Search This Blog

Tuesday, April 16, 2013

FEDHA ZA WAWEKEZAJI WA KIARABU ZINAHARIBU USHINDANI KWENYE SOKA - DORTMUND

Ofisa mkuu wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke amesema watu kutoka mashariki ya kati(Uarabuni) na uwekezaji wao kwenye soka umeanza kuharibu ushindani kwenyes soka kwa kutumia mabavu ya fedha.
 
Maoni ya Watzke’ yanakuja siku siku kadhaa baada ya Dortmund kufanya miujiza kwa kufunga mabao mawili dakika za majeruhi na kuwatoa Malaga ambao ni timu inayomilikiwa na wamiliki kutoka Qatar na kuweza kuendelea kwenye nusu fainali ya Champions League wiki iliyopita. Pia Paris Saint Germain timu nyingine inayomilikiwa na waarabu ambao waliwekeza kiasi cha Euro 200 million katika usajili - walitolewa na Barca kwenye robo fainali.

“Hili suala la kuwekeza fedha nyingi sio la kiuana michezo na halipo sawa kwa vilabu vingine - mwisho wa siku biashara yetu ni michezo," This (big cash injections) is neither sportsmanlike nor fair and our core business is still sport,” Watzke aliliambia gazeti la  Handelsblatt. 

Watzke amekuwa akisifiwa kwa mabadiliko mazuri yaliyopelekea mambo kukaa sawa kwenye uchumi wa Dortmund ambao walikuwa wakikabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi kwenye miaka ya mwanzoni ya 2000 mpaka kufikia hatua ya kukaribia kutangazwa kufilisika. 
Ripoti ya kifedha ya Dortmund mwaka uliopita ilionyesha timu hiyo imeingiza fedha ya Euro 215.2 million kwenye msimu wa 2011-12 

No comments:

Post a Comment