Mashabiki wengi wanaofuatilia kiundani mchezo wa soka jana walishangazwa sana na kitendo cha klabu ya Real Madrid kucheza mechi yao ya raundi ya pili ya robo fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Galatasary iliyofanyika nchini Uturuki bila kuwa jina la logo ya mdhamini jezi za timu hiyo - BWIN.
Katika mchezo huo ambao Madrid waliweza kusonga mbele pamoja na kufungwa 3-2, hawakuvaa jezi zenye nembo ya mdhamini wao - kampuni ya kucheza kamari ya BWIN kwa sababu inapotokea wanacheza mechi kwenye nchi ambayo hairuhusu shughuli zozote za mchezo wa kamari basi huwa wanaacha kuvaa jezi zenye nembo ya wadhamini wao.
Uturuki ni moja ya nchi ambazo haziruhusu michezo ya kamari na hivyo promotion zozote za kutangaza mambo ya yanayohusiana na kamari.
No comments:
Post a Comment