Search This Blog

Tuesday, June 11, 2013

BREAKING NEWS: AMRI KIEMBA ASAINI SIMBA KWA MILLIONI 35

Hatimaye mazungumzo baina ya Klabu ya Simba na mchezaji Amri Kiemba yamemalizika kwa pande hizo mbili kukubaliana kuongeza mkataba mpya.

Mchana wa leo Simba ilikuwa kwenye jitihada nzito kuhakikisha inamzuia Kiemba kusaini Yanga kwa kumpa ofa nono ya mkataba mpya, Kiemba alikuwa akihitaji kiasi cha millioni 38 ili asaini msimbazi lakini baada ya mazungumzo marefu Kiemba amekubali kusaini kwa kiasi cha millioni 35 kwa miaka miwili.

Pia Kiemba atakuwa analipwa mshahara wa millioni 2 kwa mwezi. Alisaini mkataba huo mbele ya kaimu makamu mwenyekiti  Mzee Kinesi.


3 comments:

  1. Hongera Mzee Kinesi....well done.
    Sasa msake huyo striker wa nigeria asaini.

    ReplyDelete
  2. Hongera mzee kinesi na wenzako ila tafuteni vyanzo vya uhakika vya mapato ili hiyo mishahara mikubwa kwa wachezaji muweze kuwalipå kinyume cha hivyo wachezaji wataambiwa hawana nidhamu wanapodai chao

    ReplyDelete
  3. At least umethibitika ukweli maana tumeshaona viblog na vijarida vya watu wavivu wa kutafuta habari sahihi vilikuwa vinawasumbua watu sana, mara BREAKING NEWS: KIEMBA ASAINI YANGA... baadae bila aibu BREAKING NEWS: AMRI KIEMBA ASAINI SIMBA..mtu wewe wewe!!! kituko!

    ReplyDelete