Klabu ya Simba SC ipo katika harakati nzito za kuhakikisha haimpotezi kiungo wake tegemeo Amri Kiemba ambaye anakaribia kutua Jangwani kwa wapinzani wao wa jadi mabingwa wa Tanzania bara Yanga.
Taarifa za uhakika ambazo mtandao huu imezipata ni kwamba Simba wameingilia kati dili la uhamisho wa Kiemba kwenda Yanga kwa kufanya mazungumzo na kiungo huyo ambaye alishawahi kuichezea Yanga miaka kadhaa iliyopita.
"Muda huu mchana Simba ipo katka mazungumzo na Kiemba ili kuweza kumshawishi asisaini Yanga na aendelee kubaki Msimbazi, lakini ili kuweza kubaki Simba Kiemba amewaambia Simba inabidi wamlipe mshahara zaidi ya aliokuwa akilipwa kwenye mkataba wake uliopita na pia wampe millioni 38 kama fedha za usajili," kilisema chanzo cha habari.
Pia Simba inajiandaa kumsajili Hamis Kiiza ikiwa Kiemba ataenda Yanga.
aende tuu kwani yeye ni nani?? huko yanga si ndio alitimuliwa kuwa kiwango kimeisha, simba wakamuonea huruma wakampa nafasi?? wachezaji wabongo ndo maana hawaendelei, mi naona aende tuu tuna makinda kibao tutakuza
ReplyDeletestory zako bwana hazina kichwa wala miguu upo nyuma sana mkuu, ume-post issue ambayo wenzako walishamaliza na jeshi la jiwe kisha anguka wino
ReplyDeletesimba sajili huyo kiemba maana sisi migogoro hatuihiji na kumbken baada ya okwi ndo nafasi ya 3 vpl
ReplyDeleteWatu wanaangalia maslahi kwani leo hii nurdin akipewa donge nono aache kwenda simba kisa walimtema?tusikurupuke wakati wa kucomment.
ReplyDeleteHalafu post zako zinakuaga kinazi nazi sana...sijui..kwanza siku za hapo nyuma ulishatupaga break newz kuwa ameshasaini yanga...
ReplyDeleteMi nadhani kama mwenye blog hii ni mnazi au anachelewa kutupa habari anzisha ya kwako ambayo haioneshi unazi na iko current sana, maana wengine kazi zunu kukosoa tu
ReplyDelete