KAMPUNI
ya S. S. Bakhressa ilipoanzisha timu ya soka ya Azam FC, viongozi na mashabiki
wa klabu kongwe za Simba na Yanga walidhani ni nguvu ya soka.
S.
S. Bakhressa ikapiga hatua ya pili kwa kujenga uwanja wa kisasa, Chamazi,
Temeke, Dar es Salaam, ikiwa ni ishara ya dhamira ya kufanya mapinduzi ya soka
nchini.
Mbali
ya kujenga uwanja wa mazoezi (unatumika hata kwa mashindano) na uwanja mkubwa
wa kisasa ambao ujenzi wake ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni,
S.S. Bakhressa imeingia hatua nyingine kubwa kwa kuanzisha kituo cha
televisheni cha Azam TV.
Moja
ya malengo ya Azam TV inayojenga barabara ya Nyerere ni kutumia kiasi cha Sh.
1.5 bilioni kuonyesha moja kwa moja mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Ikiwa
itapata haki ya kuonyesha ‘live’ mashindano hayo, taarifa zinasema Azam TV
imejipanga kutoa Sh. 100 milioni kwa kila timu kati ya 14 zitakazoshiriki msimu
ujao wa ligi hiyo. Hii ni neema kubwa kwa klabu zote hasa changa.
Hii
ina maana sasa angalau kila timu, itaweza kujikimu kwa kiasi chake na kuweka
karibu uwiano sawa wa kuchuana na timu zenye uwezo mkubwa wa kifedha kama
Simba, Yanga na Azam FC iliyo chini ya kampuni ya S. S. Bakhressa.
Kwa
hiyo, timu zisizo na wadhamini mkubwa na ambazo ndiyo kwanza zimepanda daraja kama
Ashanti United ya Ilala, Mbeya City ya Mbeya na Rhino ya Tabora na hata
zilizopo kama Coastal Union zitanufaika kwa kiasi kikubwa na ujio wa udhamini
wa Azam TV.
Timu
zilizoshuka daraja za Toto African, African Lyon na Polisi Morogoro zitakuwa
zinasikitika neema kuja kwenye ligi wakati zimetupwa nje.
Msimu
uliopita tuliiona Toto ya Mwanza ikishiriki kwa tabu ligi hiyo huku wachezaji
wake wakilala katika basi wakati mwingine huku chakula pia kikiwa shida. Hali
hii inachangia kwa kiasi kikubwa timu hizi ambazo hazipo chini ya taasisi kubwa
kufanya vibaya hasa katika mechi zake za umbali mrefu na wakati mwingine hata
zile za katika kituo chake.
Kwa
vyovyote vile Azam TV inakuja kuleta ushindani mkubwa siyo katika udhamini tu,
bali hata urushaji wa vipindi vya michezo.
Lakini
Simba na Yanga zilizoanzishwa kabla ya uhuru ‘zinapanga’ hujuma. Simba wanadai kiasi
cha Sh. 100 milioni ni kidogo na hakilingani na hadhi yao na pia hawawezi
kulipwa sawa na timu nyingine za ligi hiyo.
Mwenyekiti
wa Simba, Ismail Rage amenukuliwa na gazeti moja la michezo akisema anakubaliana
na wazo la Azam TV, lakini kiasi hicho cha fedha ni kidogo kwao na hata siku
moja timu haziwezi kulipwa haki sawa ya matangazo huku akitolea mfano katika
Ligi Kuu ya England.
Kwa
upande wa Yanga, Ofisa Habari wake, Baraka Kizuguto amesema hawezi kuzungumzia
vitu vya tetesi kwani Azam TV hadi sasa hawajawapelekea taarifa rasmi kuhusu
lengo hilo la kuonyeshwa kwa mechi zao msimu ujao.
“Sipo
katika nafasi nzuri ya kuzungumzia jambo hilo, kwani hatujataarifiwa jambo
lolote juu ya mpango huo wa Azam TV, wakituletea maombi yao, sisi kama timu
tutakaa na kutoa uamuzi,” anasema Kizuguto.
Hii
ina maana kwamba, kama Simba na Yanga zitabaki na mawazo hayo, Azam TV inaweza
kukwamishwa katika mpango huu na kubaki na ule wa kuonyesha mechi za timu yao
tu, kwani lengo lao ni kutangaza biashara zao.
Utaratibu
ni kwamba muda ukifika, uongozi wa Azam TV utaomba kibali cha kudhamini Ligi
Kuu kutoka Kamati ya Ligi ambayo itapanga kiwango baada ya kuteta na klabu.
Vituo
vya TV vikionyesha ‘live’ mechi yoyote ya ligi hupaswa kulipa gharama kufidia
kiasi cha watu ambao hawataingia uwanjani na kutumia fursa hiyo kurusha
matangazo ya biashara. Azam TV haitazungumza na klabu binafsi.
Lakini
kwa desturi za Simba na Yanga, ambazo miaka nenda rudi ni kupanga mikakati ya
kuangushana, hata hili zinaweza kukwamisha. Kwa husuda zitaweka mgomo ili mpango
huu ufe ili zenyewe zibaki kutawala soka, timu ndogo zibaki zikinyanyasika kama
ilivyokuwa kwa Toto African iliyopigana hadi inashuka daraja.
Rai
yangu kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kamati ya Ligi ni kwamba, Simba
na Yanga zisiachwe kuharibu mapinduzi ya soka yanayoletwa na Azam TV.
