikamilika kwa €57 million," Moreno alisema. "Lakini hapa Santos wanaongelea kiasi cha €17 million. Tunahisi tunachezewa mchezo mchafu. Santos wanauficha ukweli ili wawekezaji wapokee fedha kidogo."
Akiongea siku ya Jumatatu, Bartomeu alisema kwamba majadiliano yalichukua muda mrefu lakini hakuweza kusema maelezo zaidi kuhusu mgawanyo wa fedha kwa wawekezaji wote wa Neymar.

No comments:

Post a Comment