Search This Blog

Monday, March 18, 2013

UBUTU WA TEGETE, KAVUMBAGU, NA BAHANAUZI WAMENIFANYA NIMCHEZESHE NIZAR KAMA MSHAMBULIAJI - ASEMA KOCHA WA YANGA

KOCHA wa Yanga, Ernie Brandts ameeleza sababu za kumchezesha Nizar Khalfan kama mshambuliaji wa kati ni ubutu wa safu hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mholanzi huyo alisema alifanya maamuzi hayo magumu baada ya kuchoshwa na washambuliaji butu Jerry Tegete na Didier Kavumbagu.
Tegete na Kavumbagu ambao walikuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi cha Yanga wameshuka dimbani mechi tatu  bila kufunga bao lolote.
Kitu ambacho kimemlazimu Mdachi huyo kufanya maamuzi magumu kumwamini Nizar aliyekuwa mchezaji wa akiba na kumpa jukumu la kuongoza mashambulizi kwenye kikosi chake.
"Nimelazimika kufanya mabadiliko baada yakuona kuna tatizo sugu la ufungaji."
"Tegete na Kavumbagu naweza kusema wanashindwa kufanya yale ambayo nawatuma uwanjani."
"Sababu ambazo zinanifanya nishindwe kuwaamini kwa sasa." alisema kocha huyo.
Hata hivyo, alisema mabadiliko aliyoyafanya kuwachezesha Nizar Khalfan na Hamis Kiiza katika nafasi ya ushambuliaji  badala ya Tegete na Kavumbagu yameonyesha tofauti kubwa.
"Kwa ujumla walicheza vizuri na kufuata maelekezo yangu. Hata goli ambalo Kiiza alifunga lilitokana na juhudi binafsi za Nizar."
Nizar alimvisha kanzu kipa wa Ruvu, Benjamin Haule aliyetoka langoni kuokoa hatari hiyo naye Kiiza akafunga kwa kichwa huku lango likiwa wazi.

3 comments:

  1. Hata kama hakufunga Nizar alikuwa serious, anafanya vitu vya msingi tu uwanjani, alikuwa hatari sana akiwa na mpira na na kama hana mpira, jamaa ni professionall kweli kweli, touch zake si mchezo. apewe michezo zaidi huyu ndio atatupa ubingwa mapema. nikaanza kufikiri kuwa kuna mechi stars zinamuhitaji huyu jamaa, maana wale watoto kuna kuna kipindi wanakosa mchezaji mwenye maono zaidi

    ReplyDelete
  2. nadhani Nizar atarejea kwenye kiwango chake na kuisaidia sio tu yanga bali Taifa Stars, kuumia kwake kwenye mechi dhidi ya Ruvu Shooting kulishtua mno na kutukosesha raha, jamaa anajua mpira kwa kweli.

    ReplyDelete