HABARI
HII IMETOLEWA KATIKA GAZETI LA MAWIO, IMEANDIKWA NA ELIUS KAMBILI
Umemuandika aliyeongea lakini huku comment, najua anapingana wewe huyu, kila siku unataka timu zijitambud thamani yao sasa leo unaanza kuifananisha ashanti na simba, mil 100 ni nyingi sana kwa toto lakini kwa simba hazitoshi, mil 100 kwa mechi 26 ni kama mil 3.8 mshahar wa ngasa tu yanga kwa mwezi, nimemuelewa rage acha akomae
ReplyDeleteNawapongeza Azam kwa ha2a ambyo wamefiki lkn kwa simba na yanga ni haki yao kusikilizwa kama wanatka kiac kikubwa 2naona kwa mfano ligi ya Hispain madrid na barca wanapata zaid ya timu nyngne. sasa iweje simba uwalipe sawa na mgambo?
ReplyDeleteWewe Mwandishi ni mtabiri au unajaribu kutengeneza mazingira ili Yanga wakuunge mkono, kwa nini huongelei wakati mwingine hizi timu pia huwa zinapishana kwa maamuzi. kikubwa zaidi ulitakiwa uzungumzie hao simba waliokwisha toa tamko na kuielimisha jamii umma wa wapenda soka na kuwaomba viongozi wa Yanga watoe maamuzi ya busara badala ya kupinga kwani kuukubali mkataba huo ni hatua ya kuinua uchumi wa klabu hata kama ni kidogo kuliko kukosa kabisa. KAZI KUBWA YA MWANDISHI NI
ReplyDeleteKUELIMISHA
KUFUNZA
KUREKEBISHA
KUBURUDISHA
KUTANGAZA
kwa lengo la kukuza maendeleo hasa kwenye faida sio kundeleza uchochezi tena UNGETUMIA BUSARA KUWAOMBA SIMBA KAMA KWELI WANA NIA NJEMA WABADILI KAULI, msemaje wa Yanga yuko sahihi wanasubiri ipelekwe rasmi ndipo watoe kauli, sasa huo ndiyo wakati muafaka wa vyombo vya habari kutoa mafundisho mema kwa watu ambao pengine wanaweza kuwa na mtazamo potofu wa kupinga kila kitu. yeye huyo aliye kataa hizo kidogo ana mipango ye yote mbadala wa kuendeleza klabu. WAPUNGUZE SIASA AU WAACHE KABISA, KILA KITU NI HELA BORA UPATE KIDOGO KULIKO KUKOSA KABISA
Ndugu mwandishi asante kwa taarifa ila kwa upande mwingine ni kuwa Simba wako sahihi hawawezi kulipwa sawa na yanga au azam ambao ni mabingwa pia timu ndogo haziwezi kulipwa sawa na simba au azamu...la kufanya kwakuwa ndiyo azam wanalinaznisha ningependekeza kwanza timu zote zikubali mkataba ila kwa masharti kuwa dau litaongezeka kwa vigezo husika kwa timu hisika...kwani hiyo mil. mia moja timu kama yanga c wanaipata kwa mechi mbili tu...?
ReplyDeleteNI SWALA LA MAKUBALIANO NA KUELEMISHANA NA NAONA MWANDISHI UMESHAWAHUKUMU YANGA WAKATI MSEMAJI WA KLABU KATOA YA KWELI AU ULITAKA ATOE MAONI YAKE BINAFSI...? HUWA HATUENDI HIVYO TAARIFA RASMI INAKUJA.....WAHUSIKA WANAKAA CHINI NA BAADAYE MSEMAJI ANATOA MAAMUZI YA KIKAO KWA UMMA SIYO KUROPOKA TU..ULITAKA ASEJE NA BAADA YA KIKAO MAAMUZI YAKAWA TOFAUTI NA KAULI YAKE UTASEMAJE..?
Tru kaka ww ndo umejibu kisheria(beyond reasonable dought) yani hapo m2 hana wcwc tn na swala hilo,keep t up bro!hv ndo vichwa 2navitaka tz
ReplyDeleteJamani hata kampuni kubwa kama SuperSport zinatoa kiasi chini ya hapo...Nimetafiti Kenya na Zambia,nikaona kiasi anachotaka kutoa Azam ni sawa kabisa...Zambia wanapokea kama dola 39000 kwa mwaka,Kenya wanapata kama Tsh110mn.Kumbuka sio kila mechi itaoneshwa live.Tubishane kwenye mahesabu sio empty statistics!
ReplyDeletemil 100 kwa kila timu ni pesa ndogo sana kwa vilabu vyote. walipwe mechi ambazo watacheza azam tu tena hata hivyo haitoshi kabisa weka mezani bil 15.9 ili kila timu ichukue bil 1 kwa mwaka au cmba na yanga wachukue bil 1.5 kila moja vilabu vikubwa tena wachukue mil 800 kila moja tena cmba na zina brand kubwa tofauti na azam. mwandishi ka2mwa na azam azungumze kwa chapaaaaa
ReplyDeleteHizi timu za simba na Yanga ndo source ya kushuka kwa soka la TZ, yan akili za wachezaji wetu na hata mashabiki zinadumaa kwa sababu ya ushabiki hata ktk mambo ya msingi. Namshangaa sana mtu anaesemma hyo hela ni ndogo, mi sioni sababu ya kukataa hyo ofa, atleast wangeanza atleast kwa msimu mmoja halaf baadae ndo wacomment chochote. Hata hao Yanga watakataa, bcoz wao na Simba lao ni moja, sionagi tofauti yao. Mbona hyo hela ni nying kuliko anayochukua mshindi wa ligi kuu?. Mi naona hapo ni chuki tu, hawana reason kwa kwel
ReplyDelete