Wakati kwenye viwanja vingine vyote duniani fremu za nje zinazonguka uwanja zimekuwa zikitumika kama vitega uchumi kwa wamiliki wa uwanja husika, hali ni tofauti mkoani Kigoma kwenye dimba la Lake Tanganyika. Uwanja huo mkongwe ambao unaingiza mashabiki takribani 20,000, upo kwenye hali mbaya kuanzia ndani mpaka nje. |
Matokeo yake uwanja huo mkubwa wa mkoa umezidi kuwa kwenye mazingira mabovu, na inawezekana ukosefu wa mapato ya milangoni kutokana na kutokuwepo kwa mashindano ya maana ya kuvuta washabiki kuingia uwanjani hivyo kuzidi kusababisha ukosefu wa fedha za kuweza kuboresha mazingira ya uwanja huo.
Asante mdau kwa kutuletea vituko hivyo! Jambo la kujiuliza je kuna viongozi wa michezo kweli ngazi ya mkoa?kama wapo ndio kusema hawalioni hilo? Au wanaona sawa tu bora watoto hawakosi kwenda maliwato.Mapinduzi ya michezo yanahitaji watu wenye miono ya mbali.kuweni makini mnapofanya chaguzi !!!!
ReplyDeletejitihada zifanyike ccm irudishe viwanja serikalini sababu wakati wa ujenzi wa viwanja hvyo nchi ilikua na chama kimoja
ReplyDeleteMimi sijui uwanja huu unamilikiwa na Serikali Chama au Mtu Binafsi, Insikitisha kuona Mkoa Kama wa Kigoma wenye heshima ya kutoa wachezaji Bora hapa nchini unakua katika mazingira ya hovyo kiasi hiki, lawama ziende wapi chama serikali au chama cha mpira. Ttanzania ni nchi ndogo sana lakini tumeona Brazil Ivory cost an nchi zingine zikija kucheza Taifa kwa nini??. kwa sababu Tanzania tuna uwanja wenye kiwango. Sasa hata kama Kigoma hatuna timu ligi kuu lakini kama kuna uwanja wenye ubora ni rahisi kualika timu kubwa kama samba yanga azam na zingine na zikakubali kuja Kigoma kama brazil walivyokubali kuja Bongo. Viongozi wa Mkoa serikali chama tawala na Chama cha mpira achenu blah blah na Fitna anagalieni hilo.
ReplyDeleteJunior Mwamba
sasa fika pale kigoma kwenye chama cha soka jaribu kuwauliza kuhusu michakato mbalimbali ya TFF, watu watazungumza mpaka povu mdomoni jinsi mambo yanavyoendeshwa ndivyo sivyo, hlf tutegemee mjumbe kutoka huko nae anakuja dar kutuchagulia viongozi wa TFF!!.
ReplyDeleteNdio maana tunataka mabadiliko katika uongozi wa mpira kuanzia Taifa yaani TFF hadi mikoani hii ni Aibu ya karne.Wao kazi ya kusingizia FIFA na serikali kuingilia ulaji wao.Makato kibao hela haijulikani inakopelekwa huku kocha na timu ya Taifa wanashindwa hata kuwalipa posho.DAWA YAO NI KUWAPIGA CHINI TU WOTE
ReplyDeleteHv lake tanganyika unachukua wa2 20000 au 60000
ReplyDeleteDuuh! Noma kweli kweli.! Mdau
ReplyDeleteKIGOOMA LEKA WATIGITE!!!!!!!!
ReplyDelete