Barcelona watajaribu kila mbinu iliyopo kwenye kitabu kujaribu kubadilisha matokeo ya 4-0 ya mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya klabu bingwa ya ulaya dhidi ya Bayern Munich kwenye mchezo marudiano hapo Jumatano wikii, raisi wa heshima wa Bayern Franz Beckenbauer ameonya leo jumatatu.
Bayern waliwanyoosha wahispania wiki iliyopita na kipigo cha kushangaza lakini Beckenbauer, mchezaji wa zamani, kocha na raisi aliyepata mafanikio kuliko wote katika historia ya Bayern, ameonya Barcelona hawapo tayari kupoteza mchezo huo.
"Barca watajaribu kila mbinu ili kuwatoa Bayern," aliliambia gazeti la Bild la Ujerumani. "Watatumia kila njia, chochote kinachoruhusiwa na kilichokatazwa. Watafanya hivyo sababu kujaribu kuilinda hadhi yao."
"Barca watajaribu kuwatoa Bayern mchezoni na mpnago ya vita vya mmoja mmoja. Wachezaji wa Bayern hawapaswi kuingia katika mapambano hayo - hawatokubali kufungwa kirahisi, watajaribu hata kuwachokoza, kufanya ushawishi wa maamuzi kwa refa pamoja na mbinu zote nyinginezo."
Hawa wajerumani ni viongozi wa mpira kweli kweli, hawa barcelona ndo tabia zao na marefa wanawabeba, nakumbuka matukio kama ya rvp fainali na matukio na mechi za chelsea wanabebwa sana, sasa wamekutana na watu wa pira lazima wafe tena
ReplyDeleteNi rais kiongoz
ReplyDelete