Serikali imekiri kuwa haina utaratibu rasmi wa kuwasaidia wanamichezo waliolitumikia taifa, pindi wanapokumbwa na matatizo.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa Bungeni na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni Idd Azan.
Azan alitaka kujua ni utaratibu gani ambao serikali imekuwa nao juu ya kuwasaidia wananichezo wenye matatizo waliyowahi kuzitumika timu za taifa, kama vile nahodha wa Taifa Stars, Jellah Mtagwa ambaye kwa sasa anasumbuliwa na maradhi.
Akijubu swali hilo, Makalla alisema kuwa serikali haina utaratibu rasmi wa kuwasaidia wanamichezo wake waliowahi kuzitumikia timu za taifa pindi wapokuwa na matatizo isipokuwa imekuwa ikiwaenzi kupitia utaratibu usio kuwa rasmi.
"Serikali haina utaraibu rasmi wa kuwasaidi wanamichezo waliowahi kuzitumikia timu za taifa wakati wanapokuwa na matatizo.
"Hata hivyo imekuwa ikiwaenzi kupita kwa vyama mbalimbali vya michezo hapa nchini kwa kuwapa tuzo kutokana na kutambua mchango wao," alisema Makalla.
Katika hatua nyingine serikali kupitia kwa Naibu huyo wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo haikuweza kuweka wazi kama itamsaidia Mtagwa mara baada ya Azan alipouliza swali la
nyongeza kuwa serikali inampango gani katika kumsaidia mchezaji huyo wa zamani ambaye alitumikia Taifa Stars kwa zaidi ya miaka 15 na kuingizia serikali mamilioni ya fedha kupitia shirika lake la posta lililokuwa likiuza stemp zilizokuwa na picha yake.
Mtagwa ni miongoni mwa wachezaji wa Taifa Stars waliyoiwezesha Tanzania kushiriki katika Fainali za Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza mwaka 1980 nchini Nigeria.
Hata hivyo tangu mwaka huo Tanzania hajawahi tena kushiriki katika fainali hizo na mara kwa mara imekuwa ikishia njiani.
No comments:
Post a Comment