Search This Blog

Tuesday, April 16, 2013

MASHINE YA KUPIMIA UMRI YAZIDI KUDHIHIRISHA UONGO WA WAAFRIKA KWENYE KUDANGANYA UMRI - WACHEZAJI WA NIGERIA, IVORY COAST NA CONGO WATIMULIWA MICHUANO YA AFRIKA


Wachezaji tisa wameondolewa kwenye michuano ya mataifa  ya Africa chini ya umri wa miaka 17 yanayofanyika nchini Morocco baada kipimo cha kugundua umri kupitia kiganja cha mkono kuonyesha kwamba wan a umri mkubwa zaidi kuliko inavyopaswa.
Wachezaji watatu kutoka Congo-Brazzaville, Ivory Coast na Nigeria wamefungiwa kabisa kushiriki kwenye mashindano yoyote.
Mashine ya Magnetic Resonance Imaging (MRI) ilitumika kupima viganja vya wachezaji ili kujua ukweli wa umri wao.
Wachezaji ambao wameondolewa kwenye michuano hiyo ni kutoka Congo Cherlevy-Diabala Carim, Hardy Binguila na Bermagin Kangou, kutoka Ivory Coast  ni Dagou Britto, Abdul Diarrassouba na Siriki Dembele, na kutoka Nigeria ni Onyinye Ndidi, Ibrahim Abdullahi and Emmanuel Asadu.
Vikosi vya timu zote tatu vimepunguzwa mpaka kufikia wachezaji 18.
FIFA walianza kufanya utafiti wa umri wa wachezaji kwa kutumia technolojia ya MRI mwaka 2003 lakini wakaanza kuifanyia majaribio machine hiyo kwenye michuano ya U-19 World Cup in Nigeria.
Matokeo ya vipimo kwenye michuano ya kombe la dunia U-17 kuanzia 2003, 2005 na 2007 yalionyesha kwamba asilimia 35 ya wachezaji walikuwa wamezidisha umri unaoruhusiwa.

1 comment:

  1. Wababaishaji wakubwa hao. Sisi si tuliwakatia Congo rufaa? Wanatulipaje na wameprove ni vijeba?

    ReplyDelete