Search This Blog

Tuesday, April 16, 2013

RAISI WA BAYERN MUNICH: LIGI YETU NI NYEPESI - NAHOFIA ITAKUWA KAMA YA SPAIN: LIGI YA TIMU MBILI

Raisi wa Bayern Munich Uli Hoeness anaogopa namna ligi ya Bundesliga ilivyokuwa rahisi wa upande wa klabu yake, na ana matumaini wapinzani wao wataweza kujizatiti ili kuwa na uwezo wa kupambana nao.  

Mabingwa hao wa Ujerumani walishinda ubingwa wao wa 23 huku kukiwa kumebakiwa michezo 6 ligi kumalizika na wamebakiza ushindi mmoja tu kufikia rekodi ya pointi nyingi iliyowekwa na Borussia Dortmund.
Vilabu hivi viwili vimekuwa vikitawala ligi ya Bundesliga kwa miaka kadhaa sasa, lakini Hoeness anaomba utawala wa vilabu hivyo viwili usije ukawa kama ule wa Barcelona na Real Madrid.

"Kumekuwepo ha hali ya uwepesi sana kwenye mechi zetu za ligi, upinzani umepungua sana, hatuwezi kuwa na furaha juu ya hilo," aliliambia jarida la Kicker. "Inabidi tufahamu nini chanzo cha tatizo hili na kulipatia ufumbuzi."

Bayern hivi karibuni waliipiga 9-1 Hamburg na wamekuwa wakishinda kwa mabao mengi bila nyavu zao kuguswa mara kwa mara - wakati timu inayoshika nafasi ya pili - Dortmund nao wakiipiga 6  Greuther Furth jumamosi iliyopita, wamefunga mabao 72 msimu huu, zaidi ya mabao 20 kwa timu inayomfuatia.

No comments:

Post a Comment