Search This Blog

Monday, April 15, 2013

RONALDO NA LIONE MESSI WAFUNGAJI BORA WA KIZAZI HIKI CHA SOKA WENYE JUMLA YA MABAO 500 NDANI YA LA LIGA

Namba huwa hazidanganyi. Mabao mawili ya Cristiano Ronaldo katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Athetic Bilbao jana jumapili yalimfanya mreno huyo kutimiza mabao 50 ndani ya msimu wa 2012-13, akifuata nyayo za mpinzani wake Lionel Messi ambaye tyari ameshatimiza idadi hiyo ndani ya msimu huu. Wachezaji hao wawili ndio wachezaji pekee kuweza kufika mabao zaidi ya 50 ndani ya msimu mmoja katika soka la nchi la Hispania - na wameweza kufanya hivyo ndani ya misimu mitatu mfululizo.

Messi hakuwepo kwenye mechi ya ushindi wa Barcelona dhidi ya  Zaragoza 3-0 pale La Romareda. Muargentina huyo amepewa mapumziko ili awee kuwa fiti zaidi kutokana na majeruhi ya nyama za paja aliyoyapata kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Champions League dhidi ya Paris Saint-Germain.

Lakini nahodha huyo wa Argentina tayari ameshafunga mabao 57 ndani ya msimu huu katika michezo 46 aliyoichezea Barcelona, na Ronaldo ameifikia rekodi ya mabao 50 jana usiku. 

 


MESSI & RONALDO: THE 50-GOAL SEASONS
Season
2010-11

2011-12

2012-13
Messi
53 goals

73 goals

57 goals
Ronaldo
53 goals

60 goals

50 goals
Ronaldo alifungua kitabu cha mabao kwa goli lake la haraka zaidi kwenye maisha yake ya soka, goli la faulo katika sekunde ya 71 ya mchezo, akishindwa kufikia rekodi ya goli la haraka zaidi la Xerez aliyefunga sekunde ya 45 mwaka 2009.

Kabla ya baadae hajawakatisha tamaa Athletic ambao walikuwa wanakuja juu kutafuta goli kwa goli la kichwa na hivyo kufikisha mabao 50 ndani ya msimu katika mechi 48.

Messi na Ronaldo walimaliza msimu wa 2011-12 wote wakiwa na mabao 53 (Leo katika mechi 55; Cristiano katika mechi 54). Muargentina alivunja rekodi ya Gerd Muller ya mabao 69 ndani ya msimu kwa kufunga mabao 73 msimu uliopita (ndani ya mechi 60), wakati Mreno Ronaldo alifunga mabao 60 katika mechi 55 msimu uliopita.

Katika msimu wa sasa,  Messi ameshafunga mabao 57, huku michezo saba ikiwa imebakia kwenye La Liga, huku kukiwa na uwezekano wa kuwepo kwa michezo mingine miwili au mitatu kwenye Champions League. Na kama Barca, Madrid wapo kwenye nusu fainali ya Champions League, hivyo Ronaldo ana karibia michezo 10 iliyobaki ndani ya msimu kwenye La liga na Champions League, huku akisubiri fainali ya Copa del Reymwezi ujao, ambapo Real watakutana na mahasimu wao wa mji mmoja Atletico Madrid katika dimba la Santiago Bernabeu.

Messi akiwa na miaka 25, tayari ndio mfungaji bora wa muda wote wa Barcelona akimpita mkongwe Cesar Rodriguez. Baba Thiago ana mabao 310 katika mechi 375 alizoichezea Barca. Kwa kiwango alichonacho hivi sasa kama ataendelea kuwa hivi ndani ya misimu mingine minne au mitano anaweza kufikisha mabao 500 akiwa na jezi ya Blaugrana.

Cristiano, akiwa na miaka 28, sasa anahitaji mabao manne ili kufikisha mabao 200 akiwa na jezi ya Real Madrid akiendelea kupanda juu kwenye listi ya wafungaji bora kabisa wa klabu hiyo. 

Anaweza hata kumpita mchezaji anayeshika nafasi ya tano Hugo Sanchez (Mwenye mabao 208 ) ndani ya msimu huu, wakati  Alfredo Di Stefano (308) na Raul (323) anaweza kuwafikia ikiwa ataendelea kuwepo Santiago Bernabeu kwa miaka miwili mengine.  Akiwa na mabao 196 kwenye  192 games, wastani wa mabao wa mreno huyo ni mkubwa kuliko wachezaji waliopo kwenye Top 10 ya wafungaji bora wa Real Madrid. Pia Ronaldo ameshaweka rekodi mpya ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi(11) kwenye ligi ya mabingwa ulaya ndani ya msimu mmoja.

Messi ameshasema mara kwa mara kwamba ataendelea kubaki Barcelona kwa miaka mingi na mashabiki wa Madrid wataendelea kuomba Ronaldo aendelee kubaki Bernabeu pia. La liga sasa sio tu ni nyumbani kwa vilabu vikubwa na tajiri zaidi duniani lakini pia ni nyumbani kwa wafungaji bora kabisa kwenye soka la miaka ya kizazi hiki.



1 comment: